Uchambuzi: Shirika la ujasusi la Uisraeli Mossad

Uchambuzi: Shirika la ujasusi la Uisraeli Mossad

Nanyaro Ephata

JF-Expert Member
Joined
Jan 22, 2011
Posts
1,234
Reaction score
1,815
Kitabu.Mossad
Mwandishi.Michael Bar Zohar & Nissim Mishal
Mchambuzi.Nanyaro EJ


Dibaji.
mwandishi anasema kuwa hiki kitabu ni mchanganyiko wa kazi za kutukuka zilizofanywa na Mossad,nafanikio na changamoto moto,mkusanyiko wa operesheni mbalimbali ambazo zimefanywa maeneo mbalimbali Duniani.
Mossad ni shirika la ujasusi la Uisraeli,ambalo ni miongoni mwa mashirika bora kabisa na ya kisasa katika mambo ya ujasusi.Shirila hili limefanya kazi kubwa ya kuifanya Israeli iwe ilivo leo,na limekuwa likilinda maslahi ya Uisraeli na mataifa ya magharibi hasa USA.


Novemba 12 mwaka 2011 ilitokea mlipuko mkubwa kwenye moja ya vinu vya kutengeneza silaha za maangamizi na masafa marefu Jijini Tehran nchini Iran.Mlipuko ule uliua baadhi ya wanajeshi wa Revolutionary Guards wa Iran,ingawa lengo la mlipuko halikulenga kuua binadamu tu bali kuharibu mfumo mzima wa mradi huo.Mradi huu ulilenga kuendeleza silaha za masafa marefu ambazo zingeweza kuipiga Marekani kutokea hapo jijini Tehran.Kwa muda mrefu sana Iran imekuwa na mradi mkubwa wa kuwa Taifa la kwanza la Mashariki ya Kati kuwa na silaha za kivita za masafa marefu(long-range misiles).Hivo Mossad walilipua hivo kuchelewesha kwa zaidi ya mwaka mpango huo
Wakati wa arab spring Misaada walionya nchi za Magharibi kuwa wasishangilie na kufikiri kuwa ni neema imewaangukia,Mossad walionya kuwa huo utakuwa mwanzo wa makundi yenye misimamo mikali,na mwanzo wa USA kukataliwa na wananchi kwenye eneo la mashariki ya kati,USA ulifurahi anguko la Mubarak huko Misri,lakini wale waandamanaji waliokusanyika Taharir square walikuwa wa kwanza kuchoma bendera ya Marekani,na uchaguzi uliofuatia ulishuhudia kundi la hasimu la USA kuingia madarakani yaani Muslimu brotherhood.Hata Libya baada ya kuangushwa kwa Gharadi makundi hasimu wa USA amezaliwa mengi,ndio kusema bora shetani unayemjua kuliko malaika usiyemjua


Chapter 1


King of shadows


Hili ni jina alipewa ofisa mmoja wa Mossad aliyekuwa anaitwa Meir Dagan.Huyu ofisa alikuwa na akili ya ziada katika kupambana na adui wa Israeli,alizaliwa mwaka 1945 ndugu zake wengi waliuwawa kwenye kambi za mateso na mauaji zama za chama cha Nazi huko Ujerumani.Wakati akikuwa alijiapiza kulinda Taifa la Israeli kwa gharama yoyote ile.
(kwa miaka mingi Waisrael wametumia mauaji hayo kupata public sympath) kama huku Afrika tunavyotumia Ukoloni kama sababu kuu ya kutokuendelea)
Huyu Bwana Degan alikuwa na kipaji cha kipekee sana katika uwanja wa vita.Miaka ya 1971 ni miaka ambayo Wapalestina walikuwa wanafanya mashambulizi ya kushtukiza kuwaua Waisraeli,walitumia mabomu ya kurusha kwa mikono,kujitoa muhanga,milipuko na njia yoyote ambayo waliona ni sawa,hii hali iliwalazimu Mossad kuanzisha kitengo kisicho rasmi kilichoitwa Rimon,hiki kitengo cha vijana werevu kiliundwa na Ariel Sharon alikuwa mkuu wa Mossad wakati huo,na Dagan akawa mmoja wa vijana wake. (Ariel Sharon alikuja kuwa waziri mkuu wa Israel,alieshinda iwa kura nyingi sana lakini akaharibu kwa kuwaondoa Waisraeli Gaza,baada ya hapo alikaa ICU akiwa mgonjwa sana kwa miaka nane,ndio binadamu mwenye rekodi ya kukaa ICU kwa muda mrefu zaidi tangu zamani za Pontio Pilato hata sasa)


