KERO Uchimbaji wa mchanga Mtaa wa Mbopo Kata ya Mabwepande mto Nyakasangwe

KERO Uchimbaji wa mchanga Mtaa wa Mbopo Kata ya Mabwepande mto Nyakasangwe

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
A

Anonymous

Guest
Kwa muda mrefu sasa mto Nyakasangwe unaotenganisha wilaya ya Ubungo kata ya Msumi na Kinondoni kata ya Mabwepande kumekuwq na uchimbaji holela wa mchanga.

Mara kadhaa wanachi kwa kushirikiana na serikali za mitaa ya Mbopo na Msumi wamekuwa wakitoa taarifa kwenye vituo vya polisi vilivyo jirani vya Madale na Nguzo bila mafanikio, wabunge wetu waheshimiwa Mtemvu wa jimbo la Kibamba na mwenzake Gwajima wa Kawe wamekuwa wakipuuzia pamoja na wapiga kura wao kulalamika.

Mto huo ambao zamani ulikuwa ni kijito umachoweza kuruka kwa miguu sasa umezidi kutanuka na kuharibu mazingira na nyumba zilizo jirani.

Sisi wakazi wa Msumi na Mbopo tunaomba mamlaka husika likiwemo baraza la Mazingira (NEMC) na mheshimiwa Ashatu Kijaji mwenye dhamana ya mazingira ziingilie kati.
 
Hii Kero ni kubwa mno


Huo mto nyakasangwe kwa huu upande wa Boko Magengen kuelekea Burumawe uchimbaji wa mchanga umeathiri sana makazi ya watu..

Kama unavyosema mleta mada miaka ya nyuma mto ulikuwa mdogo mno lakin miaka hii ya karibu baada ya uchimbaji holela kuchukua nafasi madhara kwa wakazi ni makubwa mno

Mamlaka zipo kimya ,Vyombo vya usalama wanadaka mlungula wanapita kimya


Hii sio sawa
 
Back
Top Bottom