Uchambuzi Ngao Ya Hisani: FT Simba SC 0 Vs 1 Yanga SC

demigod

JF-Expert Member
Joined
Jan 2, 2015
Posts
8,292
Reaction score
15,250
Huu ni mtazamo wangu binafsi wa kiufundi kwenye mechi ya leo ambayo Mabingwa Wa Kihistoria wamerudi kwa staili mpya.

Mabeki wa Kushoto/Kulia wa Simba SC walikuwa wakishinda nyuma wakati wote wakihofia Mashambulizi ya winga machachari za Yanga. Kitu ambacho kilitengeneza ombwe la nafasi kwenye flanks za Simba. (Hilo lilisababisha beki za yanga kuwa free kupanda juu kuwafuata).

Washambuliaji wa Kushoto/Kulia wa Simba SC hawakuwa na ufanisi katika kurudi nyuma kuwasaidia walinzi kufanya marking kipindi Yanga wanashambulia. Hilo lilipelekea Yanga kumiliki mpira sana katika eneo la katikati na hata simba wakaamua kutumia nguvu zaidi kutafuta mipira na kuzalisha faulo nyingi zaidi katika historia ya fainali za Ngao Ya Hisani.

Changamoto za Yanga SC bado ziko kwenye mipira ya cross inayokuja kwenye box la Diarra. Simba walishindwa kutumia madhaifu hayo kwa kuwa washambuliaji wao wengi wa mbele ni wazembe na wavivu.

Mikimbia ya Mayele ilikuwa hatari kwa beki za Simba (Huenda ilikuwa sababu ya Prof NABI kumuanzisha yeye badala ya Makambo).

Yanga SC ime improve kwenye uwezo wa kugombania mipira iliyokufa, hii inatokana na kuwa na wachezaji wengi wenge nguvu zaidi kuliko wachezaji wa sSimba ambao wengi ni soft players (Bwalya, Banda, Pape Ousmane nk co.)

Kanoute alikuwa poa katika wakati wote uwanjani, alikosa wachezaji wenye uwezo wa kutafuta nafasi za mbele ili jitihada zake zizae matunda. Hii inatokana na mpangilio wa safu ya ulinzi wa Yanga ambayo aikuwaruhusu wachezaji wa simba kufanya forward-runs. Nabi aliweza kufahamu strength hii ya simba mapema zaidi na kuifanyia kazi isiweze kumfukuzisha kibarua.

Yanga SC walitumia mfumo wa 4-5-1 kukabia juu mara pale Simba wanapochukua umiliki wa mpira. Mara simba walipokuwa wakifanikiwa kuuvunja mfumo wa Yanga wa ukabiaji juu (yaani 4-5-1), Yanga SC walikuwa wakibadili mfumo ghafla na kutumia 4-4-2 ili kujiandaa na hatua ya kutengeneza mashambulizi ya ghafla pale wapatapo mpira.

Coach Gomes ana homework kubwa sana ya kufanya kwa kuwa imeonekana hana plan B pale plan A yake inaposhindwa kufanya kazi. Na plan B yake iko bayana - ambayo anapenda kutumia mipira mirefu na kuongeza washambuliaji. (kumbuka leo dakika za 68 & dakika za mwisho za mechi ya Kaizer Chiefs).

Simba SC imeporomoka ki-ubora ukilinganisha na Yanga SC ambayo ki-ubora imeimarika zaidi ukilinganisha na wakati ulio pita.

Yanga SC watafanikiwa kuchukua Ubingwa wa msimu huu 2021/22
Simba SC watafanya vibaya sana kwenye michuano ya CAFCL
Okwi atasajiliwa SImba SC katika dirisha dogo la usajili ili kuwasaidia wakina Morison & Banda.
 
Pia yanga kwenye suala la Aerial balls tunatakiwa kulifanyia kazi.

Pia chance nyingi tunashindwa ku covert kua magoli.

Yannick bangala what a man!![emoji119].

Khalid Aucho jamaa anapiga forward pasi balaa..
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…