Sasa huyu jamaa Dagan alifanya operesheni mbalimbali kwa mafanikio makubwa.Alikuwa na uwezo wa kujibadili kutokana na mazingira kama kinyonga.Mwaka 1971 Januari 2 aliongoza operesheni kinyonga.Operesheni hii ililenga kuwaua jamaa fulani hatari wa kundi la PLO,sasa hawa Mosad wakiongozwa na Mosad walikuwa na boat mbili moja ikiwa kama inakimbiza ingine kuelekea kwenye kambi ya wakimbizi wa Kipalestina,hii kambi ilikuwa jirani na fukwe yenye kijiji cha wavuvi..kwenye boat ya mbele alikuwa Degan aliyejifananisha na wapiganaji wa Wapelestina alipofika ufukweni alikimbia kuingia kambini kuomba msaada wa maficho,ile boat ya pili ilisimama majini.Sasa huyu bwana Degan alipata hifadhi huku alijitambulisha kwa majina ya Kipalestina na kuwa ametoka Lebanon kwenye kambi ya mafunzo(hawa wapalestina hawakutambuana kwa sura bali kwa ishara fula ni na majina ya viongozi wao)Degan alitumia udhaifu huo kujifannanisha na kupata fursa ya kujichanganya akiwa huko na bastola ambazo hazitoi sauti aliuwa yule aliyemkusudia kisha kutoroka kurudi kwenye eneo lake la kazi


Mwandishi anasema bwana Degani alipanda vyeo hadi kuja kuwa ndio kiongozi wa Rimon,alifanya Rimon kuwa tishio sana kwenye eneo la mashariki ya kati,wakuweza kupenya kwenye ngome ya adui kwa mtindo wao huo huo wa kinyonga.Wakati mwingine wakivaa kama adui na kuishi na adui.Hii iifanya wafanikiwe sana katika kuzuia mashambulizi yaliyokuwa yanafanywa kila siku na makundi mbalimbali ya wapelestina




Chapter 2


FUNERALS IN TEHRAN




Mwandishi anasema kuwa siku ya July 23, 2011, 1630 P.M.zilitokea pikipiki mbili katika viunga vya Jiji la Tehran wakampiga risasi mwanamume aliyekuwa herini kwake,akisubiri geti ufunguliwe aingie,kisha zile pikipiki zikatokomea kusikojulikana.Aliyeuwawa alikuwa niv Darioush Rezaei Najad, aliekuwa na miaka 45 profesa wa chuo kikuu.Huyu jamaa alikuwa mmoja wa wataalamu wa mpango wa Siri wa utengenezaji wa silaha za nyuklia nchini Iran.Kuuwawa kwa huyu mtaalam ulikuwa mwendelezo wa mauaji kadhaa ya watalaam wa mpango huu wa Iran,mauaji haya yalifanywa na Magharibi pamoja na washirika wake.


