Determinantor
Platinum Member
- Mar 17, 2008
- 59,045
- 94,974
Wakuu Umofia Kwenu! Yajayo yanaumiza!
Nimesoma taarifa iliyokua kwenye Gazeti la Tanzanite na Nimevumilia lakini Nikaona nifanye uchambuzi Wenye hoja chache tu. Hoja hizi zinaongozwa na Uzalendo na sio Ukada wala Ukamanda. Nitashukuru kama wote tutakaosoma Mjadala huu tutasimama kwenye misingi hio pia. Picha yeye Tarehe na kichwa cha Habari nimeambatanisha hapa chini.
Tanzanite "CHADEMA wajifunza Ujasusi Libya"
Gazeti hili limeandika vyema kabisa lakini mambo Kama haya yanahitaji kutolewa ufafanuzi na Vyombo husika ili kulinda hadhi ya nchi, baadhi ya athari ya hoja Kama hizi zimebebwa hapa chini.
Moja, kauli Kama hizi zinaweza kuleta utata au mgogoro wa Kidiplomasia Kati ya nchi na nchi. Kwa Vyombo husika kutokukemea jambo hili basi huenda watu wakaamini kuwa Ubalozi wa Libya nchini Tanzania na Libya kwa ujumla inahusika kuihujumu Tanzania. Kwa kuwa hadi Leo hii taarifa hii haijakanushwa, je Itakua ni Sahihi kwa Wageni wengine kuamini jambo hili? Leo hii Libya ikitutaka kutoa vielelezo tutakua na ushahidi? Tutaishia kwenye mgogoro mkubwa wa Kidiplomasia.
Pili, Athari Za Kiuchumi kwa Taifa zaweza kuwa mbaya kutokana na Gazeti hili kuwajengea Picha mbaya Wawekezaji kuwa Tanzania ina magenge ya kijasusi au Kwa maneno mengine Tanzania sio nchi rafiki Kwa ajili ya Wawekezaji na Wadau wa kibiashara au conclusively kuwa Usalama wa Tanzania ni mdogo. Hadi Leo hii, hakuna chombo chochote cha kiserikali kilichotoa tamko kuhusu jambo hili, maana yake ni kwamba tumekubaliana na jambo hili, tutawafukuza watalii na Wawekezaji, trust me!
Tatu, Je, tuna Jeshi dhaifu? Ndio, maana kwa mujibu wa article hio ni kwamba Jeshi na Vyombo vyetu vya kiintelijensia vimeshindwa Kutambua jambo hili na kulidhibiti hadi sasa jambo hili linaporipotiwa na Gazeti lenye Usajili halali wa Serikali. La, jeshi letu sio dhaifu basi tungeweza kudhibiti Majasusi hayo nasema.
Suala la Nne, ni uhalali wa taarifa hii! Je imelenga kujenga au kubomoa? Naam, kwa juu juu utaona lengo la Mwandishi ni kuichafua CHADEMA lakini ukweli Katika muktadha huu, tumeichafua nchi.
Suala la tano, kwa kuweka picha ya Wangwe na Ben Saanane tunalenga nini? Tunaziumiza familia za Wapendwa Watanzania WENZETU waliopoteza ndugu zao. Hao ni Akina Baba, ni Wajomba, Marafiki, Wazazi wa Watanzania WENZETU. Leo hii ukikuta picha ya Mpendwa wako ambaye ametoweshwa hujui alipo, unaikuta kwenye ukurasa huo utajisikiaje? Huu ndio uzalendo wetu? Huu ndio Utanzania wetu? Kumbuka, Likimpata mwenzao na wewe Muda wako Utafika.
Ikitokea Mwekezaji, Mfanyabiashara au mtu mwingine yoyote akatekwa, akashambuliwa, akavamiwa basi mtu atakayekuwa amesoma taarifa ya Gazeti hili Kwa Jicho la tofauti Kamwe hataweza kufikiria CHADEMA Bali Serikali nzima.
Kumbuka, huko Duniani hakuna CCM wala CHADEMA Bali kuna Tanzania, ni vyema Sana tukadhibiti haya mambo kungali mapema maana tutakimbiwa na Potential Investors!! Ni investor gani atakuja kuwekeza kwenye nchi yenye Usalama mdogo na Majasusi kibao?
Wakati tukidhani tunaiumiza CHADEMA tuifikirie na Tanzania. I stand to be correct.
Elli
Kijito Upele - Zanzibar