Johnny Sins
JF-Expert Member
- Nov 4, 2019
- 2,537
- 3,873
.Ndio roho yake...kila kitu chake..furaha yake imelala kwenye mikono ya binti yake..hakuna anachopenda hapa duniani kuliko kumona mwanae akiwa anacheka...ni kama waliungana mwili,akaipa maana ile kauli kuwa binti jasiri rafiki yake baba...wakaishi hivo...
...Uzuri wake ulisababisha apate mtu wa kumuoa,baba ake alilia sababu alikuwa anatenganishwa na kipande cha mwili wake...akaumia maumivu yasiyokuwa na tiba..maana ataolewa tu iwe au isiwe...
....Ulisukwa mpango na watu waliokuwa wanammezea mate binti yule...wahuni...washenzi...
...Siku moja kabla ya ndoa mtoto wa sanjay dutt anabakwa na watu watatu kwa zamu..huku akirekodiwa picha...mji mzima unajua...siku ya ndoa ndo siku anayomwambia mumewe mtarajiwa kuwa asimuoe amuache maana ye sio msafi tena...ndoa inavunjika katikati ya sherehe...
Machozi aliyotoka baba wa mtoto huyu hayakufananishwa na chochote kwenye maisha yake...sio harusi tu..na aibu..aibu ya kubakwa siku moja kabla ya ndoa na watu wengi..na bado ukaonekana mtaani na mumeo kukuacha siku ya ndoa...sanjay alilia...akalia..akalia tena...
...Siku ya mahakama baada ya kufungua kesi,wahusika waliitwa lakini kesi walishinda...ndIo walishinda sababu kuna sheria na ukweli...mahakamani ilitumika sheria...ukweli ukakosa nafasi...
mbele ya hakimu ikaonekana binti wa sanjay dutt alitengeneza mchezo aonekane kabakwa ili asiolewe sababu hakumtaka yule mume...bali alikuwa akimtaka mmoja katika wale wabakaji...serious!...sanjay dutt akalia tena mtoto wake kuitwa malaya mbele ya hadhara bila kosa lolote maskini...
...Akawaomba radhi wabakaji,mawakili na majaji,...akawaambia atafuta kesi..yaishe...
.....Yes ni kweli yaliisha,yaliisha pale mahakamani...mwanaume akaihamisha kesi uraiani...ni huko ndipo maskini tunajilipa wenyewe...sanjay dutt mla unga..muhuni sana...mwenye chimbo za hatari...akamwambia binti yake naomba ruhusa...binti akamwambia nenda baba..nakuruhusu...
....Ni kwa ruhusa ya binti huyu ndiyo iliyowafanya maaskari waokote maiti zikiwa na sura tofauti...mahakama ikahamia kwenye mikono yake...machozi yake aliyokopesha wabakaji wakayalipa kwa riba...walihama mji,na kuna aliowakata hadi sehemu zilizotumika kumbaka binti yake...
....Mji ukachafuka...mchana baba...giza likiingia anasomea watu vifungu vya sheria za kifo gani wangechagua...ni kisasi adhimu...kutoka kwa baba mwenye mapenzi na binti yake...
#BHOOMI