DOKEZO Ucheleweshaji wa zoezi la ulipaji fidia kutoka Kwa Jeshi la Uhamiaji Tanzania kwa wanakijiji wa Vuo Kata ya Moa Wilani Mkinga

DOKEZO Ucheleweshaji wa zoezi la ulipaji fidia kutoka Kwa Jeshi la Uhamiaji Tanzania kwa wanakijiji wa Vuo Kata ya Moa Wilani Mkinga

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
A

Anonymous

Guest
Habari ya za majukumu wakuu, mwaka jana Jeshi la uhamiaji Tanzania waliitisha mkutano katika kijiji cha Vuo wilayani Mkinga ili kuelezea wananchi wa kijiji hicho juu ya adhma yao ya kuongeza eneo la chuo chao cha Uhamiaji ambao kila mwananchi ambaye anamiliki eneo au shamba kwenye eneo hilo wanalolihitaji walitakiwa wajitokeze ili kuweza kufanyiwa tathmini na hatimaye kulipwa fidia.

Ilipofika mnano mwezi Septemba mwaka jana Wathamini walifika na kufanya tathmini maeneo yote yanayohitajika na Chuo hicho cha Uhamiaji cha Raphael Kubaga kilichopo Wilayani Mkinga, ila hadi sasa hivi mwezi huu wa August ni takribani miezi kumi na moja (11) lakini hakuna fidia yoyote watu wenye maeneo tajwa wamelipwa.

Zaidi ya hapo waliwahi kuja mara kadhaa kufanya uhakiki wa taarifa lakini cha kushangaza hadi sasa wapo kimya na hakuna taarifa yoyote kutoka kwao juu ya zoezi la ulipaji fidia na ukizingatia tathmini ilikwisha fanyika tangu mwezi wa tisa mwaka jana 2023 ingawaje pia hadi sas hakuna mmiliki yoyote anayejua au kufahamu tahmini yake ya malipo ni kiasi gani.

Wananchi wanachotaka ni hatma ya maeneo yao maana hadi sasa wanashindwa kufanya shughuli zozote za kilimo au biashara kwa kuogopa kuwa muda wowote maeneo yatachukuliwa na chuo hicho.

Kwa hiyo kwa weledi na uaminifu wa kazi yenu naomba mtuulizie hili suala lipoje huko uhamiaji, kama hawayataki maeneo yetu basi wawe wawazi kwetu ili nasi tuweze kuyaendeleza kama ilivyokuwa awali maana wanatuweka njia panda.

Natanguliza shukran za dhati kwenu JamiiForums.
 
Back
Top Bottom