Uchawi ni nini? (Roho, Nafsi, Mwili)

Uchawi ni nini? (Roho, Nafsi, Mwili)

Surya

JF-Expert Member
Joined
Jun 7, 2015
Posts
8,774
Reaction score
13,566
Nitajitahidi nitumie lugha ya kiswahili, waswahili wote tuelewane vizuri.. pia nitajitaidi nitumie maneno machache kufikisha ujumbe au elimu kubwa na pana kumuhusu Binadamu na uchawi au ushirikina (Shiriki)

Kwanza unatakiwa ujue wakati Mungu anamuumba mtu hapa duniani haikuwa kazi yake au uumbaji wake wa kwanza,

Tayari kuna viumbe wengine wengi walikuwepo, yani kwamba tayari kuna Malaika(roho) mmoja aina ya Kerubi alifukuzwa atoke karibu na uso wa Mungu, nae ndie tunamuita shetani na majina mengine mengi mabaya.

Kama tulivyo sisi binadamu tulivyo unaweza zaliwa kwenye familia fulani mfano ya kimasai, lakini ukaamua tu kutoka na kwenda mbali na watu wa kwenu, hiko hivo hadi kwa viumbe kama Malaika(roho) Malaika waliokataa Kumtii Mungu na kukataa kumsujudia Mtu aliyeumbwa kwa mfano wa Mungu basi wakafukuzwa kwenye makao yao.

Pata picha hapo, Ulimwengu ni mkubwa sana una makao mengi sanaaa, (Elon Musk ana chimbo anafukuzia na yeye)

Kwahiyo Mungu yeye kaweka utaratibu kwamba atakayekiuka maagizo ni unatupwa mbali na uso wake.

(Ati kuna raha ya Ajabu sana kuwa karibu na uso/utukufu wa Mungu)

God the Creator, Yani Mungu anamajina mengi sana aelezeki kwa kifupi.

Turudi kwa Mtu(roho)
Mungu alianza kuumba roho ya binadamu kwanza(biblical) na kumpa utawala, kutawala mbingu na nchi na vyote vilivyomo.

kisha Mungu akaita umande na mvua katika nchi hapa ndipo vitu vya kuonekana kwa macho ya mwilini vilianza kuumbika.
Vilianza kutamkwa na kutokea katika ulimwengu usio onekana na mwili (ulimwengu wa roho) kila jambo linaanzia rohoni.

mvua ikadondoka miti ikachipuka, kisha sasa Ndipo mwili ukatengenezwa kuoka kwenye mavumbi ya ardhi (udongo)

Kwanza yalianza maneno(words) kisha
maji na udongo kuungana Mungu anachipua Mimea,
Tena kupitia udongo na Maji akatengeneza mwili wa mtu.
Alipo pulizia Pumzi yake mwili mtu(roho) akawa nafsi hai.

Nafsi ya mtu ni zaidi ya DNA ya mtu, kisayansi inaeleweka kuwa damu hubeba oksijeni, kwahiyo Nafsi ya mtu inamahusiano makubwa na damu ya mtu, Mwanadamu hawezi kufanya lolote na mwili wake pasipo kushirikiana na damu, bila damu mwanadamu ni maiti, ila ukikosa mguu tunakuita kilema.

maji + udongo = mimea
maji + udongo = mwili wa mtu

Nafsi.
Katika nafsi, zinakaa Akili.

Kwahiyo Adamu alipoanza kutembea katika ulimwengu wa mwili, alikuwa empty brain yani alikua hajui chochote kuhusiana na dunia lakini nafsi yake ilikuwa na uwezo mkubwa wa kusikiliza taarifa zinazotoka kwa bwana mkubwa Roho na kuzifanyia kazi akilini kisha kutenda sawa na maagizo.

Adamu hakuwa na mshauri zaidi ya Mungu, na walikuwa na mahusiano mazuri tu na Mungu, na uhakika walikuwa wanapiga story hasa adamu akiwa usingizini, nafsi inapata wasaa mzuri wa kusikia na kuona katika ulimwengu wa roho, kwani mwili unakuwa off. (Namna ya Kupokea taarifa au kuongea na viumbe visivyoonekana hii ni elimu pana nyingine) ikae kando kwanza.

Ili kuishi Miaka 60, miaka 20 niya usingizi.

