1. Mtu kutofahamu lugha nyingine vyema(yaani anaongea kiswahili, lakini ni lugha yake ya pili au ya tatu).
2. Mtu ambaye lugha yake ya Kiswahili ni ya kwanza lakini bado ina mapungufu(ukosefu wa maneno kwa ufasaha zaidi).
3. Tabia: Kwa wale wenye tabia ya kuongea lugha ya kigeni(mf. Kiingereza/Kifaransa/Kihispania/Kidachi n.k) kwa kuhisi itawafanya wawe katika tabaka fulani(hasa watu wa juu/wenye uelewa n.k) katika jamii.
4. Mazoea: Yaani mtu kutumia maneno kwa kusikia kila mara mtu akiyatumia bila kuwa na uelewa au ufahamu kuwa ni maneno ya lugha ya kigeni.