November 29, 2010, Mwanasayansi mwingine aliuwawa kifo cha ajabu tena,yeye akiwa barabarani na gari ikiwa inatembea ilitokea pikipiki ikapachika kifaa fulani kwenye kioo cha nyuma ya gari ya huyu mtaalamu,baada ya dakika chache ile gari ikalipuka ikiwa inatembea.Huyu profesa nae akasambaratika kabisa,kumbe ile pikipiki iliweka kifaa kilichosababisha huo mlipuko,Serikali ya Iran iliwanyooeshea mkono Mossad.Idadi ya waandamanaji waliouawa ilizidi kuongezeka na ilizidi kuwachanganya Iran maana baadhi ya waliouwawa walikuwa wanasayansi ambao Serikali iliwapa kazi nyingine hasa Uhadhiri wa vyuo vikuu,na huko walitakiwa kuwa wakosoaji wakubwa wa Serikali ili waonekane wapinzani wa utawala wa Irani.Mfano kuna jamaa aliitwa Mahmud Mohamed ambaye aliuwawa kwa mlipuko uliotegwa kwenye gari yake,baada ya kuuawa wengi wa rafiki zake walishindwa kuelewa lakini baadae kwenye mazishi nusu ya waombolezaji walikuwa maofisa wa Revolution Guard!


Kwa mujibu wa gazeti la London Telegraph mwaka 2007 liliripoti kuwa mauaji ya hawa wanasayansi wa Iran yalifanywa na Mossad ambayo kwa kipindi hicho Mkurugenzi wake alikuwa yule kijana matata Meir Dagan.Hii yote ikifanyika na vijana wa Dagaa kwa kutumia kitu walichoita Double Agent na Sleeping Agents.Mosad walifanikiwa kuweka mawakala wa Siri sana ambao walikuwa raia wa Iran na wengine walikuwa hao hao wanasayansi ambao walilipwa pesa nyingi ili kutoa taarifa
Hatua ya kwanza Mosad waliamua kuwaua kabisa wanasayansi wa Iran kama njia ya kuhujumu mpango wa Nyuklia wa Iran.Mosad walitumia njia kadhaa ikiwepo hujuma,operesheni za siri,mauaji,hadi ile maarufu ya kutengeneza virusi


Ni muhimu kukumbuka kuwa miaka ya 70 Iran ikiwa chini ya utawala wa Shah ilikuwa mshirika muhimu wa Ustawi,wakati wa vita ya Iran na Iraq Israel ilisaidia Iran sana hasa kijeshi,bahati mbaya utawala wa. Shah uliangushwa na Ayatollaa Khomein ambao hawakutaka ushirika na Israel hadi leo.Kufuatia kuuwawa kwa Wanasayansi wake wengi Iran ilibadilika mbinu ya urutubishaji wa Vinu hivi vya Nyukilia kwa kutengeneza vinu bandia ili kumchanganya adui,mbinu hii ilifanikiwa kwa kiasi fulani,mashirika ya Magharibi na Mosad hawakuweza kung'amua mara moja nini hasa kiliendelea Tehran
Wakati wa anguko la Soviet Irani ililitumia kama fursa kwa kuwanunua wanasayansi wa Soviet,kipindi hicho ilitokea wanasayansi wengi kutoweka nyumbani kwao hasa wanasyansi wa silaha za kibaolojia na silaha nyingine.Iran ilitumia fursa hii ya anguko la Soviet kimkakati sana



Mashirika mengi ya kijasusi yana mbinu ya kisasa sana ambayo huanzisha makampuni ya kutoa huduma mbalimbali haya makampuni yanaitwa Front companies sasa kazi ya haya makampuni ni kutafuta kazi mahususi kabisa kisha kutumia kazi hiyo kufanya upelelezi,kukusanya taarifa au kutengeneza vifaa hafifu kumshughulikia adui.Sasa basi Mosad walitengeneza kampuni ambayo ilikuwa iko Urusi ikimilikiwa na jamaa mmoja Mrusi na Mu Iran hii kampuni iliitwa Eastern European hii kampuni ilikubali kutengeneza vifaa kwa ajili ya Kinu cha Nantaz hiki kilikuwa Kinu kikubwa kuliko vyote,Iran ililazimika kutumia kampuni za Siri kwa kuwa walikuwa wamewekewa vikwazo.kumbe hii walikuwa wanajiweka mdomoni mwa adui,hii kampuni wamiliki wake walikuwa mawakala wa siri wa Mossad waliosambazwa Ulaya yote,hii Eastern European ilitengeneza vifaa vya maabara ya siri kisha kwenye hizi vifaa wakaweka shoti ya umeme,wanasayansi wa Iran hawakugundua hilo,hivi siku waliyopanga kuzindua rasmi,wakawasha ghafla kompyuta zote zenye taarifa maalum zikapigwa shoti na kulipuka,safari hii hakuna kifo ila mifumo yote iliharibika vibaya


