Stephano Mgendanyi
JF-Expert Member
- May 16, 2020
- 2,833
- 1,301
UCHIMBAJI WA VISIMA VIREFU VYA MAJI UMEANZA NDANI YA JIMBO LA MUSOMA VIJIJINI
Jumatatu, 26.8.2024, Mkuu wa Wilaya ya Musoma (DC), Dkt Khalfany Haule amepokea na kushuhudia gari lenye mtambo wa uchimbaji wa visima virefu vya maji ukianza kazi kwenye Kata ya Bugwema ya Jimboni mwetu.
Jimbo letu litachimbiwa visima vitano (5) - taarifa kutoka kwa Meneja wa RUWASA wa Wilaya ya Musoma, Injinia Edward Sironga
Baadae, maji kutoka kwenye visima virefu vinavyochimbwa yatasambazwa kwa mabomba ndani ya vijiji venye visima hivyo.
Mbali ya upatikanaji wa maji kutoka visima virefu, vijiji vyetu vyote 68 vinayo miradi ya kusambaziwa maji ya bomba kutoka Ziwa Victoria. Miradi hii iko kwenye hatua mbalimbali za utekelezaji wake.
CLIP/VIDEO iliyoambatanishwa hapa:
Tafadhali sikiliza shukrani nyingi za wananchi kwa Serikali yetu kutoka kwenye CLIP/VIDEO hii - muongeaji wa hitimisho kwenye CLIP/VIDEO hii ni DC Mhe Dkt Khalfany Haule.
Soma Pia: Vijiji vya Jimbo la Musoma Vijijini Vyaendelea Kusambaziwa Maji ya Bomba Kutoka Ziwa Victoria
Ofisi ya Mbunge
Jimbo la Musoma Vijijini
www.musomavijijini.or.tz
P. O. Box 6
Musoma
Tarehe:
26.8.2024