Uchawi wa 500 matumizi ya madawa ama vitabu maalum

Uchawi wa 500 matumizi ya madawa ama vitabu maalum

Empedocles

Senior Member
Joined
Sep 11, 2024
Posts
151
Reaction score
192
Wakuu habari za usiku huu.Pasipokuchosha nijikite katika mada.Tuongeleapo uchawi twalenga matumizi ya madawa ama vitabu maalum(grimoires) ikihusisha manuizo na kudhuru watu wengine kimiujiza.

Tabia hii haukubaliki katika jamii nyingi,zipo jamii zilifanikiwa kukemea tabia hii kwa nguvu na hivyo mambo haya hufanyika kwa kificho.Kwa jamii zilizoshindwa kukemea tabia hii huishi kwa kuwahofia magagula.

Katika Tanzania ipo mikoa inayotuhumiwa kuendekeza tabia hii na watu wake huishi kishirikina zaidi.Athari za kuishi kishirikina na kuishi kwa kuhofia kila ukionacho mbele yako kukihusianisha na uchawi.Mathalani,nimeishi Kibondo miaka 20 nikiwa mikoani natazamwaje na jamii?

Soma Pia: Uchawi ni nini? (Roho, Nafsi, Mwili)

Bundi akilia nyumbani kwako anatafsiriwaje? Chungu kinachouzwa 500 sokoni kwa huku Kibondo ukikuta kimewekwa sehemu kwa kufunikwa kinatafsirikaje?Je,nikisema mshirikina ni mgonjwa wa akili akisumbuliwa na schizophrenia nitakuwa nimekosea?Karibuni kwa mjadala.
 
Mimi kweli akili zinaanza kuniruka, yaani kusema ukweli sijaelewa kabisa hata kidogo
 
Back
Top Bottom