Richard
JF-Expert Member
- Oct 23, 2006
- 15,692
- 23,038
Habari za mwisho wa wiki wadau na kheri ya mwaka mpya.
Lakini kwanza nitie angalizo kwamba mie si mwanachama wa chama chochote bali ni mtaalam tu niliejifunza kufanya chambuzi na mambo mengine khasa ya kimataifa zaidi. Hivyo kuna wakati najikuta naangalia kinoendelea hapahapa nchini mwetu na jana nikaangalia kumbe CCM wamefanya mambo kadha wa kadha huko Dodoma.
Sasa nipo hapa Kibaigwa na naangalia masuala kadhaa yanoendela duniani na naona jinsi Russia inavyojinyakulia maeneo huko Ukraine huku nchi za magharibi na Marekani wakiandaa kauli mbalimbali za kusema juu ya hilo (la ushindi wa Russia).
Mara paap, naona CCM imewasilisha hoja kupitia mjumbe wa NEC Adam Kimbisa kwamba Mwenyikiti wa CCM na raisi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Hassan awe mgombea pekee wa CCM kwa upande wa Tanzania Bara na raisi wa Zanzibar mheshimiwa Dr Hussein Mwinyi awe mgombea wa CCM kwa upande wa Zanzibar!
Ni jambo ambalo limefanywa bila kufuata taratibu za kawaida kwa CCM kupendekeza majina kadhaa na kisha wajumbe wa NEC kupigia kura majina hayo na kisha majina kuchujwa na kubaki majina matatu ambayo hupelekwa kwenye kikao cha kamati kuu ya CCM yaani "Central Commitee" ambayo kwa CCM CCM hiyo yaweza kuwa na majina ya ziada ambayo huweza kupitishwa endapo kwatokea jambo la dharura.
Ni dhahiri kila mmoja wetu akumbuka uzuri jambo lilotokea Dodoma mwaka 2015 na upatikanaji wa jina hayati John Magufuli ambae baadae alimteu raisi Samia kuwa mgombea mwenza kwa upande wa CCM badala ya Dr Hussein Mwinyi ambae ndie aliekuwa amependekezwa na hayati Magufuli mwenyewe, hiyo ikiwa ni baada ya wazee wa kamati kuu kuingilia kati na kumshauri hayatoi Magufuli amteue Samia Hassan kuwa mgombea mwenza.
Hii ya kumteua Samia Suluhu Hassan kuwa mgombea mwenza, Hayati Magufuli aliizungumzia baada ya uteuzi wa wagombea badala ya jina la Dr Hussein Mwinyi (ambae ndie aliekuwa chaguo lake hayati Magufuli) na video yake ipo You Tube.
Lakini kwanza ni jambo la uzuri tukiangalia kilicho nyuma la hili la leo la CCM kumchagua Steven Wassira mzee wa umri wa miaka 80 kuwa makamu mwenyekiti wake. tawasema "background".
Ni baada ya kuondoka kwa mzee mwingine Abdulrahman Kinana ambae aliomba kuachia nafasi hiyo. Kinana ndie aliekuwa meneja wa kampeni wakati wa uchaguzi wa 2015 na kutokana na uwezo wake mkubwa (ni mstratejia mahiri) na uwezo mkubwa kusuka mitandao ndani ya nje ya CCM, chama hicho kilishinda uchaguzi huo kwa mbinde.
Ni dhahiri kwamba tangia kuondoka kwa Kinana, nyuma ya paza CCM imekuwa ikiangalia namna ya mfumo wake wa kuteua watu utavyowasaidia kumpata mtu sahihi wa kukabiliana na kuibuka kwa Tundu Lissu ndani ya Chadema ambae amejitokeza kugombea nafasi ya uenyekiti. Ni dhahiri pia kuwa wachambuzi wa siasa ndani ya CCM wamebaini mapungufu kadhaa kwa CCM dhidi ya Chadema khasa kanda ya Ziwa ambako bado kifo cha hayati John Magufuli chawatatanisha sana.
Kikiwa chama dola kama kinavyojiita CCM kwa miongo kadhaa kimejikita ndani ya dola zake tatu yaani serikali za mitaa, serikali ya Muungano na dola ya serikali ya mapinduzi Zanzibar. Akidhihirisha haya katika hotuba yake ya kukubali nafasi hiyo, makamu mwenyekiti mpya Steven Wassira amesema kuwa CCM ina majukumu makubwa mawili, kwanza ni kushika dola kwamba wamemaliza jambo la serikali za mitaa na kwamba hilo halina mjadala. kilobakia ni kugombea kushika dola la Muungano yaani uchaguzi wa raisi wa Bara na uchaguzi wa raisi wa Zanzibar.
Kwanini Steven Wassira?
