Uchambuzi wa filamu ya You Again

Uchambuzi wa filamu ya You Again

Chachasteven

JF-Expert Member
Joined
Jul 4, 2014
Posts
1,941
Reaction score
2,044
67729509_349337142609314_546115568031409172_n.jpg

You again (2019).

Cast: Mimi mars, Nick Mutuma, Amalie Chopetta, Moriss Mwangi, na wengine wengi.
Director: Nick Mutuma & Natasha Likiman

Uchambuzi:
Hizi ni moja kati ya zile wanaita romantic comedy movies. Zina u serious f'lani hivi lakini lazima zikuache mbavu zikiwa hoi na mafundisho juu. Filamu yenyewe ina dakika 68 na sekunde 37, na niwe mkweli tu, nimeiangalia yote bila kufowadi kwa sababu haiboi na haikeri. Ilitoka mapema tarehe 2 december huko YouTube kwenye channel ya Giraffe Africa films ambao kwa kushirikiana na Darling hair Kenya, na Film Studios ndiyo wanauleta mchongo mezani.

Sasa ipo hivi, Sofia (Mimi mars) na Kingsley (Nick Mutuma), baada ya kumaliza masomo yao ya chuo wanaingia mtaani na kukuta mambo ni tofauti kidogo na waalivyokuwa wanafikiria yatakuwa. Licha ya kuwa na elimu na vyeti vyenye sifa kibao bado mchongo wa kupata ajira ambayo ni salama inakuwa ishu nzito. Shida ni moja, Chuo walikuwa wapenzi na wakati wanamaliza masomo hawakuwa na maelewano mazuri. Kwa hivyo wanaachana na hakuna anaetaka kujua kuhusu mwenzake. Hapa na hapa, hapa na hapa, kama bahati sijui nzuri au mbaya, wanakutana tena baada ya miaka 7 kwenye intavyuu ya kazi na wanakubaliwa wote na ndipo muziki unapoanza. Wazungu wanasema lovers never die, na ni kweli. Japo mwanzo, Sofia na Kingsley wanaonesha kama hawazimiani lakini kama utani wanaweka tofauti zao pembeni na penzi lao linaota mizizi tena. Hatari sana nguvu ya mapenzi.

Mambo yanaenda poa upande wao. Penzi linanoga hadi co workers wengine wanajua kinachoendelea kati yao. Kunae co-worker mmoja amebatizwa jina la Wikipedia si kwa bahati mbaya. Ana balaa huyo. Hakuna data ambayo haifahamu hapo ofisini... Well, pamoja na wao kufurahia mapenzi yao kuna maonyo wanayapata kutoka kwa marafiki ukizingatia ukweli kuwa walikuwa wapenzi zamani wakakorofishana, sasa wanafanya kazi sehemu moja na wanaruhusu mahusiano kati yao ilihali ni jambo hatari sana kwao na kwa kazi yao - Unajua wahenga hawakukosea kusema, Don't dip your pen in the company's ink. Au waliposema, don't get your honey where you get your money. Au waliposema, don't get your meat where you get your bread and butter. Sasa ndiyo yanawatokea puani: Wakiwa dinner, Sofia anaomba simu ya Kingsley, anachokikuta ni balaa. Si balaa dogo, ni balaa zito. Ukiacha ukweli kuwa kiwango cha elimu yake kwenye makaratasi ni kubwa kuliko kile cha Kingsley bado alikuwa analipwa pesa kidogo sana. Hisia zinamshika anashindwa kujizuia analifikisha suala mbele kwa bosi wake. Huko anaombwa rushwa ya ngono and she does not reciprocate, and so she gets fired. Upande wa Kingsley pia anazipata taarifa analeta noma, na kwa kufanya hivyo anafukuzwa kazi pia. Msoto unaanza upya tena. Jambo zuri ni kuwa wanapoteza kazi zao lakini mapenzi yao yanaendelea. Yamkini hiyo ndiyo ilikuwa sababu kubwa ya wao kukutana.

Nimejaribu kuandika kwa ufupi sana ili nisikuchoshe. Kama ningeipa wastani basi kati ya alama kumi naipa 8.5 kwa sababu nyingi tu. Plot na story imekaa vizuri. Sauti na Picha pia ziko poa. Maudhui na kila kilichoelekezwa mle kinaeleweka.! Pia Mimi mars, Ile lafudhi ya Kikenya umeua sana. You are a good actress, i hope i will work with you in a not too distant future. Kazi nzuri sana na hongereni.

Kwa wale ambao hamjaitaza hii hapa:
 
Imeniuma sana kumwona crush wangu akipigwa French Kiss..Namkubali sana Mimi Mars "Chugaqueen"
 
Back
Top Bottom