Uchawi umedunda kwa Ally Kiba

Uchawi umedunda kwa Ally Kiba

Old Member (Retired)

JF-Expert Member
Joined
Sep 29, 2012
Posts
3,401
Reaction score
1,610
Kilele cha fiesta siku ya jana tarehe 18 octoba 2014 Tanzania na dunia nzima kwa ujumla imeshuhudia msanii Ally Kiba akioyesha kuwa uchawi hauna nafasi kabisa kwenye muziki baada ya kumkalisha Diamond ambaye siku chache zilizopita alijinadi kupitia Clouds fm kuwa yupo tayari kumsaidia Ally Kiba kufanya nae collabo na sasa kibao kimemgeukia yeye ndiye atakayesaidiwa kufanya collabo.

MASHABIKI: Mashabiki walikuwa hawataki kusikia lolote zaidi ya Ally Kiba. Mashabiki wengine walienda mbali zaidi na kusema bora wasimuone T.I wao wanamtaka Ally Kiba tu.

DIAMOND AZOMEWA KAMA MBWA: kila akiimba mashabiki kila kona ya uwanja walikuwa wakimzomea Diamond huku wakitaka Ally Kiba arudi stejini. Mashabiki wasikika wakisema ''kiba kiba kiba kiba kiba'' huku wakimzomea Diamod ''buuuh buuuh buuuh''

Diamond apata wakati mgumu, Davido na Ney wa Mitego watumika kumbeba Diamond lakini mashabiki hawakuacha kumzomea.

DIAMOND ATAFUTA MCHAWI WAKE: Diamond huku akitapa tapa anahisi amechezewa mchezo na Clouds fm au Ally Kiba eti kwa kile anachokiita mafanikio yake, mashabiki wamjibu ''nani akuchukie wewe? kwa mafanikio yapi? kubadilisha wanawake au kutokumaliza nyumba? kama tunachukia mtu mwenye mafanikio wa kwanza angekuwa Mengi na Bakhresa sio mtu ka wewe''
Alizomewa Kikwete mwaka 2012 pamoja na Yoweri Museven chuo kikuu cha dar es salaam, who is Diamond bwana?

Msanii huyo aliyekulia Tandale na kufanya biashara ya kuuza mitumba na voucher, siku kadhaa zilizopita alinukuliwa na vyombo vya habari kuwa Jiji la Mbeya halina hotel inayoendana na hadhi yake, baadhi ya mashabiki kutoka Mbeya pia waahidi kumzomea siku akienda Mbeya kwani kumuacha ni kumuendekeza ipo siku atasema hajaona hotel ya kulala Tanzania nzima/hajaona chakula cha kula Tanzania na hatimae atasema watanzania wote sio level yake.

Ukweli ni kwamba Diamond kwasasa hapendwi nchini Tanzania, si kwamba ni msanii mbaya ila sababu kubwa ni dharau zake na kiburi. Hivyo aashauriwa aache kusingizia watu. ''Waliomzomea ni watu waliotoka kwao na wakalipa pesa zao''

Nimeamini kuwa ''MBELE YA ALLY KIBA UCHAWI HAUNA NAFASI''

Dr. MCHUNGUZI HURU (PhD)
 
Ally k nina zawadi yako.......njoo unywe supu isiyochemshwa uzidi kunoa sauti hyo.
 
eti aliva manguo ya kijeshi pale mikwara hakuna kitu kafanyz nayo nini sasa zaidi ya kuzomewaa buuhuuu
 
Mimi leo kazi yangu kuangalia mtanange wa hizi timu shindani kwenye tasnia ya muziki huu wa playback hapa nchini kwetu Tanganyika na huku nikiingiza vichombezo kidogo kuboresha uzi.
 
Daaaah japo ni mimi ni mpenzi wa daimond na kiba always napenda mafinikio kwa vijana kwani wanatupa changamoto hasa. Japo sijui wanapitia sehemu zipi kuongeza ufanisi wao wa kazi na bahati..ila kitendo cha nasibu abdul kwenda mbeya na kusema hakuona hotel ya hadhi yake tena ndani ya nchi hii tanzania ni kejeri kubwa sana ukiangalia yeye katokea wapi...?? Pia kitendo cha kumtangazia ali kiba kuhusu kumtafutia collabo hivi kwa nini asingekutana naye ana kwa ana wapange mambo yao paka amtangazie kwa public , hapa nasibu hata mimi ningekuzomea kwa kweli.
 
Tatizo watu wa Dar kula miguu ya kuku na utumbo kumewaathiri sana..Mi niko songea hapa juzi kulikuwa na uvumi wa ujio wa Diamond mji mzima ulijaa hekaheka, Huyo Ali kiba wenu hakuna anaemjua ...
 
Tatizo watu wa Dar kula miguu ya kuku na utumbo kumewaathiri sana..Mi niko songea hapa juzi kulikuwa na uvumi wa ujio wa Diamond mji mzima ulijaa hekaheka, Huyo Ali kiba wenu hakuna anaemjua ...

Yaani wewe ndo diamond mwenyewe maana kauli zenu ndo hzo hzo......hao wala miguu ya kuku ndo walitoa kiingilio chao na kuingia hapo leaders.Wanapaswa waheshimiwe
 
Tatizo watu wa Dar kula miguu ya kuku na utumbo kumewaathiri sana..Mi niko songea hapa juzi kulikuwa na uvumi wa ujio wa Diamond mji mzima ulijaa hekaheka, Huyo Ali kiba wenu hakuna anaemjua ...

Wewe unasema huko kwenye viingilio vya 3000,Diamond kazomewa na watu wanaoingia na viingilio vya 15,000 mpaka 25,000.
 
Ali Kiba ndio nani?

Tatizo watu wa Dar kula miguu ya kuku na utumbo kumewaathiri sana..Mi niko songea hapa juzi kulikuwa na uvumi wa ujio wa Diamond mji mzima ulijaa hekaheka, Huyo Ali kiba wenu hakuna anaemjua ...

Mbona haujielewi?Tulia kwanza unajua kuzomewa sio mchezo eeeh?Usicomment mara mbili mbili kwa kumtetea domo kama mnampenda baba masifa wenu mwambie aache dharau na sifa
 
Wewe unasema huko kwenye viingilio vya 3000,Diamond kazomewa na watu wanaoingia na viingilio vya 15,000 mpaka 25,000.

Wala miguu ya kuku na utumbo wa kuku wa Dar ndio hawampendi Diamond kwa sababu amewazidi kipato na umaarufu.. Huku mikoani kwa wajanja wote wanamkubali Diamond
 
I agree with him!!! ------ just WANT a reason to hate on him ugh
 
Mbona haujielewi?Tulia kwanza unajua kuzomewa sio mchezo eeeh?Usicomment mara mbili mbili kwa kumtetea domo kama mnampenda baba masifa wenu mwambie aache dharau na sifa

Mafukara kama wewe hamumpendi Diamond kwa sababu ana.pesa wakati nyie mnaishia kula miguu ya kuku huko manzese
 
Back
Top Bottom