Lucas Mwashambwa
JF-Expert Member
- Jul 28, 2022
- 28,722
- 20,610
Ndugu zangu Watanzania,
Uongozi ni kugusa maisha ya watu, ni kuleta tabasamu, furaha, na matumaini kwenye maisha ya watu. Ni kufanikisha na kuwezesha kutimizwa kwa ndoto za watu, ni kukidhi matarajio na kukata kiu ya watu, na kuwapa watu vicheko vya furaha na kuacha alama katika mioyo yao.
Uchapakazi na uongozi wa Rais Samia umeonekana kuwakosha, kuwagusa, na kukonga mioyo ya vijana wengi sana waliomaliza kidato cha sita. Hii imepelekea wengi wao kutafuta kadi za CCM usiku na mchana ili waweze kuwa wanachama wa CCM kama sehemu ya kumuunga mkono Rais Samia, ambaye ni Mwenyekiti wa CCM Taifa.
Vijana ambao nimekutana nao wameongea kwa hisia kali sana kutoa shukurani zao kwa Rais Samia kwa hatua yake ya kufanya maamuzi magumu ya kutoa elimu bure hadi kidato cha sita. Wengi wao, kutokana na vipato vya wazazi wao, hawakuwa na matumaini kama wangeweza kufika hapo isingekuwa elimu bure.
Wanasema kitendo cha Rais Samia kufuta ada na michango mingine kiliwafanya kuelekeza mawazo na akili zao zote katika kusoma kwa bidii na kufanya vyema katika masomo yao, pasipo kuwa na hofu ya kufukuzwa na kurudishwa nyumbani kuchukua ada na michango mingine kama ilivyokuwa zamani.
Katika hili, nami nawaunga mkono vijana hawa katika kumshukuru sana Mheshimiwa Rais wetu mpendwa na Jemedari wetu kipenzi Daktari Mama Samia Suluhu Hassan kwa uamuzi wa kufuta ada, ambayo imekuwa ni neema na nuru katikati ya giza kwa familia nyingi sana. Leo, hata mtoto wa maskini ana uhakika wa kupata elimu na kutimiza ndoto zake.
Tofauti na sisi wakati wetu, tuliteketeza mali nyingi sana kuanzia mifugo hususani ng'ombe, mashamba, na kuingia madeni kwa ajili ya kulipia ada na michango mingine iliyokuwa mingi. Hali ya kiuchumi, hususani vijijini, ilikuwa mbaya sana kuweza kumudu gharama hizo ambazo sasa zimebebwa na Jemedari wetu Daktari Mama Samia.
Katika hili, nasema Rais Samia, Mama yangu na Rais wetu mpendwa, utakumbukwa na maelfu ya vijana kwa kuwawezesha kutimiza ndoto zao bila shida. Kikubwa, nakuomba sana Mheshimiwa Rais na serikali yako kuwa zinapokuwa zimetoka ajira, hususani za ualimu, basi jitahidini sana kwa jicho la huruma kuanza kuwapa kipaumbele wale vijana waliomaliza miaka ya nyuma hasa wale wa mwaka 2015, 2016, na hata wale wa 2017. Hii ni kwa kuwa huwa inawaumiza sana vijana waliomaliza mwaka 2015 na 2016 wanapokosa ajira, halafu aliyemaliza hivi karibuni anapata ajira na kwa masomo yale yale ambayo amesomea huyu wa 2015 na 2016.
Naamini serikali yako, Mheshimiwa Rais, italizingatia jambo hili. Fikiria hata wewe, Rais wetu ambaye ni mzazi mwenye huruma kama unavyofahamika na wengi, unaweza jisikiaje mtoto wako amemaliza ualimu 2015 au 2016 na hajapata ajira mpaka leo hii, licha ya kuwa na ufaulu mzuri na kukidhi vigezo vyote na ulimsomesha kwa shida, taabu, na mateso makubwa. Halafu anakuja anapata ajira wa juzi juzi tu na kwa masomo yaleyale na ufaulu ule ule.
Kazi iendelee, Mama ametufikia na kuwafikia Watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa maisha ya Watanzania wanyonge wasio na sauti.
Lucas Hebel Mwashambwa, Mama ANATOSHA kuendelea kuliongoza taifa letu kwa muhula wa pili.