SoC02 Uchakataji mafuta ya parachichi

SoC02 Uchakataji mafuta ya parachichi

Stories of Change - 2022 Competition

Zulu Man Tz

Member
Joined
Sep 23, 2020
Posts
73
Reaction score
99
WAZO LA UCHAKATAJI WA MAFUTA YA KUPIKIA KWA KUTUMIA TUNDA LA PARACHICHI.


UTANGULIZI
.
Kutokana na uhaba wa mafuta ya taa, gesi asilia, petroli na diseli Ulimwenguni kote iliyosababishwa na oparesheni ya kijeshi ya Nchi ya Urusi kuishambulia nchi ya Ukreini mnano tarehe 24.2.2022. Wakati mzozo wa Ukraine umeanza kuleta athari kwa bei ya mafuta, Waziri wa Mambo ya Nje wa Ukraine Jumamosi Februari 26 mwaka huu ametoa wito kwa nchi za Magharibi "kuweka vikwazo kwa mafuta ya Urusi". Lakini hatua kama hiyo "haiwezi kutekelezwa", kwa sababu Urusi ni nchi ya pili kwa kuuza mafuta ghafi nje ya nchi, ikitoa 11.5% ya usambazaji wa mafuta, kulingana na Pierre Terzian, mtaalam wa maswala ya mafuta. Kupanda kwa bidhaa hiyo ya mafuta kumepelekea kupanda kwa bidhaa pia muhimu za chakula katika soko la Dunia kama vile Ngano, mahindi, mafuta ya kupikia na Sukari.

Kutokana na athari tajwa apo nitajikita zaidi katika tatizo la uhaba wa mafuta ya kupikia katika nchi ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, nikipendekeza nini kifanyike ili kupunguza ukali wa maisha wa mtu mmoja mmoja nchini na hivyo basi ata kutengeza ajira mpya kwa vijana. Hili wazo kama likitekelezwa itasaidia kukuza Uchumi wa nchi yetu na pato la taifa kwa ujumla.


UPATIKANAJI WA PARACHICHI.
Tanzania ni Nchi iliyobarikiwa katika uzalishaji wa matunda ya parachichi, Nyanda za kusini magharibi Kwenye mikoa ya Mbeya, Njombe, Songwe na Iringa. Vivyo hivyo Nyanda za kaskazini mashariki mwa Nchi Kwenye mikoa ya Tanga, Arusha na Kilimanjaro hii ni mikoa maarufu katika ulimaji na uzalishaji wa tunda la parachichi kwa ajili ya biashara. Bei ya mashambani kwa ujumla ni wasatani Tsh 30,000-45,000/= kwa gunia moja la Kilogramu 100.


UANZISHWAJI WA KIWANDA.
Ili kupunguza mlipuko wa bei ya mafuta ya kupikia kutokana na uhaba wa malighafi ya bidhaa hiyo, napendekeza uanzishwaji wa viwanda vya ndani vya kuchakata mafuta kutokana na matunda ya parachichi yanayozalishwa katika mikoa tajwa hapo juu. Gharama za mwanzo za kuanzisha kiwanda kimoja ni Tsh. 420,000,000/= hii inajumuisha gharama za mitambo ya uchakataji parachichi. Gharama za kununua kiwanja, ujengaji wa kiwanda pamoja na leseni ya biashara itategemeana na thamani ya ardhi katika mkoa husika. Serikali na mashirika binafsi wanaweza wakachukua hatua madhubuti katika kuona fursa Kwenye hili wazo. Kutokana na shirika la utafiti la kilimo na ufugaji nchini Kenya (KARLO) mnamo 2016 inasema Kilogramu 10 za parachichi inaweza ikachakata wastani wa lita 4 mpaka 7 za Mafuta kulingana na ubora wa Parachichi.


MPANGILIO WA UCHAKATAJI MAFUTA.
Uoshwaji wa Parachichi; Usafishaji wa Parachichi kwa maji safi na salama kwa kutumia vinegar inasaidia kupunguza athari za dawa za kuulia wadudu zilizopulizwa kwenye mimea hiyo kwa binadamu kama vile madhara kwenye mfumo wa upumuaji, uzalishaji, na magonjwa ya moyo.
Ukatwaji na usagaji wa Parachichi; Kwa kutumia mitambo maalumu ya kufanya milling itapasua maparachichi kuwa vipanzi vidogo vidogo sana.

Ukandamizwaji wa vibanzi vya parachichi; kwa kutumia mgandamizo mkubwa wa presha wa takribani 45-55Mpa ambapo mafuta ghafi yatazalishwa, hii hufanywa na kifaa cha "hydraulic press machine".
Uchujaji wa Mafuta ghafi ya mwanzo; Mafuta ghafi ya mwanzo yanakuwa na uchafu hivyo uchujwaji wake unachochea usalama kwa asilimia 70%.

Utakatishwaji na kupanga bidhaa kwa makundi; Utakatishwaji inaongeza usafi wa Mafuta kwa asilimia 99.8% hivyo huwezesha bidhaa kuwa tayari kwa matumizi na kuimarisha afya ya mtumiaji. Baada ya utakatishwaji ni kupanga bidhaa kwa makundi kwa ajili ya kusambazwa kwa wadhabuni.