Kwa miaka saba mfululizo Mossad waliendelea kufanya hujuma kwenye vinu na maabara za siri za Urai,pamoja na kuua watalaam,katika kipindi hiki zaidi ya wataalam wa hali ya juu wa Iran 240 waliuwawa kwa milipuko na njia mbalimbali ambazo hazikuacha alama.Mwaka 2007 Rais Bush wa USA alisaini mpango wa siri wa Rais wa kuruhusu CIA ianze operesheni mahususi kuzuia Iran isiendelee na mpango wake wa Nyukilia


Mwandishi anasema kuwa mwaka 2010 ulikuwa mgumu zaidi kwa Iran,uliosababishwa na vikwazo vilivyowekwa na UN hivo kusababisha Iran kushindwa kupata spea kwa ajili ya vifaa mbalimbali kwenye mpango wao wa Nyukilia. Mwaka huu 2010 Kirusi *Stuxnet virus* kilishambulia maelfu ya Komputa kwenye vinu vya Iran na kusababisha madhara na uharibifu mkubwa sana,kirusi hiki ni matokeo ya hujuma za Mossad na kilikuwa kirudi hatari zaidi kwenye mifumo ya Komputa Duniani,kwa kuwa kulikuwa hamuwezi wa kushambulia Komputa fulani..yani kilitumwa kwa komputa fulani,na kwenye hiyo Komputa kilielekezwa kuharibu nini,so kiliweza kuharibu mafaili fulani na kuacha faili fulani hata kwenye komputa moja.Ilikuwa pia vigumu kujulikana kikishaingia kwenye komputa
Mwandishi angurumisha chapter hii iwa kusema kuwa Magharibi na Mossad walifanikiwa tu kuchelewesha mipango ya Iran lakini sio kuiharibu kabisa,kwani walikuja kuendelea na mipango yao hasa baada ya shirika la UN la Nguvu za Atomic kuwachunguza na kusema kuwa hawakukuta kinu kwa matumizi ya kijeshi bali kiraia ambayo yanakubalika kisheria


Kitabu.Mosad
Mwandishi
Mchambuzi.Nanyaro EJ


Chapter 3


A HANGING IN BAGHDAD


Mwandishi anasema kuwa kabla ya uhuru wa Taifa la Israel mwaka 1948,waisrael wengi walikuwa wanaishi kwenye jumuiya ndogo ndogo kwenye miji mingi Duniani.Ujerumani ilikuwa na Waisraeli wengi kuliko nchi nyingine yoyote ile.Katika hizi jumuiya walifundishana mambo mengi hasa ya ujasusi huku wakiwa na matumaini makubwa ya kurejea nchini kwao siku moja.Nchini Iraq kilikuwa kituo kikubwa baada ya Ujerumani ambako mto wa Bagdad ulijaa Waisrael wengi wakiwa katika idara nyeti za serikali na binafsi,kutokea Baghdad ambako waliishi kwa majina bandia ili wasijulikane walisambaa kwenye miji mbalimbali ya Mashariki ya Kati kwa lengo la kufunza kuhusu eneo hilo,ndio maana baada ya uhuru wameendelea kushinda vita kadhaa kutokana na kuwa na intelijensia ya kutosha kuhusu eneo hilo


