Nanyaro Ephata
JF-Expert Member
- Jan 22, 2011
- 1,234
- 1,815
Kitabu.Parenting with Love and logic
Mwandishi.Foster Cline & Jim Fay
Mchambuzi.Nanyaro EJ
Utangulizi
Mwandishi anasema kuwa swala la malezi ni mjadala mpana na ambao hakuna njia moja yenye manufaa kwa asilimia mia moja.Hivo kitabu hiki kitajikita kwenye mbinu mbalimbali ambazo zimefanyiwa tafiti na kuwa na matokeo tarajiwa.
Wazazi wengi wamekutana na changamoto nyingi katika malezi!na pale changamoto inapotokea hujikuta wakikata tamaa na kulaumu upande mwingine,hulaumu shule,jamii,ndugu mke/mme na hujilaumu sana kuwa sijui hasa huyu mtoto ana nini! Etc
Mwandishi anasema ni muhimu kuelewa kuwa nyakati zimebadilila sana,kuanzia haki za binadamu! Mawasiliano ya habari,teknolojia uwepo wa simu za mikononi etc ni miongoni wa vitu ambavyo vimebadili mtazamo wa watoto kwenye maisha ya kila siku.Hali hii huwalazimisha watoto kukua haraka kuliko huko nyuma!watoto wanajua mambo mengi kuliko miaka ya nyuma
Mwandishi anasema lazima wazazi wajifunze namna bora ya makuzi ya watoto kwa kuzingatia nyakati za leo!Hapa ndio makuzi ya LOVE & logic yanapokuja,makuzi na malezi lazima yazingatie upendo! Lazima yazingatie na yajengwe juu ya msingi unaoitwa love na logic.Ufanisi katika makuzi na malezi unategemeana sana na namna unavozingatia kanuni hii,ila uwe upendo unaoendana na adabu,heshima,na upendo ambao unaweza kukubali na kuruhusu mtoto kufanya makosa,upendo wenye uvumilivu,upendo…….Makosa mengi yana logic lazima kuruhusu mtoto achambue logic kwenye kosa husika
Hivyo basi kitabu hiki kimeandikwa ili kutoa majibu ya njia sahihi katika kuleta malezi na makuzi mwafaka,utajifunza jinsi ya kutenganisha changamoto za watoto,jinsi ya kuzuia hasira na kubishana na mtoto,pia utajifunza jinsi ya kutumia maneno fikirishi na maelezo yenye tija,kutoa fursa mbalimbali kabla mtoto/watoto hajajiingiza kwenye makosa makubwa.Matokeo tarajiwa yatakuwa ni uwezo wa mtoto kukua katika uwezo wa kufikiri,na kufanya uamuzi ambao wataweza kuishi nao,itawajengea watoto uwezo wa kuwajibika nah ii ndio maana halisi ya makuzi na malezi!Tukifanikiwa tu kuwafundisha watoto uwajibikaji tutakuwa tumetimiza sehemu kubwa sana katika makuzi na malezi
Maandiko matakatifu katika Mithali 22.6 inasema mlee mtoto katika njia impasayo nae hataiacha hata akiwa mzee
Kitabu.Parenting with Love and logic
Mwandishi.Foster Cline & Jim Fay
Mchambuzi.Nanyaro EJ
Chapter 1 Parenting: Joy or Nightmare?
Mwandishi anaanza kwa kunukuu Bibilia takatifu Mithali 13.1 Mwana mwenye hekima husikliza mausia ya Babaye,bali mwenye dharau hasikilizi maonyo
Anasema kwenye mgahawa fulani alikuwepo Baba na mama wakiwa na mtoto wao wa miaka mitatu,sasa wakati wanaondoka wazazi wale walitumia zaidi ya dakika kumi na tano kmtaka mtoto wao wa miaka mitatu apande kwenye gari lao ili waondoke,huku mtoto akiendelea kukaidi.Ilibidi baba mzazi apige magoti kumwomba mtoto wake wa miaka mitatu kukubali apande garini ili waondoke,licha ya kupiga magoti mtoto alimgomea baba yake hadi baba alipotoa ahadi ya kununua SODA ndipo yule mtoto wa miaka mitatu alikubali kuingia kwa gari
Swali ikiwa wazazi hawa wanalazimika kununua soda ndio mtoto wao wa miaka 16 akubali je watalazimika kufanya nini mtoto huyu akifika miaka kumi na sita?
Kwa upande mwingine kulikuwa na mama kwenye eneo fulani akiwa na mtoto wake wa kiume wa miaka mitatu pia,sasa huyu mama alikuwa anamkataza mtoto wake aliyeitwa Logan akisema Logan usiende huko,usifanye huo mchezo Logan….oohh Logan ntakuchapa usiponisikiliza…..oohh Logan mbona husikii? Alimradi mama aliendelea kumsihi mtoto wake lakini mtoto hakusikia alienda hadi kwenye kiti alichokuwa ameketi abiria mwingine wa kiume..yule mwanmume mtu mzima akamwuliza yule mtoto wa miaka mitatu Je mama yako atakufanya nini maana hujamsikiza?mtoto akajibu kwa ujasiri hatonifanya chochote….yule mama alimfuata huyu abiria wa kiume na kumtaka radhi akifikiri pengine mtoto wake amemchafua au kumsumbua na kuanza kusema niwie radhi tu,unajua hawa watoto wakiwa nan umri huu huwa wasumbufu na hawasikii kabisa
Hawa wazazi wote wawili ni kielelezo cha malezi na makuzi yasiyozingatia weledi,kiasili mtoto anapozaliwa anakuwa ni mtegemezi wa wazazi kwa asilimia mia moja,wazazi ndio kila kitu kwa watoto,kuna mambo wanajifunza kwa wewe mzazi kuwaambia au wao wenyewe kuona matendo na maneno na mienendo yako! Ndio pahali unapaswa kumfanya mwanao afikiri,na afikiri sawasawa.. makuzi na malezi ya Love and Logic yamejengwa juu ya falsafa ya kumsaidia mzazi/wazazi kushinda,wazazi watafanikiwa kuwaelekeza watoto wao bila kulazimika kutumia ahadi za pipi/soda au zawadi ingine au vitisho(Uswahili unaambiwa kula au niite fisi au polisi).Chini ya falsafa hii mtoto hujiona mshindi kwa kuwa hujifunza uwajibikaji na maana halisi ya maisha