Uchambuzi wa Tatizo Katika Uibuaji wa Mradi (Problem Analysis in Project Planning)

The Consult

JF-Expert Member
Joined
Jan 20, 2017
Posts
220
Reaction score
252

Uchambuzi wa Tatizo (Problem Analysis) ni hatua katika kipengele cha Uchambuzi wa hali halisi (Situational Analysis) wakati wa uibuaji wa mradi. Katika elimu ya miradi, tunaamini kwamba; kadiri unavyolitambua tatizo ndipo urahisi wa uibuaji na utekelezaji wa mradi hutokea.
Uchambuzi wa tatizo katika uibuaji wa mradi, huzingatia mambo makuu matatu (3) ambayo ni;
  • Tatizo lenyewe (problem); hii ni hali isiyoridhisha (negative situation) ambayo ina athari katika ustawi wa mtu mmoja mmoja au kundi la watu, mfano; Ongezeko la Mimba za Utotoni (high pregnancy rate among teenage girls)
  • Vyanzo (Causes); hivi ni vitu vilivyopo katika jamii ambavyo husababisha uwepo wa tatizo. Vyanzo huweza kuwa tabia (behaviour),mtazamo (attitude), hali (situation) n.k. Vyanzo vya tatizo vimegawanyika katika sehemu kuu mbili ambazo ni vyanzo vya nje (underlying causes) ambavyo huonekana kwa haraka zaidi, kwa mfano wa tatizo la mimba za utotoni; sababu za nje tunaweza kusema, "Wasichana wengi kutotumia njia za uzazi wa mpango" n.k . Aina ya pili ya vyanzo hujulikana kama vyanzo mzizi/halisi (root causes), kwa mfano wa tatizo la Ongezeko la Mimba za Utotoni, chanzo halisi tunaweza kusema ni tamaduni (cultural norms) za jamii husika ambazo haziruhusu matumizi ya njia za uzazi wa mpango. WAFADHILI WENGI HUTOA FEDHA KWA MIRADI INAYOJIKITA NA VYANZO HALISI VYA TATIZO.
  • Madhara yatokanayo na tatizo (consequence); hii huweza kuwa hali ya kiuchumi, kijamii au kiutamaduni ambayo husababishwa na uwepo wa tatizo. Mfano kwa tatizo la Ongezeko la Mimba za Utotoni; madhara yake ni pamoja na Ongezeko la idadi ya vifo (mortality rate) n.k
NAMNA YA KUCHAMBUA TATIZO (HOW TO ANALYZE A PROBLEM)
Njia rahisi ya kufanya uchambuzi wa tatizo ni kujiuliza swali la "WHY" kuna tatizo fulani? jibu utakalopata utajiuliza tena "WHY" ? utaenda kwa mtiririko huu mpaka utakapofikia hatua ya kwamba "there is no WHY's answer", na hapo utakuwa umeweza kupata aina zote mbili za vyanzo vya tatizo (underlying causes & root causes), mara nyingi mti wa matatizo (problem tree) hutumika katika kufanya uchambuzi huu.

Wakati mwingine, uchambuzi wa tatizo huweza kuja na vyanzo vingi vya tatizo (full range of causes) kiasi cha kukuchanganya katika kuchagua "cause" ipi kwa ajili ya ku-design mradi wako. Unapokuwa katika hali hii, ni vyema ukaangalia upatikanaji wa rasilimali (availability of resources), uwezo wa taasisi (organization capacity), kutamalaki kwa chanzo (magnitude) n.k kama vigezo katika kuchagua chanzo kwa ajili ya kubuni mradi wako.

Ahsante

KARIBU KWA HUDUMA ZIFUATAZO;
  • Kupatiwa taarifa za fedha (Grants, (Awards for Start-ups/Entrepreneurs)), Kuandaliwa Mchanganuo wa Mradi (Project Proposal, Business Plan/ Concept Paper Preparation) na kutumiwa Maombi/Mchanganuo wa Mradi wako kwa mfadhili.
  • Kuandaliwa Mipango Mkakati (Strategic Plans) na Mipango ya Utafutaji wa Fedha (Fundraising Plans)
  • Utoaji wa mafunzo mafupi (trainings) katika Uibuaji na Usimamizi wa Miradi (Project Planning and Management), Usimamizi wa Mipango Mikakati (Strategic Management) na Mbinu za utafutaji wa fedha kwa ajili ya miradi na biashara (Fundraising Strategy)

The Consult ; +255 719 518 367
E-mail; theconsult38@gmail.com
Dar es Salaam

Tanzania
 
Natarajia kuwa mwanafunzi wako
 
Natarajia kuwa mwanafunzi wako
Karibu Sana Chief. Huwa natoa mafunzo kwa mtu mmoja mmoja pia, ima ya masafa (na mara nyingi hutumia simu, katika muda maalum tuliokubaliana na mteja) ama kukutana na mteja "physically"

"Additional Package"
Kwa mtu anayehitaji kujifunza namna ya kuandaa Mchanganuo wa Mradi/Biashara, huwa namuwezesha (through consultation, just freely) ku-transform his/her idea into a complete Project/Business Proposal pamoja na kumpatia taarifa juu ya current funding source inayo-match na nature ya mradi wake ili aweze kutuma andiko lake.

Again, Karibu Sana Chief.
 
Wazungu lakini bado wanafinance miradi ya wabongo?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…