Ucheleweshaji mizigo bandarini alaumiwe tra au tpa?

Ucheleweshaji mizigo bandarini alaumiwe tra au tpa?

Congo

JF-Expert Member
Joined
Mar 13, 2008
Posts
2,081
Reaction score
2,325
Nawasilisha jambo hili ili mtu au taasisi yoyote yenye kuguswa nalo atutafutie majibu au afuatilie nini kinaendelea bandarini na idara ya forodha ya TRA. Kwa muda kama wa mwezi au zaidi kumekuwa na ucheleweshaji mkubwa wa utayarishaji wa kadhia (tansad) pale Customs service centre (zamani Longroon). Tatizo kubwa ni kukatika kwa mawasiliano ya kompyuta kati ya mawakala mwa forodha na TRA. Asycan, MODBRK zinapatikana kwa shida sana. Inaweza kupita nusu siku nzima bila mtandao wa aina hiyo kupatikana. (hata VPN imekatika leo). Hili ni tatizo sugu. Naomba mtu yeyote mwenye kuguswa au mdau yeyote iwe awe serikalini, NGO za kibiashara na kadhalika wafuatilie waangalie kuna tatizo gani. Ukusanyaji wa kodi unaathirika sana. Kule bandarini makotena hayahamishwi kwa wakati kwenda kwenye ICD zinazohusika. Mawakala wakiuliza wanaambia na TPA na TICTS kuwa ucheleweshaji huo unatokana na taratibu za TRA. Kuna kontena hazijahama sasa kutoka bandarini wiki ya pili tangu meli ifike, kisa, tunaambiwa ni taratibu za TRA. Gharama za bandari zikilipwa kupitia CRDB inchukua zaidi ya masaa manne hadi siku nzima malipo hayo kuonekana kwenye mtandao wa TPA. Heri kulipia NMB ai CITI Bank. Je, CRDB ina tatizo gani? Watu wanatoka Congo, Zambia n.k. kuja kufuatilia mizigo yao wanakaa mahotelini wiki 2 tangu meli zifike lakini inashindikana kutoa mizigo hiyo. Mizigo inapata adhabu ya utunzaji wa mizigo bandarini (storage charges) kwa sababu ya taratibu hizo. Ninachoomba wadau wafuatilie na wahusika watujibu kuna tatizo gani linalosababisha ucheleweshaji huu.
 
Back
Top Bottom