Steven Masatu Wassira aliingia TANU mwaka 1959 na kadi yake alipewa akiwa na umri wa miaka 16. Mzee Steven Wassira ni mwanasasa mkongwe, mwanafunzi mzuri wa hayati baba wa taifa Mwalimu Nyerere na waziri wa zamani katika serikali zote ya awamu ya kwanza hadi ya tano. Pia mzee Wassira amesomea uchumi na utawala hivyo anafahamu namna ya kutawala watu ingawa ni katika mtindo wa kimamlaka zaidi (authoritarian) kuliko katika kusikiliza ukosoaji toka pande zingine. Kwa sifa hizo ni dhahiri mzee Wassira ameteuliwa kuwa makamu mwenyekiti ili kumsaidia mwenyekiti wa chama Samia Hassan katika kujibu hoja za upinzani khasa majukwaani na katika mijadala mbalimbali ambayo mzee Wassira amekuwa akijitokeza kushiriki.
Ni wazi katika kampeni za mwaka huu katika kukabiliana na kinoonekana kuja kwa mwenyekiti mpya wa Chadema, CCM imetumia mfumo wake wa ndani ya kukabiliana na matishio ya ndani na nje unoweza kuitwa "Hybrid Emergence Rotation System" ambao ulitengenezwa ili kuweza kuchagua watu kadhaa ndani ya chama wakati wa dharura au wakati wa kawaida na kilofanyika juzi ni kumteua mzee Wassira kwa dharura iliyopo ya kukikabili Chadema na kuhakikisha Samia Hassan anakuwa raisi kwa namna yoyote ile.
Katika mazingira yoyote yale ya kisiasa na kiutawala ni lazima kutakuwepo kwa mifumo kadhaa ya kutambua athari (Risk Assessment) na CCM imetumia ipasavyo mifumo hiyo kutambua athari kadhaa zinotokana na yale ambayo Chadema inafanya kwa sasa. Ni dhahiri kwamba Chadema imejikita zaidi katika mitandao ya kijamii na majukwaani lakini pamoja na vuguvugu na sekeseke la kumpata mwenyekiti mpya baada ya Freeman Mbowe CCM nayo imekuwa kimyakimya ikijiandaa kwa uchaguzi wa mwaka huu wa 2025.
Sasa ni athari zipi zingine ambazo CCM imezitambua na yakabiliana nazo kwa sasa?
Hizi ni twaita kwa kiingereza "managing risks".
1. Watu kutekwa kupotea na kuuawa. Hii pamoja na kuonekana kwamba watu watekwa na kupotea na kisha kuuawa kama yalotokea kwa mzee Ali Kibao, bado vitendo hivyo vya utekaji vimeonekana kuendelea na serikali kuendelea kukaa kimya na wiki ilopita mwanaharakati Maria Tshesai Sarungi alitekwa kwa muda na baadae kuachiwa huko Naironi nchini Kenya. Hii athari bado CCM haijaweza kuitambua yafanywa na akina nani khasa iwe nai TISS, Polisi maalum au vikundi kadhaa visivyoshikamana na upande wowote.
2. Athari ya matumizi ya mitandao ya kijamii ni athari ingine kubwa kwa CCM kwani Amos Makala ambae ndie katibu mwenezi na Dr John Nchimbi ambae ni katibu mkuu bado hawajaweza kutumia uzuri mitandao ya kijamii kukabaliana na hoja zinopelekwa kwenye mitandao ya kijamii hususan hoja kwamba Maridhiano yamenunuliwa na pesa imetumika kunyamazisha hoja hiyo.
3. Athari ya Chadema kupata msaada zaidi kutoka ndani na nje (external risk)
Hii imejibiwa na mzee Wassira kwa kuanisha jukumu la pili ambalo CCM inalo baad aya jukumu la kushika dola kwamba kukamilisha zile R nne za raisi Samia na hususan suala la maridhiano. Kwa wachambuzi twalichukulia hilo kuwa ni onyo kwa asasi za kijamii, wadau mbalimbali hususan jamii za kigeni waishio nchini kwamba kuna mtu kaingia mjini (New Man in Town) kwamba Amani ndo silaha pekee ya kuwezesha Maridhiano. Kwamba ni CCM pekee ambayo itaweza kumaliza suala la maridhiano na ni pale itaposhinda uchaguzi wa 2025.
4. Athari za migongano ndani ya chama (Internal Risk).
Hii imedhibitiwa kwa kumtumia Adam Kimbisa kutangaza mapema hoja ya kutaka Samia Suluhu Hassan kwa mgombea wa uchaguzi Bara na Dr Mwinyi kwa upande wa Zanzibar bila kufuata taratibu za kawaida za chama. Hilo la migongano ndani ya chama limezimwa mapema na kuondoa tatizo la vijana kuonyesha nia ya kutaka kugombea nafasi hiyo ilhali wagombea wanohitajika kwa sasa Samia Hassan na Dr Mwinyi ni tayari wagombea. Sababu kuwa ambayo yatumika kuwapitisha wagombea hao bila kupingwa ni kwamba wametekeleza kwa ufanisi ilani ya CCM ya 2020/2025. Hivyo kwa Kimbisa kutumwa na wazee akiwemo Jakaya Kikwete atangaze majina hayo ni ishara kuwa wazee wa CC wameamua hivyo na ndo kauli yao ya mwisho.
