Uchawi na mizimu inasaidiaje mtu kufanikiwa?

Uchawi na mizimu inasaidiaje mtu kufanikiwa?

makolola

JF-Expert Member
Joined
Sep 15, 2014
Posts
765
Reaction score
289
Wadau nataka kujua vitu hivyo vinaweza kutumika kumfanya mtu akafanikiwa na ni namna gani mtu ambaye hajihusishi navyo anaweza kuzuia ili visimuharibie biashara zake.
 
ndio vipo...mbona watu wanapata nyota ya kupendwa sijui nw wananyumba na magari na mashamba hapa mjini, ila ndio hivyo, masheria kibao, peleka kichwa cha kondoo, samaki wa njano etc LOL..kama hujihusishi unaweza kuzuiza kwa kusali tu, omba protection kwa Muumba wako, bila hivyo kila mtu yuko vulnerable..hivi ndivyo ninavyoamini
 
Wadau nataka kujua vitu hivyo vinaweza kutumika kumfanya mtu akafanikiwa na ni namna gani mtu ambaye hajihusishi navyo anaweza kuzuia ili visimuharibie biashara zake.

imefikia wakati sasa kuna mawazo tunapaswa kuyafuta kwenye vichwa vyetu. vitu kama mizimu, majini, jehnamu, shetani n.k havipo kwenye huu ulimwengu. ukifuatilia kwa makini utakuta vimeumbwa na binadam kutia hofu wengine wawe misukule wao. waliojitambua wanawatia hofu wengine ili kujipatia kipato. ombi langu ndugu jitambue
 
Ukiamini tu hakuna mtu anaweza kukuroga kutokana na nguvu ulizonazo umemaliza mchezo.
 
Vitu hivyo kamwe haviwezi kukusaidia Ufanikiwe. Utajiri unaoletwa kwa njia hyo haudumu kamwe na utakutesa sana. Juu ya agano utakaloingia huwezi kutoka utakufa.. Masharti na Sadaka utakazotakiwa kutoa. Vitu hvyo vitakuletea Umaskini wa Kimwli na Kiroho hapo baadae hvyo usithubutu kufanya hivyo. Bora ukaridhika na Hali uliyonayo na kidgo unachopata na Ukabaki na Furaha na Amani. Utajiri mzuri unatoka kwa Mungu peke yake. Fanyakazi kwa bidii kuwa karibu na Mungu.. Hakika hakuna kitakachogusa Biashara yako.
 
mbona kuna wengi husema vinahusika?
 
Kuna aina mbili za fikra.
1. Sahihi(positive au affirmative)
2. Potovu (negative)
Ukifikiri vizuri utapata matokeo mazuri. Na ukifikiri vibaya utapata matokeo mabaya.

Chochote kile utakachofanya na kufanikiwa, utakuwa ukifikiri na kutenda sahihi. Ukifanya na ukashindwa ulifikiri na kutenda vibaya.
 
Wadau nataka kujua vitu hivyo vinaweza kutumika kumfanya mtu akafanikiwa na ni namna gani mtu ambaye hajihusishi navyo anaweza kuzuia ili visimuharibie biashara zake.
Vinaweza kukusaidia na ukafanikiwa sana Kama ukifuata masharti yake lakini Kumbuka unaingia kwenye maagano ambayo yatakutesa sana
 
Back
Top Bottom