Baada ya uhuru ilitokea vita kati yao na mataifa ya Kiarabu iliyodumu kwa mwaka mmoja,na Israel kupata waziri mkuu wa kwanza aliyeitwa Ben Gurion.Kipindi hiki walianzisha idara ya siri ya ujasusi,iliyoongozwa na Isser Beer huyu jamaa aliongoza Idara hii kwa mfano wa KGB ya Urusi.Kipindi hicho idara hii ilikuwa ikihisi kuna msaliti basi alikamatwa na kuhukumiwa kifo au kifungo cha maisha au kuuawa.Jamno hili lilikiuka msingi wa kuanzishwa kwa kwa Taifa changa la Israel.Hii iliwafanya watafakari njia mbadala ambayo itaheshimu utu wa watu wao hata pale wanapokea Taifa lao,ikaonekana kujenga mapenzi ya kweli kwa Taifa pamoja na uwajibikaji wa hali ya juu ndio vitakuza mapenzi na hivi kuondoa uwezekano wowote wa kununuliwa na nchi nyingine.


Baadaye sana iliundwa chombo kilichoitwa political research ambacho kilikuwa idara ya ujasusi,na baada ya ufanisi wakaja kuunda Mossad ambayo iliundwa kwa mujibu wa kitabu cha Bibilia takatifu
*Mithali:11.14
Pasipo mashauri taifa huanguka; Bali kwa wingi wa washauri huja wokovu.*
ingawa mwandishi anasema hawafuati misingi tajwa


Chapter 4


A SOVIET MOLE AND A BODY AT SEA


Mwandishi anasema kuwa uanzishwajinwa Mossad haukuwa mrahisi hata kidogo,kulikuwa na watu wa ile idara ya siasa ambao hawakuafiki wazo la kuwa idara moja,maana walizoea kula.Pia kulikuwa na kusalitiana kwingi mno,ambako idara kama M16 ilikuwa inapambana kuweka watu wake ndani ya Mossad.Sovieti hawakuwa mbali pia!anatoa mfano wa jamaa mmoja Mwisarael aliyeitwa,Avin ambaye alikuwa na moyo wa kujitolea sana,kwenye Mossad na baadae akawa mwajiriwa wa sasa huyu bwana aliwekwa kituo cha kazi Yugoslavia ya zamani,kwa miaka mingi alikuwa anashawishi wakubwa zake wafungue kituo kikubwa hapo Yugoslavia bila mafanikio,aliporejea kwao ghafla alienda makao makuu ya Mossad ili aonane na Mkurugenzi kwa wakati huo alikuwa Bwana Harel ili kumshawishi kuwa wafungue kituo,alipofika ofisini alikutana nae sasa huyu Mkurugenzi hisia zake zikamwambia huyu ni msaliti,hapo hapo akamweka chimbua ulinzi na kumhoji baada ya kubanwa sana alikiri kuwa wakala wa Soviet,alifungwa miaka 14 hii ilikuwa miaka ya 1956


