Sheikh23
JF-Expert Member
- Jul 11, 2016
- 1,175
- 1,934
Wakuu Habari ya Jumapili...
Niende moja kwa moja kwenye mada,miaka ya karibuni kumezuka mtindo mpya wa maisha ya kusifia watu Mbele ya camera na kupewa pesa,wenyewe machawa wanaita "kuokota".
Vijana wengi wamekua wakidhani hayo ni maisha halisi bila kujua scene nyingi ni maigizo,matangazo au Kiki tu.
Mbaya zaidi machawa hawa au ma_influencer wamekua wakidhihaki wasomi na usomi (ELIMU) hivyo kuaminisha vijana kua usomi hauna future (maokoto/maisha Bora) kitu ambacho sio kweli.
Rai yangu ni kuwa mentality hizi zikiachwa ziendelee kupandikizwa zitaua jitihada za vijana wetu kwenye kuisaka ELIMU.
Kama Taifa tusiruhusu vijana na jamii iamini kwenye uchawa na ujanja ujanja wa mjini kama mfumo wa kupata pesa za haraka.
Kama Taifa pia tusiruhusu watu wachache kwa umaarufu wao mitandaoni waeneze propaganda hasi zenye kudogodesha au kuua Hali ya ubunifu,kujifunza na uwajibikaji kwa jamii na kizazi chetu.
Naomba kuwasilisha....
#PINGA MACHAWA NA UCHAWA KWA MASLAHI YA TAIFA