Elections 2015 Uchambuzi wa ahadi za mgombea urais kwa tiketi ya CCM, Dr. John Pombe Magufuli

TANZANIA YA MAGUFULI

Hii ndiyo Tanzania mpya ya Dr. John Magufuli
1. Vijiji vyote Tanzania vitakuwa na umeme wa uhakika, Rural Energy Argency (REA) imeshaanza kazi hiyo.
2. Wanawake na vijana watapata mikopo kupitia vikundi vyao. Milioni 50 zitatengwa kufanikisha mikopo hiyo inatolewa ili kupunguza umasikini katika ngazi ya familia
3. Madereva wote watakuwa na mikataba ya ajira. “madereva jiandaeni kusaini mikataba nikiingia ikulu”
4. Wanyonge wote watathaminiwa mf: wamachinga na mama nitilie. “serikali yangu ya awamu ya tano haitowaonea wanyonge”
5. Watumishi wa serikali watapata nyumba za kuishi karibu na vituo vyao vya kazi. Nikiapishwa watendaji wote wa serikali wajiandae kuishi kwenye vituo vyao vya kazi, sivyo waache kazi.
6. Kila kijiji kitakuwa na zahanati, kila kata itakuwa na kituo cha afya, kila wilaya itakuwa na hospitali ya wilaya na kila mkoa utakuwa na hospitali ya rufaa
7. Shule zitajaa walimu wa sayansi
8. Miundombinu ya barabara itaimarishwa zaidi na barabara zitapitika majira yote ya mwaka
9. Wafanyakazi wazembe wote watawajibishwa
CHAGUA MAGUFULI MWANA MABADILIKO YA KWELI
 


Magufuli rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
 

Kupata vichekesho hivi Andika #HapaGizaTu kwenda namba 252015
 

Hakuna kipya hapo ambacho Mwinyi, Mkapa na hata JK hakukisema......tatizo si Magufuli tatizo ni mfumo usiotanguliza maslahi ya umma mbele, mfumo uliopofushwa kwa rushwa na hata kuona uuzwaji wa nyumba za serikali hata zilizokuwa karibu kabisa na ikulu ni jambo sahihi lenye maslahi mapana kitaifa.
 

Usifanye vitu kwa mazoea, Magufuli ndo rais wetu.
 

Huyu ndiye Magufuli haswa.
 
Usifanye vitu kwa mazoea, Magufuli ndo rais wetu.

you must be living in a fu.ckin ancient experience.....ccm yako imeifikisha nchi pabovu kwa kufanya vitu kwa mazoea.

kama ubongo wako ni mvivu kuwaza....pale ubungo magufuli alibomoa jengo la TANROAD. Pita pale uone palepale palipobomolewa jengo nini kinaendelea. Imekuwaje leo magufuli aruhusu jengo lianze kujengwa mahali aliposema ni barabarani?.....amelishwa nini kumshawishi otherwise?
 

Magufuli yuko vizuri katika ufuatiliaji na utekelezaji

Tumuamin na atatuvusha
 
Kila mtumishi atapata nyumba karibu na mahala pa kazi wakati alikuwa champion wa kuuza nyumba za serikali mjini na kwenda kujenga makambi bunju na dodoma na kuita nyumba za wafanyakazi.
 
Huyu ni kukariri hana ubunifu wowote. Tunataka innovative pre
 
Mkuu hivi hata dereva wa dala dala yangu kuanzia october 25 atalipwa na serikali ya ccm? au hapo kwenye bold una maanisha nini?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…