Uchawa unaangamiza Taifa

Uchawa unaangamiza Taifa

Joined
Dec 15, 2022
Posts
18
Reaction score
128
Hakuna jambo linaondoa UTU WA MTU kama hichi kinachoitwa uchawa,Uchawa ndani yake umeficha maovu,umeficha ukweli,umeficha uzalendo na umeficha uMungu,kwa tafsiri ya chawa ni mtu aliyetayari kutokemea uovu au jambo lisiloenda sawa kwa sababu tu ananufaika.

Chawa akimganda mtu haijalishi aliyegadwa anaumia kiasi gani bali chawa anaangalia maslahi yake binafsi ni jinsi gani ataendelea kufyonza Damu,hasara za Uchawa kwa vijana ni kubwa sio tu kwa vijana Bali kwa Taifa kwa ujumla.Hata ma kanisani kuna uchawa sikuhizi,ifike mahali uchawa uwe ni dhambi kama ilivyo dhambi ya Uzinzi....
 
Chawa wa mama, mitano tena
IMG_20250127_095508.jpg
 
Adabu IPO, hata hata hao machawa uliwaambia ukweli watakuja juu kama nyie, badilikeni, zamani hamkuwa hivi
 
Taifa liwena maadui wanne 1.Ujingq 2.Usmakini 3.Maradhi 4.Uchawa
Hii ni sawa kabisa.

Haiwezekani watu hawataki kufanya kazi kwa weledi wanafanya vitu vya kutweza hadi utu wao kufurahisha watawala.

Ona ujinga kama huu hapa pichani.
Snapinsta.app_461054338_545471604565975_8071883766470126917_n_1080.jpg
 
Uchawa unalipa mkuu, sema hujapata hiyo nafasi adhimu !! Kuna machawa wenye maisha standard kuliko mfanyakaz/mtumishi mwenye salary yenye tarakimu sita !! Na wengine wamejenga, wamewekeza kwa huo huo uchawa ! Tuishi humo, fanya unachoona kinakufaa, usimfurahishe binadam mwenzio kuogopa atakuonaje n.k !

Case study,,,mengele, mwijaku , baba levo na walee wenzetu wengine
 
Chawa ni mtu aliye tayari kudhuru yeyote utakayemkataa au kunyenyekea yeyote utakaye mkubali pasipo kutumia milango ya fahamu.
Pia chawa yapo tayari kutokomea pale mamlaka yako inapokoma na kuangalia ni wapi akajibanze tena ili aendelee kupata damu ambayo ndio uhai wake.

Kwa kiasi kikubwa chawa wameanzia duniani kutokana na njaa, lakini kuna chawa ambao wanakua chawa si kwa sababu ya njaa tu bali wanakua chawa ili wapate sehemu ya kujificha wao na maovu yao.

Kwa upande mwingine chawa na mwenye chawa tabia zao ni moja kwakuwa, mtu mwenye haki haambatani na chawa bali huwakemea nao wakatambua makosa yao.
 
Back
Top Bottom