5. Kuua na kuzika rasmi mitandao ndani ya CCM (Internal risk)
Uteuzi wa Samia Suluhu Hassan na Dr Mwinyi kuwa wagombea pekee wa CCM ni ishara kubwa kwamba ndani ya CCM hakutakuwa na mitandao tena hadi baada uchaguzi wa 2025. Hatua hii imechukuliwa mapema ili kuweza kujijenga vilivyo kwa ajili ya kushinda uchaguzi wa mwaka huu na hivyo kuondoa uwezekano wa kuwepo mitandao au wana mitandao kama ilivyotokea katika mkutano mkuu wa 2015. Hivyo mgobea yoyote alie na tashwishi ya kuusaka uraisi kwa mwaka huu 2025 ndoto zake hizo zimezimwa rasmi tarahe 18 Januari 2025.
Kitu gani cha kuelewa?
CCM ni zao la TANU na ASP na mwaka 1977 ndo ikazaliwa CCM kikiwa sasa na matawi nchi nzima hku ikiweka kibindoni dola la bunge, mahakama na vyombo vya ulinzi na usalama. CCM yasemekan kuwa ndo chama pekee na kikongwe barani Afrika baada ya vyama vya CCP cha China chenye wanachama milioni 99 na chama cha Baratiya Janata cha India ambacho ndicho kiloshika dola kwa sasa chini ya raisi Modi.
Ni kwa msingi huo CCM imedhamiria kutoachia madaraka kwa gharama yoyote ile na juzi imedhirisha hilo kwa kuonyesha jinsi chama hicho kinavyotumia rasilimali za nchi kukodi mabasi mengi kwenda Dodoma badala ya kuamua kila mjumbe, mpambe na machawa wao watumie SGR kwenda Dodoma na hivyo kusaidia kukua kwa uchumi (growth), kuongeza uwezo wa SGR kukamilika kwa wakati na pia fedha zmbazo zingelipwa nauli zingeiwezesha SGR.
Ni athari zipi za nje ambazo bado CCM yaweza kukumbana nazo?(External risks)
1. Kasi ndogo ya kukua kwa uchumi baina ya mtu na mtu kwamba kuna watu wengi hawana fedha mfukoni kutokana na kukosa ajira. Hili ni bomu kubwa kwani vijana wengi imewabidi kuingia kazi ya uchawa kwa CCM na kupata ujira wa mpito.
2. Kiwango kikubwa cha watu walokosa ajira. Vijana wengi wahitimu wa vyuo vikuu wazurura mitaani kwa kukosa ajira za kueleweka. Vijana hao khasa wa Generation Z wamekuwa wazururaji na kuingia katika shughuli nyingi zisizo rasmi hususan mitandaoni kupoteza muda.
3. Kuongezeka kwa vitendo vya uhalifu, uporaji, utekaji hadi watoto wadogo kwa ajili ya shughuli za kishirikina ni miongoni mwa matatizo ambayo CCM imeyafumbia macho bila kujitokeza hadharani kuyakemea. Hii ni hatari kwa jamii kwani kunapokosekana Law and Order kunachochea matukio mengi kma hayo.
Akizungumza jana makamu mwenyekiti mpya mzee Wassira alisema bila amani hakutakuwepo na maridhiano au hakuwezi kufanywa vikao vya maridhiano lakini asahau pia kwamba kukosekana kwa ajira, uchumi kuwanufaisha wachache pia kwachangia kuondoa amani inosemwa ipo.
Ningependa kuhitimisha kwamba kwa uteuzi huu wa Steven Wassira kuwa makamu mwenyekiti wa CCM kwa upande wa Bara, na kuwateua rasmi raisi Samia Suluhu Hassan na Dr Hussein Mwinyi kuwa wagombea pekee wa chama hicho kwenye uchaguzi mkuu wa raisi baadae mwaka huu, hiyo ni ishara kubwa kwamba CCM imejipanga kushinda uchaguzi huo kwa gharama yoyote ile.
Hivyo basi uwezekano wa Chadema na vyama vingine vya upinzani kuweza kutoa changamoto kali kwa CCM katika uchaguzi huo ni mdogo mno na ushauri pekee wa kitaalam kwa Chadema ni kujipanga kwa uchaguzi wa mwaka 2030.
Chadema ina nafasi kubwa na rahisi zaidi ya kupata wabunge wengi na hata kushinda uraisi kwa wakati ule kuliko wakati huu.