Petro E. Mselewa
JF-Expert Member
- Dec 27, 2012
- 10,307
- 25,932
Utangulizi
Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania linaendeshwa kwa Kanuni zikisomwa pamoja na Ibara mbalimbali za Katiba ya JMT,1977 (kama inavyofanyiwa marekebisho mara kwa mara). Kanuni za Kudumu za Bunge,Toleo la 2007 (ambazo humu nitaziita 'Kanuni') ndizo zinazotumika sasa.
Kanuni hizi 154 zilizosheheni Fasili (Kanuni ndogo) mbalimbali zina Nyongeza Nane-Nyongeza ya Kwanza hadi Nyongeza ya Nane. Hata vifungu vya kwenye Nyongeza navyo huitwa Kanuni/Fasili.
Kamati za Kudumu za Bunge huteuliwa na Spika kwa mujibu wa Kanuni ya 113, Fasili ya 3. Kanuni ya 115,Fasili ya 1 inatamka wazi kuwa kutakuwa na Kamati za Kudumu za Bunge kama zilivyoainishwa kwenye Nyongeza ya Nane ya Kanuni. Kamati hizi hazifutiki hadi kufanywe mabadiliko ya Kanuni hizi.
Kwa mujibu wa Kanuni ya 152,Fasili ya 1,mamlaka ya kubadili Kanuni yamewekwa mikononi mwa Bunge zima ambalo litafanya hivyo kwa Azimio. Lakini Spika, kwa kushauriana na Kamati ya Kanuni za Bunge, atakuwa na madaraka ya kuzifanyia marekebisho au mabadiliko Nyongeza za Kanuni, kulingana na mahitaji ya wakati, kadiri atakavyoona inafaa. Hii ni Kanuni ya 152, Fasili ya 3. Swali ni je, Kanuni hii ilifuatwa katika 'kuifuta' POAC ambayo kimsingi imo kwenye Nyongeza ya Nane ya Kanuni? Fahamuni ya kwamba Kiongozi wa Upinzani au Mwakilishi wake ni Mjumbe wa Kamati ya Kanuni za Bunge. Mh. Mbowe au Mwakilishi wake alibariki mabadiliko ya kufuta Kamati kwa mujibu wa Kanuni ya 152, Fasili ya 3?
Kwa mujibu wa Nyongeza ya Nane ya Kanuni, kuna Kamati za Kudumu za Bunge za aina tatu:
Kamati za Kudumu zisizo za Sekta ambazo ni Kamati ya Uongozi,
Kamati ya Kanuni za Bunge, Kamati ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge,
Kamati ya Sheria Ndogo na Kamati ya Masuala ya Ukimwi.
Pia zipo Kamati za Kudumu za Bunge za Sekta ambazo kimsingi hazitofautiani sana kimajina na Wizara zilizopo.Mfano,Kamati ya Fedha na Uchumi pamoja na Kamati ya Nishati na Madini.
Halafu, kuna Kamati za Kudumu za Bunge zinazosimamia Fedha za Umma. Hapa kuna Kamati ya Hesabu za Serikali,Kamati ya Serikali za Mitaa na Kamati ya Hesabu ya Mashirika ya Umma(POAC) iliyosemekana 'kufutwa'.
Zitto kafanya nini hasa?
Yawezekana Zitto amekosea katika kutekeleza majukumu ya Kamati yake. Ka mujibu wa Kanuni ya 13 ya Sehemu ya Tatu ya Nyongeza ya Nane ya Kanuni, majukumu ya POAC ni yafuatayo:
(a) kushughulikia taarifa za kila mwaka za hesabu zilizokaguliwa za Mashirika ya Umma.
(b) kushughulikia maeneo yenye matatizo sugu ya matumizi mabaya ya fedha za Mashirika ya Umma yaliyoidhinishwa katika taarifa za kila mwaka za hesabu zilizokaguliwa za Mashirika hayo na kutoa mapendekezo na ushauri wa namna ya kuyaondoa matatizo hayo.
(c) kufutalia utekelezaji wa mapaendekezo yaliyokwishatolewa na Kamati hiyo ili kuondoa matatizo hayo.
(d) kutathmini ufanisi wa Mashirika ya Umma
(e) kufuatilia utekelezaji wa Sera ya Ubinafsishaji wa Mashirika ya Umma
Jukumu gani akina-Zitto hawakulitekeleza? Je,majukumu haya hayatakiwi tena nchini mwetu? Jadilini mkijua na haya
cc Zitto