MAKADIRIO YA MAUZO.
Kiwango kidogo Cha kiwanda Cha uzalishaji wa mafuta kwa wiki ni lita za ujazo 1000 ambazo zitatumia takribani Tani 1.4 za parachichi Kwenye uchakataji. Gharama ya uzalishaji wa lita 1 kiwandani ni Tsh 4500/= ambayo italeta makisio ya mauzo ya Tsh.5,000,000/= kwa wiki.


KUTENGEZA AJIRA KWA VIJANA.
Kwa ujumla kiwanda kimoja Cha uchakataji kitatoa ajira za kudumu 30 kwa vijana na ajira 15 za muda mfupi, haya ni makisio ninavyoyaona. Kutokana na ajira hizo serikali itapata kodi ambayo itatumika Kwenye miradi mbali mbali ya maendeleo.

SOKO LA MAFUTA YA PARACHICHI.
Mahitaji Makubwa ya bidhaa hii ni Wananchi kwa ajili ya matumizi ya nyumbani, pili ni kwenye mahoteli, kumbi za starehe na migahawani na tatu mashuleni hasa shule za bweni na vyuoni. Pia kama bidhaa itapenya zaidi Kwenye soko la ndani basi tutaweza kufikiria kuudha mafuta ya kupikia ya parachichi kwenda nchi za nje.

ATHARI ZA BIASHARA.
Kutofikia Lengo la Mauzo kwa mwezi; Hii husababishwa na wadhabuni kutorejesha mauzo kwa wakati na vile vile matangazo ya bidhaa hiyo kuwa hafifu.

Tatizo la umeme; Umeme hafifu kiwandani inaweza sababisha tusifikie malengo ya kuchakata mafuta kwa idadi tutakayojipangia kwa mwaka. Pia umeme ukikatika sana unahatarisha usalama wa mitambo yetu.

Kupanda kwa bei ya Mafuta ya petroli; Baadhi ya mitambo inatumia Mafuta ya petroli kwenye uendeshaji wake hivyo kutapelekea gharama za uzalishaji kuwa juu, ila endapo serikali ikiendelea kutoa ruzuku itapunguza athari ya gharama kubwa ya uendeshaji mitambo.

Mapato ya vyanzo vya Uzalishaji mali kuwa chini ya mtaji wa wawekezaji; Vyanzo vya Uzalishaji mali na mtaji wa wawekezaji ukiwa chini husababisha mauzo ya bidhaa hizo kupungua kwa Kasi.

WASHINDANI WAKUBWA WA UCHAKATAJI WA MAFUTA YA KUPIKIA.

Wafuatao ni viwanda ambavyo vipo Kwenye ushindani wa kibiashara katika soko la bidhaa sawa za Mafuta ya kupikia nchini Tanzania ;

Murzah oil mills limited iki kiwanda kimeanzishwa mnamo mwaka 1997, hiki kiwanda kinapatikana Kipawa,Dar-es-salaam.

MeTL Group subsidiary East Coast Oils and Fats iki kiwanda kimeanzishwa mnamo nwaka 2006 hiki ni kati ya viwanda vikubwa barani Afrika.

Sanrich sunflower cooking oils hiki kiwanda kinapatikana Kijitonyama, Dar-es-salaam.

UHALISIA KATIKA TASWIRA.
Zifuatazo ni picha ambazo zinaonyesha uhalisia wa kiwanda Cha uchakataji Mafuta kitakavyokuwa, chanzo Cha picha hizi ni kutoka Kwenye mtandao wa Find quality Manufacturers, Suppliers, Exporters, Importers, Buyers, Wholesalers, Products and Trade Leads from our award-winning International Trade Site. Import & Export on alibaba.com
Screenshot_20220701-085951.jpg



Nakala hii imeandaliwa na Ndugu ;
DEOGRATIAS MAJALIWA CHIKEPA,
Shahada ya uhasibu mwaka wa II wa masomo,
Kutoka Chuo Cha Elimu ya Biashara (CBE), Dar-es-salaam,
Namba za simu; +255 -7576 -114- 15,
Barua Pepe; chikepamajaliwa@gmail.com.
 

Attachments

  • Screenshot_20220701-090119.jpg
    Screenshot_20220701-090119.jpg
    14 KB · Views: 28
Upvote 3
Wazo zuri ishu kwenye mtaji
apo ndio changamoto iliyopo mkuu serikali haina uaminifu sana kutoa mikopo ya uendeshaji biashara kwa vijana na kipaumbele kinatoka sana kwa wawekezaji wa nje kuanzia ulimaji mpaka uchakataji wa mazao.
 
apo ndio changamoto iliyopo mkuu serikali haina uaminifu sana kutoa mikopo ya uendeshaji biashara kwa vijana na kipaumbele kinatoka sana kwa wawekezaji wa nje kuanzia ulimaji mpaka uchakataji wa mazao.
Kwan hizo mashine ni shingap znauzwa?
 
Back
Top Bottom