Kamati kuu ndio kikao cha juu zaidi cha chama. Kwa case ya CCM na Chadema kunakuwa na viongozi waandamizi wa serikali wanaotokana na chama mfano Rais, Makamu wake, Waziri mkuu, spika wa bunge n.k pia wanakuwepo wenyeviti wa jumuiya zote za chama mfano UWT, UVCCM, Wazazi n.k
Mkutano mkuu unafanyika at least mara moja kwa miaka 5 unapitisha wagombea urais pamoja na uchaguzi wa uongozi wa juu wa chama.
Ila baraza kuu kwa case ya chadema ni kika cha kiutendaji cha mkutano mkuu. Hiki kinafanyika kila mwaka na wajumbe wake ni kamati kuu, viongozi wa kanda, mkoa na wilaya
Ili kutofautisha mkutano mkuu na baraza kuu, wajumbe wanaongezeka kwenye mkutano mkuu ni wenyeviti na makatibu wa jimbo pamoja na wajumbe wanaochaguliwa na mabaraza eg BAVICHA, BAWACHA etc, pamoja na wajumbe wawakilishi wa kila wilaya.
Secretariat ya kamati ni watendaji wa shughuli za kila siku za chama. Mwenyekiti wa secretariat ni katibu mkuu wa chama na anasimamia watendaji wengine kama wakurugenzi wa idara za chama, manaibu katibu bara na zanzibar, makatibu wa BAWACHA, BAVICHA, BAZECHA na wataalam 5 wanaoteuliwa na katibu mkuu.