MSEZA MKULU
JF-Expert Member
- Jul 22, 2011
- 3,763
- 5,607
Huyu mbabe hapo juu anaitwa CHARLES D.B KING
Katika uchaguzi unaoitwa wa kidemokrasia 1927 nchini LIBERIA jamaa alimshinda mpinzani wake THOMAS J FAULKNER kwa kura zilizokuwa nyingi kuliko idadi ya watu waliojiandikisha.
Watu waliojiandikisha walikuwa 15000, Mbabe huyu akajishindia kiti cha urais kwa kura 240,000 huku mpinzani wake akijichukulia kula 9000. Huu ulikuwa uchaguzi wa mara ya tatu jamaa akitetea kiti chake, kwa kituko hiki Jamaa aliingizwa kwenye record za dunia.
Tusishangae kwa nini Afrika ni vigumu kumtoa mtu ambaye Tayari ni Rais na anatetea kiti chake.