Uchaguzi 2020 Uchambuzi wa ilani ya CCM kwenye kudumisha Muungano

Uchaguzi 2020 Uchambuzi wa ilani ya CCM kwenye kudumisha Muungano

Joined
Sep 8, 2020
Posts
67
Reaction score
133
ILANI YA CCM 20200-1.jpg
Na Bwanku M Bwanku

CCM kwa miaka 56 toka kuasisiwa kwa Muungano wetu adhimu wa Tanganyika na Zanzibar imeendelea kuthamini na kudumisha Muungano wetu huu wa mfano kote duniani, wa kihistoria na wa kipekee sana kwa kuzidi kuulinda, kuuenzi na kushughulika na changamoto zake zote ili uendelee kuwa bora na imara kwa kuandaliwa kwa vikao maalum vya kamati ya Pamoja ya SMT na SMZ ili kushughulika na masuala ya Muungano.

Sura ya 9 ya CCM kwenye ukurasa wake wa 276, kipengele cha 225 hadi 227 imeeleza kwa kina mafanikio makubwa yaliyopatikana kwenye mambo yote yahusiayo na Muungano huo kwa kuendelea kuufanya kuwa imara kati ya Serikali zote mbili za JMT na SMZ za Muungano na kueleza kwa mawanda mapana jinsi CCM itakavyoendelea kuuimarisha na kudumisha Muungano wa Serikali mbili kwa vizazi vya sasa na vijavyo kama ifuatavyo:-

(a) Kuhakikisha ushirikiano wa wizara/idara na taasisi zisizo za Muungano za Serikali ya Jamhuri ya Muungano (SMT) na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ) katika mambo yasiyo ya Muungano unaendelea kuimarishwa.

(b) Kuimarisha utaratibu wa vikao vya Kamati ya Pamoja ya SMT na SMZ vya kushughulikia masuala ya Muungano kwa lengo la kutatus changamoto kwa kasi zaidi.

(c) Kuhakikisha masuala muhimu ya Muungano yanaratibiwa kwa faida ya pande mbili.

(d) Kuimarisha utoaji elimu ya Muungano kwa umma wa Watanzania ili kuendelea kujenga ari ya kuulinda, kuutetea, kuuenzi na kuuimarisha.

TUMETEKELEZA KWA KISHINDO, TUNASONGA MBELE PAMOJA.
 
Back
Top Bottom