Uchimbaji wa dhahabu unataka umakini na adabu ya fedha

ommytk

JF-Expert Member
Joined
Jul 30, 2015
Posts
520
Reaction score
1,143
Uchimbaji wa dhahabu kuanzia kwa mchimbaji mdogo mpaka mkubwa. Watu wanaingia woga sana kwenye hii biashara ambayo inataka umakini na adabu sana kwenye fedha.

Tuanze na uchimbaji wenyewe Kwanza anza kidogo kidogo kwa kuwa makini na ujitoe rasmi kuingia kazini sio uwe unawatuma watu hii kazi inataka uwe kazini nawewe sio kuwatuma Watu. Kwanza ujue eneo zuri ambalo dhahabu inatoka mfano chunya. Geita na maeneo mengine.

Utaweza kuingia uchama hii uchama ni kujiunga kama kikundi na wenzako ambapo mtaji wako Itajubá nguvu zako na pesa kidogo ambayo mnakuwa mnachanga kuendesha duara lenu mnapoanza uchimbaji na mkaanza kupata dhahabu mtaanzakuuza kidogokidogo then mnaanza kuweka pesa kuelekea kwenye kununua machine ya kusaga mawe crusher ndogo ambayo inagharama kama 9m na 10m Sasa hapo ndio unaanza safari ya kubadili maisha yako.

Hapa Sasa mtaanza kusaga mawe na kupata dhahabu ambayo itaendesha maisha na gharama zote za site na wakati huo Kwanza kutengeneza lundo ambalo mtaenda baadae kupeleka kuchenjua dhahabu hapo sasa Ndio mnapoenda kubadili maisha kwa jumla dhahabu inataka adabu na umakini
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…