UCHAMBUZI WA JASUSI : Mkutano Wa Amani Ya DRC Jijini Dar: Bosi wa AU Atimuliwa, Wahusika Muhimu Wasusia, Mkwamo Palepale

UCHAMBUZI WA JASUSI : Mkutano Wa Amani Ya DRC Jijini Dar: Bosi wa AU Atimuliwa, Wahusika Muhimu Wasusia, Mkwamo Palepale

bagamoyo

JF-Expert Member
Joined
Jan 14, 2010
Posts
24,941
Reaction score
28,869
Jasusi yupo Dar na Goma virtually akifuatilia yanayoendelea, na ataendelea kukujuza from time to time...lakini leo tuangazie mkutano wa SADC / EAC wa Dar es Salaam


View: https://m.youtube.com/watch?v=9t6awbHDou8

Evarist Chahali, afisa wa zamani wa usalama wa Taif Tanzania TISS aliyegeuka kuwa mwandishi, ametoa mchango mkubwa katika uelewa wa shughuli za uchambuzi wa kina ripoti mbalimbali kwa kuzichanganua na kuweza kuleta maana zake halisi

Makala hii inahusu mkutano wa kati ya viongozi wa nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) na viongozi wa nchi za Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) uliofanyika jana Februari 8, 2025 jijini Dar es Salaam, Tanzania. Makala inazungumzia masuala matatu, kwanza, kutumuliwa kwa Kamishna wa AU Moussa
 
Sasa ndio unasema atimuliwa badala useme atimuliwe?
Amemaanisha mtu kashatimuliwa yeye anaripoti, si kwamba anataka mtu atimuliwe.

Msikilize Jasusi Chahali nimeweka video yake ya Youtube anaripoti jambo hili.
 
Kikao si kilifanyika Jana na maazimio walishayatoa ambayo ni emergency ceasefire ifanyike na M23 waelewane na serikali ya congo. imekuaje?
 
Dar es Salaam, Tanzania

Azimio lafikiwa Mazungumzo ya Luanda na Nairobi kuhusu Amani Congo yaunganishwa kuwa kitu kimoja
Saa 6 zilizopita - Viongozi waliofanya mkutano wa pamoja katika jiji la bandari la Dar es Salaam nchini Tanzania walikubaliana kuunganisha mchakato wa Luanda unaosimamiwa na rais wa Angola mheshimiwa João Lourenço pia na Nairobi chini ya rais Uhuru Kenyatta ili kuharakisha...



Toka maktaba :

Mazungumzo ya Nairobi I na Nairobi II kuhusu Congo chini ya rais mstaafu Uhuru Kenyatta akihojiwa (lugha kiswahili) kuhusu utatuzi wa mzozo wa Congo


View: https://m.youtube.com/watch?v=BI5HRv7WVrA

Uhuru Kenyatta, rais wa zamani wa Kenya, aliyeteuliwa kuwa mwezeshaji wa mchakato wa Nairobi na Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC), anatathmini safari yake ya saa 48 mjini Kinshasa tangu Jumapili, Novemba 13, 2022. Pia inashughulikia suala la usalama mashariki mwa DRC.

Mstaafu Uhuru Kenyatta alikutana na mheshimiwa Rais Felix Tshisekedi wa DR Congo na kiongozi mkuu wa MONUSCO (SRSG-Head of MONUSCO), Bi. Bintou Keita .... kuhusu vita inayoendelea na kuona kwa njia gani wanaweza kusaidiana na wananchi wa kabila mbalimbali na jamii mbalimbali mbalimbali

Mwezeshaji wa mchakato wa Nairobi rais mstaafu Uhuru Kenyatta anasema wakutoka nje wenye maslahi binafsi wanawagawa siyo kwa mapendo bali wanaangalia madini kwa manufaa yao na kuwa bunduki na risasi haziwezi kuleta amani juu ya mzozo wa Mashariki ya Congo

Nimepewa jukumu hili na Jumuiya ya Afrika ya Mashariki EAC kuwa bunduki na risasi haziwezi kuleta ushindi wowote, mimi nimetoka Ethiopia kule wamakubali Tigray na Amhara kuwa bunduki na risasi hazileti amani na ujumbe wangu kwa Congo ni huo huo asisitiza rais mstaafu Uhuru Kenyatta

Jukumu letu kama viongozi ahadi kubwa unayoweza kutoa kwa raia ni usalama wao kwa kuhakikisha hakuna umwagaji wa damu ili watu waendelee na maisha yao ya kujiletea maendeleo

Shida zilizopo zitatuliwe kisiasa na tusiwe na fikra kuwa jamii moja inaweza kushinda pekee bali wakongomani wa aina zote wakae pamoja kwa mazungumzo

Mazungumzo ya mèzani ni muhimu iwe M23 au serikali wote kwa kuweka bunduki chini, njia ya nguvu haitafauli na wala haitaleta ushindi ...
 
08 February 2025
Mdahalo umeandaliwa na DUPSA UDSM

Dr. Richard Mbunda : Historia na Kwanini Mazungumzo Hayafanikiwi Kuleta Amani ya Kudumu DR Congo

View: https://m.youtube.com/watch?v=V8oKaFqiIIA
Mgogoro katika modeli ya chapisho la Profesa Mwesiga Baregu 2011 Obstacles to Peace Actors Interests and Strategies andiko la kuhusu maslahi na kwanini wako kule na mbinu wanazotumia ili kuweza kupata ufumbuzi wa kuleta amani .. nchi wahusika kwa sasa nchi ya Congo na jirani wake Rwanda, Burundi, Uganda.

Pia nchi za mbali Scandinavia, China, France na wahusika wengine wasiokuwa nchi kama CNDP, MLC, MaiMai, M23 n.k waliosaini makubaliano ya Machi 23 2009

Makundi ya nje FDLR kutoka Rwanda Wahutu 20,000 waliongia Congo .. ADF waasi wa Uganda walioingia Mashariki ya Congo kuishambulia Uganda, Lord Resistance Army ya Joseph Konyi walioingia Kaskazini ya Congo baada ya kukimbia Uganda, RED-TABARA wa Burundi n.k

Je hawa wote hapa juu nchi jirani, nchi za mbali, makampuni ya kimataifa na makundi ya waasi wa Rwanda, Congo, Burundi na Uganda wanamaslahi gani Mashariki ya Congo ...

More info :
Understanding Obstacles to Peace: Actors, Interests, and Strategies in Africa's Great Lakes Region
Book by Baregu Mwesiga

1739114136423.jpeg
 
Amemaanisha mtu kashatimuliwa yeye anaripoti, si kwamba anataka mtu atimuliwe.

Msikilize Jasusi Chahali nimeweka video yake ya Youtube anaripoti jambo hili.
Kumbe kashatimuliwa
 
Viongozivwa Kongo ni wabaguzi
 
Back
Top Bottom