Mwandishi anasema kisa kingine ni cha kijana Israel huyu alikulia Sofia na baadaye akarejea Israel ambako alijiunga na jeshi la majini.Huyu kijana alikuwa na tabia za wakora,muhuni na mtu wa wanawake,alipokuwa Sofia alikutana na mchumba wa kikiristo aliyemtaja abadili dini ndio atamkubali bwana Israel hakusita mara moja akabadili dini kuwa Mkiristo kutoka dini yao ya Uyuda.Sasa aliporeja akamtelekeza huyu mchumba wake huko Sofia akiwa mjamzito,alifanya kazi jeshini lakini alikuwa mkora pia,akiwa Jerusalem alipata mchumba wa Kiisrael ambaye waliooana lakini baadaye miezi mitatu akampata mfanyakazi wa ubalozi wa Italy akamtaka tena huyu mtaliano akamtaka abadili dini jamaa akaenda kufoji jina akapewa jina la ambalo alikuwa mkiristo sasa akiwa nyumbani kwake ana jina la Kiisrael akiwa mtaani kwa mchumba ni Alexender Ivor mkiristo.Alipewa na pasipoti kupitia kina la pili ambalo halikufahamika kwa wengi.
Bwana alitoroka kwenda Roma bila kumwaga yeyote sio nyumbani wala kwa Bi wa Kiitaliano.Akiwa Roma alikutana na maofisa wa Ubalozi wa Misri wanaoshughulika na mambo ya kijeshi ambako walimpa dola elfu moja na mia tano(1500)akawapa taarifa muhimu za jeshi la Israel,hapo Roma wakala wa Mossad alikuwa na *connection* kubwa hivo haikupita muda akajulishwa kuwa kuna mtu anauza ramani ya jeshi,bila kupoteza kuda akatuma cable kwa wakubwa zake,ambao nao mara moja waliagiza afuatiliwe mara moja na kurudishwa Tel aviv.Hii ni moja ya operesheni yenye mafanikio makubwa na ambayo kwa mara ya kwanza Mossad walitoa kibali cha kukamata au kuua ikibidi!
Bwana Isirael alikuja kukamatwa jijini Paris baada ya kukubali lift tax aliposhuka uwanjani akitokea Austria.Alipelekwa kwenye moja ya nyumba hapo Paris na baada ya mahojiano alikiri kuuza taarifa kwa Misri na alikuwa aende Misri kukutana na wakuu wa serikali huko ili apate hela zaidi.Ikaamuliwa asafirishwe hadi Tel Aviv akashtakiwe.Alipandishwa kwenye ndege ya shirika la ndege la Israel ambayo ingesimama kujaza mafuta Roma,kisha Athens ndio itue Tel Aviv,ili kupandisha ndege ilibidi afungwe kwenye box kama kifurushi.Akiwa angani Mossad walikuwa na daktari ambaye alikuwa akimchoma sindano za usingizi!bahati mbaya zile sindano na hali ya hewa vilimzidia hivo akafa,licha ya jitihada za kuokoa maisha,ndege ilitua Tel aviv na baada ya kushusha mizigo na abiria wote,wakuu Wa Mossad walielekeza hiyo ndege ipae na hiyo mauti hadi baharini kwenye kina kirefu kisha waitupe huko baharini! Ndio ilifanyika hivo
 
Kitabu.Mossad
Mwandishi. Michael Bar-Zohar na Nissim Mishal
Mchambuzi.Nanyaro EJ

Chapter 5
“OH, THAT? IT’S KHRUSHCHEV’S SPEECH …”

