Mohamed Said
JF-Expert Member
- Nov 2, 2008
- 21,967
- 32,074
UCHAGUZI SERIKALI ZA MITAA MZIMUNI YAMEJIRUDIA YA MWAKA WA 2020
Nimefika kituoni kwangu Magomeni Mapipa Shule ya Mzimuni kupiga kura saa tatu asubuhi na nilikutana na vurugu.
Kulikuwa na shutuma kuwa kuna kitabu cha wapiga kura kimeghushiwa na kuna watu wanalazimisha kitumike.
Wakati nateremka kwenye gari mtangazaji mmoja wa kituo cha TV akawa kaniona na akaja kunisalimu.
Anafika kwangu na mlalamikaji wa kitabu kilichodaiwa kughushiwa anafika akamwambia huyu kijana wa TV, "Ukimaliza kuzungumza na Mohamed njoo huku tukuonyeshe kitabu kilichoghushiwa kilichopenyezwa katika uchaguzi."
Nilipofika mlangoni kuingia chumba cha kupiga kura tayari chumba cha jirani watu walikuwa wanataka kuingiana maungoni.
Nimeingia ndani kupiga kura lakini sauti za vurugu nikawa bado nazisikia nje.
Nimeondoka kituoni nimeacha vurugu.
Ningeweza kuandika mengi niliyoelezwa na wagombea na wapiga kura kama mimi wa mtaa wangu lakini hii video inazungumza maneno 1000.
Inatosha kueleza yote.
Bado tunasafari ndefu.
Kiongozi aliyeingizwa madarakani kwa ghushi hana hadhi wala heshima na hawajibiki kwa yeyote kwa kuwa hakuchaguliwa na yeyote.
Ghushi ni jinai tusipuuze.