So, adamu alikuwa hivi tu peke yake analala anaamka yeye ndie mtawala
bc81a3bf-34c3-4ff1-9424-937aeeda861f.png

Angalia hii picha hapo utaona mtu roho ambae ni Adamu, Mungu alikuwa ameweka hatima yote ya dunia ndani yake, hizo rangi rangi nimeweka ni kuonesha karama au zawadi au Maisha ambayo Mungu alimpangia adamu awenayo na ayaishi na ayafanye.

Lakini huku mwilini, Adamu alikuwa kawaida tu hana chochote, hakuwa na mke wala watoto, lakini tayari rohoni kapewa.

Ndipo Kupewa usingizi mzito na kutengenezwa kwa mkewe, kwanza kabla ya kumpata mwanamke, Mungu alitengezeza miili ya wanyama kwa mavumbi na wale wanyama walipokuwa mbele ya uso wa adamu Aliwapa majina.

Kwahiyo Utagundua Taarifa adamu alikuwa anazipata kutoka ulimwengu wa roho... hakukuwa na vitabu, shule, kiti wala nyumba wala cha nini.

Roho:
Eva hakukutana na nyoka na kudanganywa unaweza ukafikiri ilikuwa ni huku upande wa mwilini, lakini hapana, ilikuwa ni rohoni ambapo shetani
(roho) akamdanganya mwanamke

Eva nae akasema sasa leo na mimi nakwenda kumpa Mume wangu taarifa mpya yani nimekutana na liroho huko likanipa madini mapya yani hapa mimi na mume wangu lazima tukafanane na sir. God

Kosa lile lile kama la shetani, kiburi unataka uwe juu kuliko aliyekuumba.

kwahiyo walidanganywa na roho, kama mababu zetu wanavyodanganywa na roho (mizimu) na kupewa maagizo na kutekeleza hadi leo hii.

Unatambua sasa mwanadamu akawa na maarifa ya kujua Jema na Baya ni lipi, mwanzo alikuwa anafanya tu sawa na maagizo lakini sasa anauwezo wa kujua lile ninaloambiwa kufanya ni jema au baya, Wema ni kufanya jambo kwa ajiri yako na wengine, Lakini ubaya au uwovu ni kufanya jambo ambalo linakwenda kumuumiza mwengine kwa sababu fulani fulani.

Na moja ya Utashi ambao Mungu kampa binadamu ni Kuchagua nini cha kufanya hapa duniani.

Mtu wa kwanza kuuwa alikuwa ni Kaini, akamuuwa pacha wake, wazo hilo alitoa wapi ?

Tayari kuna Vita Mungu karuhusu kati ya Shetani na Hatima ya Adamu na kizazi chake.

Kwahiyo Mtu ni roho anayo nafsi Anakaa ndani ya mwili.

Nafsi imegawanyika mala tatu
1. Akili
2. Maamuzi
3. Hisia.
..............
bc81a3bf-34c3-4ff1-9424-937aeeda861f.png


Taarifa/Maagizo/Mawazo
unayotekeleza hapa duniani unayapata wapi ? kwa wachawi uliowakuta dunia au Kwa roho za mizimu ? au kwa kumuiga baba yako mzazi wa mwilini ?

Nafsi au akili zako zipo katikati zinatakiwa kufanya maamuzi, unatizama na kusikia kutokea mwilini ? au unasikia na kuona kutokea rohoni ?

Uchawi...
Nisirukie kwenye uchawi kwanza moja kwa moja maana nitawaacha watu njiani wasielewe

Nikuoneshe adhabu ya Shetani.
Kwa tafsiri yake.


Mwanzo 3:14
BWANA Mungu akamwambia nyoka, Kwa sababu umeyafanya hayo, umelaaniwa wewe kuliko wanyama wote, na kuliko hayawani wote walioko mwituni; kwa tumbo utakwenda, na mavumbi utakula siku zote za maisha yako;

[15]nami nitaweka uadui kati yako na huyo mwanamke, na kati ya uzao wako na uzao wake; huo utakuponda kichwa, na wewe utamponda kisigino.