Mwaka 1956 mwandishi Victor Grayevski aliingia kwenye mahusiano ya kimapenzi na naibu waziri mkuu kutoka chama cha kikomunisti cha Poland.Victor alikuwa mlowezi wa Kiyahudi ambaye aliingia Poland akitokea Ujerumani,na alipofika alishauriwa abadili Ubini wake ili usiwe na mfanano wa Kiisrael hivo akajiita Grayevski kutoka Shiplman.Baada ya muda alipata kazi ya kuwa mhariri mkuu wa shirika la utangazaji la Poland(PAP)
Mwandishi anasema kuwa Victor alikuwa mdogo wakati wa vita kuu ya pili ya Dunia,wazazi wake walitorekea Poland,ila baadae sana walikuja kurudi nyumbani kwao huko mashariki ya kati,Siku moja Victor alienda Jerusalem kuwasalimia wazazi wake,na kwa mara ya kwanza alikuta Dunia nyingine mpya kabisa yenye uhuru na sio ule mtindo wa propaganda za kijamaa alizozoea huko Poland na Soviet….hii ilimvutia na aliamua kuhamia nchini Israel moja kwa moja..
Mwandishi anasema siku moja Victor aliamua kwenda ofisini kwa mchumba wake ambaye ni naibu katibu mkuu na naibu waziri mkuu wa chama cha kijamaa cha Soviet ili amwage,akiwa pale ofisini aliona kabrasha kubwa limeandikwa TOP SECRET,alimwuliza huyu Naibu katibu mkuu ambaye alimjibu kuwa ni sehemu ya Hotuba ya Nikita Khrushchev ambaye alikuwa katibu mkuu wa chama cha ujamaa cha Soviet.Victor alivutiwa sana na kutamani kujua nini hasa kimeandikwa hadi kiitwe Top Secret.Huyu Nikita alikuwa katibu mkuu mwenye maguvu makubwa nay a kutisha.Sasa basi kwenye mkutano mkuu wa chama cha Soviet uliokuwa umefanyika katika ikulu ya Kremli,wageni waalikwa mabibi na mabwana walitolewa nje,na wakabaki wajumbe 1400 kutoka pande zote za Soviet,hapo ndio katibu mkuu Nikita alitoa hotuba kali ambayo ilimwacha kila mtu akiwa mdomo wazi kwa mshangao mkubwa.
Nikita alihutubia kwa masaa manne,ambayo alielezea kwa nukta na kwa ufasaha mkubwa madhambi na uhalifu wote ambao ulikuwa umefanywa na Rais wa Soviet bwana Stalin(Stalin alikuwa anaabudiwa na watu kutokana na ukatili wake,inaaminika aliuwa watu wengi Zaidi nyuma ya Mao wa China).Sasa Nikita alielezea jinsi utawala wa Stalin umeua mamilion ya raia wasio na hatia,inasemekana ukumbi mzima ulilia hadi ikafikia wanajingoa nywele kichwani kwa uchungu,wajumbe wengine walizimia,na wengine walipata mshutuko wa moyo,angalau wajumbe wawili walijiua usiku huo huo kwa uchungu(Yaani wanasikia uchungu hadi unajiua)…..lakini hakuna habari yoyote kuhusu hii hotuba ilichapishwa kwenye vyombo vya habari vya Kisoviet(wakati huo serikali na chama vilishika hatamu)
Mwandishi anasema kuwa Moscow walikuwa na nguvu sana hasa kwenye taarifa ambazo wanataka umma ulishwe,ilifikia hadi CIA wakaweka dau la USD 1mil kwa mwandishi atakayesaidia kupata hotuba hii yote,lakini jitihada hizo za CIA ziligonga mwamba.Sasa Kijana mdogo Victor akiwa ofisni kwa mchumba wake ndio anagundua kuwa hii taarifa ni dhahabu,ni lulu.Ilikuja kugundulika baadae kuwa Nikita alikuwa ametuma sehemu ya hotuba yake hii kwa vyama vya kijamaa huko Magharibi.Sasa Victor alimwomba huyu mchumba wake akasome hii hotuba,na akapewa kwa masharti kuirejesha kabla ya saa kumi jioni,alipoisoma akakuta jinsi Stalin alivokatili maisha ya Warusi wenzake na mataifa mengine,kiukweli Stalin alikuwa mhalifu dhidi ya ubinadamu,alikatili maisha ya watu wengi sana wengi wakiwa Wajamaa wenzake kutoka chama cha kijamaa.Victor akapeleka hotuba hii kwenye ubalozi wa Israel nchini Poland baada ya kuona kuna taarifa muhimu kwa Taifa lake,pale ubalozini wakatoa nakala kisha Victor akawahisha hotuba ofisini kwa mchumba wake kwa muda mwafaka
