Uchambuzi wa filamu ya Cube

Uchambuzi wa filamu ya Cube

Johnny Sins

JF-Expert Member
Joined
Nov 4, 2019
Posts
2,537
Reaction score
3,873
Haikuwa bahati mbaya...wala sio ajali kwao...ilitokea kama wamelala na ikatokea wameamka tofauti na walipolala..ni rahisi hivo tu..wakajikuta wapo kwenye chumba kimoja,chenye vyumba vingi..ni complete cube...

......Engineer designer wa majengo..daktari anaeujua nje ndani mwili wa binadamu...askari mwenye kutimiza jukumu lake kwa raia...mfungwa alietoroka maisha ya utumwa gerezani...mwanafunzi mtiifu nyumbani asiekosa mahudhurio shuleni..ndani ya vichwa hivo vitano kuna password inapaswa kufunguliwa na wao...

...Ni chumba baada ya chumba..na pengine ingekuwa rahisi kwao kama vyumba hivi vingefunguka na kuonesha njia ya nje..hapana...havikujengwa ili watu watoke...vipo ili wafe...

...Ndio...ndani ya cube rooms kuna kila aina ya mitego inayomsubiri mteguaji.. ni vifaa hatari visivoonekana kwa macho..kila kosa moja ndani ya cube linachukua uhai wa mtu..na wala hakuna muda wa kusawazisha kosa lako...

...Ni kama mjengaji alikosea..au mmiliki wa vyumba alitoa ramani isiyoeleweka...ila ukweli ni ule ule...ni vyumba vya kifo..na ataetoka salama ni yule ataeuona mlango wa nje akiwa hai...

...Kwanini wako pale!...kwanini wao na sio watu wengine!...hakuna mtu hakuna maelekezo wafanye nini ili watoke ..wakiendelea kukaa watakufa njaa...wakiamua wasife na njaa watakuwa wamechagua njia ya pili ya kuwaua...sababu hakuna njia ya tatu ya kuwaweka hai...

...NI KISANGA...

...Wakijitahidi waamue ushirikiano...na matumizi mazuri ya akili...na kutodharau hata pini utayoiokota....kila kitu humu ndani kimewekwa kwa makusudi..na kinatumika kama sio kwa faida ni kwa hasara...akili ya mtumiaji ndo itaamua..

...Je password zitafunguka!..watatoka!!!..

Image may contain: 1 person, standing and outdoor


Credt: Kaisal Ally
 
Back
Top Bottom