Shetani ni jeshi kubwa, roho zilizo hasi ni nyingi tu, na baada ya Adamu kula Tunda sasa zina kibali cha kupiga vita na binadamu (kwahiyo tupo uwanja wa vita)
~ Kalaaniwa.
~ Kwa tumbo utakwenda: haya maneno tafsiri yake ni kwamba shetani kila akitembea na kupiga hatua atakua akitembea kwa kazi moja, yani kutafuta chakula.
~ Kula mavumbi - Kumbuka kutoka katika ardhi, Mungu alifanyiza mwili wa mtu, wanyama na ndege.
~ Mtu atamponda kichwa shetani - yani tunatawala juu yake.
~ Shetani atawinda kisigino - Maana yake shetani kazi yake ni kuhakikisha hufanikishi lile ambalo Mungu alipanga ufanikishe hapa duniani. atawinda njia zako kuziharibu.

Si kuzuri hapa dunia, vita ni vita mula

Kwahiyo kama Mungu anavyoitaji kafara ya damu kama Sadaka hapa dunia ili kutawala, na Shetani au Miungu, inahitaji damu kama chakula kizuri cha Kumpatia nguvu ya kutawala dunia.

UCHAWI ni nini? Nakupa tafsiri nyepesi

is to alter someone soul in order to operate in certain condition.
Uchawi ni maombi ya kubadilisha nafsi ya mtu ili ifanye kazi katika hali fulani. kwa kutumia(vifaa) maneno, mimea/wanyama (chakula), na roho.

Katika ulimwengu wa roho kuna roho nyingi sana. wale wazee wa nightmare mna ushaidi wa kusumbuliwa.

Kwahiyo roho chafu ikimuingia mtu nafsi yake inakuwa kifungoni na kufanya mambo kwa bila idhini binafsi.

Wafungwa ni wengi,

Wachawi ni mengiiiii,

Kuna wachawi wanaojijua kuwa sisi ni wachawi na kuna wengine hata hawajijui kama niwachawi, ila wanatumika kufanya uchawi hapa duniani.

Tunaona wachawi wanakuq na mbinu nyingi, maagizo wanaoteshwa huko wengine, wengine wanafundishwa na watu mwilini kabisa.

Ukimdanganya mtoto wako au jirani yako kwa sababu za kibinfsi huo pia tunaita Uchawi, ni maneno tu bila mzizi wowote wala kizimba.

Niendelee na Uchawi?

Unaweza kufanya jambo kwa upendo na kwakupenda, kutokana na msukumo wa ndani na kuona kuwa ni wajibu wako, kumbe uchawi umetumika kukupa hiyo hurka.


Jinsi gani hatima/Kipaji/karama ambayo Mungu kamzawadia mtu inaweza kuibiwa kishirikina..?

Tunaendelea..l
 
Uzi ni mzuri hongera sana,,ila naomba nikuchallenge kidogo...Shetani hakuhukumiwa Kwa kumdanganya eva,, alivyomtumia nyoka kumdanganya mama yetu mkubwa tayari yeye fate yake ilishakuwa sealed..Alielaaniwa ndani ya bustani ni nyoka halisi tulie nae Huku mtaani.

Shetani alichokuwa anakitafuta ni hio nafasi ya utawala ya Adamu ambayo aliikalia mpaka alipokuja YESU KRISTO
 
Hizi ni hadithi tu ,kama hadithi nyingne.
Tatizo ya hii mada, huwafanya watu kupiga picha ni Ndoto gani zinawatokea wakiwa usingizini.

Wengi, ni kukimbizwa na mapolice, kutekwa, marafiki, kupotea, kukosa chakula, kukimbizwa na mbwa.

Mwisho akili inakwambia, kataa ndoto hazina maana 😥😂😂😂😂



Pole ChiefGodlove ataendelea kukuona ndezi na umasikini wako.
 
Tatizo ya hii mada, huwafanya watu kupiga picha ni Ndoto gani zinawatokea wakiwa usingizini.

Wengi, ni kukimbizwa na mapolice, kutekwa, marafiki, kupotea, kukosa chakula, kukimbizwa na mbwa.

Mwisho akili inakwambia, kataa ndoto hazina maana 😥😂😂😂😂



Pole ChiefGodlove ataendelea kukuona ndezi na umasikini wako.
Umaskini ,huyo chief ana husiano gani na uzi wako?

Thibitisha ulicho kisema sio hadithi kama za fisi na sungura?
 
Uchawi, umasikini. ndio mada ya huu uzi lakini uko hapa ulewi chochote upo upo tu, huoni husikii chochote, blind
Uchawi ni hadithi za abunuasi mkuu, umaskini sio jambo la kudumu ukiwa na akili timamu.
 
Back
Top Bottom