Uchezaji wa kamari chanzo kikubwa cha shinikizo na mashambulizi ya moyo

Uchezaji wa kamari chanzo kikubwa cha shinikizo na mashambulizi ya moyo

Tipstipstor

JF-Expert Member
Joined
Nov 29, 2021
Posts
1,528
Reaction score
3,352
Ahlan wa sahlan

Nikiwa kama Ex-mkamaria kuanzia sasa, ninelifanyia uchunguzi suala hili na kugundua kuwa Kamari ni jambo linaloweza kumpelekea mchezaji kupata shambulizi la moyo la ghafla.

Kwa mchezaji kamari yoyote naomba ajiangalie hali yake ya mapigo ya moyo pindi anapobeti mpaka pale majibu yanapotoka,Niwazi kuwa atagundua kuwa kuna ongezeko kubwa la mapigo ya moyo ,jambo ambalo ni hatari sana na linaweza hata kumpelekea mtu akapoteza maisha.

Wito wangu ni kuwa kama unaipenda afya yako au hutaki kuzeeka kabla ya wakati wako kutokana na stress za kubeti basi acha kubeti mara moja.
 
Fuatilia takwimu uone idadi ya wakamaria wanaoamua kujiua baada ya kupoteza pesa kwenye makasino
Ndo maana unaambiwa uweke unachoweza kukipoteza, tatizo Ni pale unapoitegemea Kama chanzo Cha kukuimgizia kipato hapo ndipo tatizo linapokua kubwa
 
Ndio maana wazungu wanasema, "bet with the money that you can afford to loose". Sio wajinga wale wana maana yao kubwa tu. Na wenyewe huwa wana msemo kuwa betting is just a fun and not for living.

Sasa nyie waswahili mnalundika matimu 10-50 na unaweka 10k hadi 50k, hapo ni lazima yakukute mkuu.
 
Aiseeeh, kamari imenitia hasara sana sitaki hata kuiona mwaka 2020 mwanzo corona iliposhika kasi job tulisimama kidogo, muda mwingi sana nilikuwa nyumbani na vichenchi nilikuwa navyo basi nikaanza kucheza kamari weee nikuwa napigwa mpaka nilikuwa natetemeka, toka niliporudi job siitaki kabisa kusikia kitu kinaitwa kamari.
 
Hatari sana mzee baba
 
Back
Top Bottom