Uchaguzi wa Marekani ndiyo huamua hatima ya Dunia

Uchaguzi wa Marekani ndiyo huamua hatima ya Dunia

Allen Kilewella

JF-Expert Member
Joined
Sep 30, 2011
Posts
21,470
Reaction score
40,593
Zikiwa zimebakia siku mbili ili uchaguzi wa Marekani ufanyike, Dunia nzima imeshika pumzi ikitafakari nini kitatokea Marekani.

Dunia nzima imegawanyika makundi mawili. Kundi la kwanza ni lile linalotaka Donald Trump ashinde na kundi jingine linalotamani Kamala Harris ashinde.

Pande zote mbili zinazotamani mgombea kati ya hao wawili ashinde, zina maslahi yake ikiwa mmojawapo wa wagombea hao atachaguliwa.

Soma Pia: Yanayojiri kuelekea Uchaguzi Mkuu Marekani 2024: Nani kuibuka kidedea?

Kwa sasa, uchaguzi wa Marekani ndiyo uchaguzi pekee duniani unaoamua hatima ya Dunia.
 
Demokrasia ndio inatakiwa iibuke mshindi sio mtu anasema akishindwa hatokubali kushindwa.
 
Utake usitake uchumi wa Marekani unaathiri bakuli la mboga mezani kwako! Utaniuliza kivipi? Ni kwasababu kila bidhaa ya kigeni kutoka nje inanunuliwa kwa Dollar ya Mmarekani! Uchumi wa Marekani ukiimalika thamani ya Dollar nchini kwako inaimarika (Dollar haipandi). Uchumi wa Marekani ukishuka au kuyumba kitu cha kwanza kufanya ni kupandisha thamani ya Dollar hivyo huwe na uhakika thamani ya hela yako (local currency) itashuka sana na Dollar kupanda sana kupelekea ugumu wa maisha kiasi cha kutoweza kumudu hata kilo moja ya nyama! Anayeongoza uchumi wa dunia muogope sana!
 
ndio ni uchaguzi wenye athari fulani fulani lkn si kwamba ni kama pumzi ya uhai ya kwamba unatupa kula,kunywa n.k
sidhani kama neno "hatima ya dunia" limetumika vyema hapa labda kama limebadilishwa maana!
Bisha tu lakini huo ndiyo ukweli. Ni nchi gani duniani itabakia salama kama Marekani kutakuwa na utawala wa hovyo?
 
Utake usitake uchumi wa Marekani unaathiri bakuli la mboga mezani kwako! Utaniuliza kivipi? Ni kwasababu kila bidhaa ya kigeni kutoka nje inanunuliwa kwa Dollar ya Mmarekani! Uchumi wa Marekani ukiimalika thamani ya Dollar nchini kwako inaimarika (Dollar haipandi). Uchumi wa Marekani ukishuka au kuyumba kitu cha kwanza kufanya ni kupandisha thamani ya Dollar hivyo huwe na uhakika thamani ya hela yako (local currency) itashuka sana na Dollar kupanda sana kupelekea ugumu wa maisha kiasi cha kutoweza kumudu hata kilo moja ya nyama! Anayeongoza uchumi wa dunia muogope sana!
Umemaliza 100%✓
 
Back
Top Bottom