Pale ubalozini walikabidhi hotuba ile kwa mossad ambao nao baadae ya kuisoma walitoa nakala wakawapa CIA.Hili liliwashangaza sana USA kuwa hotuba ambayo wamewekea dau kubwa na bado hawakufanikiwa kuipata lakini shirika dogo kama Mosad walifanikiwa kuipata.Baada ya wataalam kuichunguza kwa kina walikubaliana kuwa ndio yenyewe hivo CIA wakai leak kwa gazeti maarufu la New York times kwenye Makala yake maarufu ya Juni 5 mwaka 1956.Taarifa hii iliishtua jumuia ya kijamaa Dunia na ilileta mpasuko mkubwa sana,nan chi kama Hungary na Poland zikaanza harakati za kujiondoa kwenye ujamaa
Serikali ya Israel iliamua kumpa Victor kazi nzuri Zaidi kama shukrani kwa kusaidia Taifa lake,ambako aliajiriwa kwenye wizara ya mambo ya nje.Akiwa jijini Tel aviv alikutana na agenti wa KGB ambaye alimshawishi Victor akubali kuwa wakala wao,yeye Victor alienda Mossad akawajulisha kuhusu offer aliyopewa na Mossad walimtaka Victor akubali offer hiyo.Mossad wakamfunndisha Victor na kumpa taarifa mabazo alipaswa kuwapa KGB,kwa miaka kumi nan ne KGB walimwamini Victor na wakala wao akawa anakutana na Victor maeneo mbalimbali ya siri bila KGB kugundua kuwa walikuwa wameuziwa mbuzi kwenye gunia…….KGB walichezewa cheupe cheusi.Moscow waliamini wana mtu wao mwaminifu ndani ya serikali ya Israel na kila taarifa waliyopewa na Victor waliamini ni sahihi kumbe ilikuwa ni taarifa za kupikwa na Mossad….kitaalamu Victor alikuwa anafanya kazi ya double agent
Mwaka 1967 Moscow walimpuuza na kwa bahati mbaya ilikuwa kipindi ambacho yeye Victor aliwapa taarifa za ukweli.Ilikuwa wakati wa vita ya siku sita…wakati huo Misri waliandaa jeshi kuikabili Israel,na Israel ilitaka kuitumia Soviet ambayo ilikuwa na ushawishi mkubwa kwa Misri,hivo Voctor alitumwa awajulishe Moscow kuwa kama Misri ikiondoa vikosi vyake na kuvirudisha nyuma Israel pia haitaingia vitani.Lakini Moscow walipuuza wito huo na wakaitaka Misri iendelee na wao Soviet watawaunga mkono na kuwapa kila aina aina ya msaada.Matokeo ya ile vita yalidhihirisha udhoofu wa silaha za Soviet,Israel ilishinda na kujipanua Zaidi.
Mwandishi anahitimisha kuwa Victor alikuja kupewa Nishani ya heshima na Soviet inayoitwa Lenin.Hii inamfanya kuwa wakala pekee ambaye alitumika nan chi mbili bila kustukiwa,nan chi yake ilimpa nishani ya utumishi uliotukuka…..na ni moja ya watu wanaoshemika zaidi
 
Bush Sr hata biography yake inaonyesha aliwahi kushika wadhifa huo. Lakini kwa Ariel Sharon, sidhan kabisa. Alitoka jeshini akaingia kwenye siasa.
Hahahaha huwezi kujua Mkuu

Ujue hata Bush snr ashawahi kuwa mkuu wa CIA ?
 
Hawa mawakala wa ujasusi kwenye mafunzo yao wabafundishwa na somo la kutongoza. Kumtongoza naibu waziri akukubali akupe siri na kitumbua chake, si mchezo.
Ahahahah hawa jamaa huwa wanakula Totoz high class!!
Sio Slay Queen's
 
Ha ha ha lakini mbabe wao alikuwa jiniasi mmoja hivi anaitwa qassimu suleiman tena huyo kashakufa sasa hivi kuna mrithi wake anaitwa ismail kaan huyu ndo hatari kabisaa juzikati alisimamia mashambulizi ya cyber kwenye manuwari ya marekani
Hahahaha, jiniasi akakutana na ma jiniasi wenzake wakampeleka kuzimu

Sasa hivi naona Republican Guards wanashtumiana tu kuuza info CIA na Mosad ,zilipelekea jiniasi kufa kwa makombora

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom