unaleta taarifa ambazo hujazifanyia utafiti.Labda utafiti wako unaufanyia hapa JF.haya maelezo yako yanaangukia neno lako kwamba ni ngano.Unachojaribu kuandika kipeleke kwa Mohamed Said akusahihishe kama anavyofanya hapa
Pole sana mkuu, soma mantiki ya nilichokieleza, Muulize Mohamed Said anaelewa maana ya tunachojadili hapa!
Mkuu Mohamed Said, nimerejea baada yakuwa kimya kidogo, hii ni kwasababu ya majukumu yakusaka mkate.
Nitaelezea kwa ufupi jinsi kanisa la Tanganyika lilivyoshiriki harakati za ukombozi wa Tanganyika na madhila liliyokumbana nayo.
Ifahamike kuwa vyama vya harakati za ukombozi Tanganyika vilikuwa vingi sana, na vipo vilivyokuwa vikipingana vyenyewe kwa vyenyewe.
Mwaka 1927 1929 kanisa Katoliki nchini chini Joseph Gabriel Zelger, lilibainika kuingiza siasa katika utendaji kazi zake, kitendo hiki kiliwakwaza wakuu wa mamlaka ya kikoloni na kupelekea majasusi wakikoloni wapendekeze aachishwe uongozi wa kanisa nchini. Ni kweli tarehe 12 februari 1929 Zelger alistaafu wadhifawake kwa lazima.
Kisa hiki kinasema, Kanisa lilianzisha mafundisho yenye kuchochea fikra za kimaasi, nalilifanikiwa kuandaa wakufunzi maalumu kwenda katika majimbo yote ya kihuduma Tanganyika, hilo lilipelekea kuleta mtafaruku na dola ya mkoloni wa kiingereza ambapo ilimgharimu kiongozi huyu wa kiroho kuachia madaraka yake.
Alipoingia askofu Edger Aristide Maranta mwaka 1930, ikiwa kama vile mwendelezo wa mtangulizi wake, Askofu Maranda alianzisha harakati za kuwashawishi viongozi wengine wa majimbo kuendeleza kutoa mafundisho yenye kumfanya mtanganyika ajitambue na adai uhuru wake,
Mfano: 23 mei 1938 wakati makanisa saba ya Kilutheri yakiwa kwenye hatua za mwanzo za mchakato wa kuungana, Askofu maranda aliomba kuhudhuria kikao cha tarehe 8 mwezi wa sita kilichofanyika Mjini Arusha, Askofu Maranda aliudokeza mpango ule wa siri wa katoliki katika kikao hicho, japokuwa kulikuwa na hofu ya kutoaminiana, lakini uthabiti wa malengo hayo ulijipembua baadae na kuwa wamafaa.
Juhudi za kanisa kupigania ukombozi ziliendelea kushika kasi huku zikiendeshwa kwa siri sana kwamfumo wa neno la kiroho, na ilipofikia miaka ya 1950+ kanisa sasa lilikuwa tayari linanguvu ya ushawishi kufuatia mafanikio ya harakati za kanisa katika nyanja za ukombozi barani afrika.
Mtihani mkubwa kwa kanisa ilikuwa ni namna gani linaweza kuingia rasmi kudai uhuru wa Tanganyika. Katika kipindi hiki tangu harakati za kanisa zianze, Askofu Maranta pamoja na mapadre wa baadhi ya mikoa, walikuwa tayari ameshafanya juhudi kadhaa za kukutana na Mashehe waliokuwa na ushawishi mkubwa, mfano 05/02/1948, Askofu Maranda alikutana Shehe Issa bin Amir kiongozi wa kiroho katika msikiti wa Ilala - mchikichini. Mazungumzo yao yalihusu harakati za ukombozi, Shehe Issa alimshauri Askofu kuwa ikiwa makanisa na misikiti yanapigwa marufuku na mkoloni kujihusisha na siasa za ukombozi basi watafute baadhi ya vyama vya harakati za ukombozi na waviunge mkono, wazo hilo lilimvutia Askofu lakini akajenga hofu kama je ndani ya vyama hivyo watapata vijana wasomi?.
Siku chache baada ya makutano yake na Shehe Issa, Askofu Maranta aliletewa mapendekezo kutoka kwa Attilio Beltramino kassi wa katoliki aliyehudumu kule Iringa, mapendekezo ya kasisi huyu yalikuwa ni, Umishonari makao makuu uruhusu udurufu wa biblia zisomeke kwa makabila ya wahusika wa eneo, ndani ya biblia hizo yaongezwe mafundisho ya haki ya kujitambua na kujitawala wenyewe. Pendekezo hili lilimvutia sana Maranta hivyo akalipa baraka zake, kwa hakika lilifanikiwa na ndio lilizaa hisia kali za mwamko wa kudai uhuru, mfano biblia ya lugha ya kihehe ilikuwa inaeleza wazi athari za kutawaliwa.
Harakati za Ukombozi za Mwalimu Nyerere zililivutia kanisa na likaamua kumuunga mkono, mfano mwaka 1953 wakati TAA kikiwa chama chenye nguvu, Askofu Maranta alimwalika ofisini kwake Mwalimu Nyerere, walizungumza mengi lakini kubwa nikuwa alimsifu kwa juhudi za kujipambanua bila kuwaogopa wakoloni na akamweleza jinsi kanisa linavyounga mkono juhudi za ukombozi wa Tanganyika, kisha akamshauri kuwa ajaribu kuvishawishi baadhi ya vyama vya harakati za ukombozi viungane ili kuvipa nguvu ya kudai uhuru na kanisa litasaidia.
Wazo la Askofu Maranta lilimkaa Mzee Nyerere na mwaka 1954, alianza juhudi za kuwaunganisha vijana wenzake wa kariakoo ambao walikuwa ndani ya TAA na wenye nguvu ya ushawishi lakini wakikabiliwa na matatizo makubwa mawili katika lengo lao.
- Elimu,
- Woga
Ikumbukwe kuwa mwaka 1953 baada ya harakati za ukombozi kupamba moto na kamata kamata ya wanaukombozi, Askofu Edger Aristide Maranta alihamishiwa Zanzibar na nafasi yake ikachukuliwa na Vicar Apostolic, lakini bado aliendelea kuwa mshauri imara wa Mwalimu Nyerere. Jambo la kushangaza kama si kufurahisha, mwaka huohuo mwezi wa 8, Edger Aristide Maranta alirudishwa tena Dar es Saalam, na sasa mbinyo dhidi ya ukoloni ikahika mkondo wake.
Mnamo tarehe 7/71954, Vijana (wazee wa kariakoo) wakiongozwa na Julius Kambarage Nyerere, walikubaliana wazo la kuhuisha chama kutoka TAA kwenda TANU, chini ya uratibu wa karibu wa kanisa Katoliki (Askofu Maranda) na Waislamu (Shehe Issa bin Amir)
Mpaka hapo ndugu yangu Mohamed Said angalau umepata picha kwa KIFUPI tu ya harakati za uhuru chini ya kanisa.
Nikipata wasaa nitakuletea picha za Mwalimu Nyerere na Edger Aristide Maranta
Sasa nini kilifuata baada ya uhuru? Kwanini Kasisi huyu wa kikatoliki Edger Aristide Maranta hatajwi popote katika historia ya nchi? Kwanini kanisa katoliki halilalamiki kutokuwepo kwenye kitabu cha kivuko?Yote hayo nitakushushia taratibu kadiri mnakasha huu unavyoenda.
huna unachojadili,sema unajifunza na kusahihisha kile ulichomezeshwa cha batili
Hakika nafurahiiswa sana na weledi wako na majibu yako muruwa na wengi tunanufaika na darsa lako. Kama nilivyowahi bainisha huko awali kuwa Y Nyerere hajafanya utafiti wowote katika maandiko yake ndio maana yanakuwa na mashaka mashaka na kutofahamu vizuri hata wale anaowazungumzia majina yao na hata familia zao. nashukuru kwa msaada mkubwa unaompa kwa nia ya kumsaidia na hiyo kama atakuwa ametulia itambidi nae afanye utafiti wa kina na kuleta hoja mbadala kama atazipata. Shukran kwa darsa lako na Allah akuzidishie zaidi na zaidiItabidi nami niulize walionipita umri. Sina kumbukumbu ya Sheikh Issa bin Amir sheikh ambaye alikuwa na ushawishi kwa Waislam kiasi atafutwe na Father Maranta kuzungumzia mambo makubwa ya nchi. Lakini jambo ambalo nina hakika ni kuwa sheikh huyo hawezi kuwa baba yake Sheikh Hassan bin Amir hata kwa mbali. Nakushauri ujaribu "Sheikh Idrissa bin Saad" maana katika wakati huo usemao yeye ndiye alikuwa sheikh maarufu kupita wote Dar es Salaam. Sheikh Idrissa bin Saad alikuwa akikaa Mtaa wa Narung'ombe na Bonde nyumba yake ikitazamana na msikiti wake. Zipo taarifa kuwa kulikuwa na padri akimtembelea Sheikh Idrissa pale nyumbani kwake na wakifanya mazungumzo ambayo hayakuwa ya faragha. Hebu pita na huko. Wajukuu wa Sheikh Idrissa bin Saad wapo na wanaishi nyumba hiyo hiyo ya babu yao. Ahsante kwa darsa.
Mzee Mohamed Said,Yapo maneno yakizungumzwa na wazee wa Dar es Salaam kuhusu kushiriki kwa Nyerere katika maziko ya wanaharakati Waislam.
Wanasema kuwa baada ya maneno yaliyosemwa baada ya maziko ya Abdu Sykes Nyerere aliona itakuwa bora ajitenge nao kwa mbali sana.
Unafahamu ikiwa Nyerere atahudhuria maziko ya mtu yoyote watu watataka kujua ule uhusiano kati yao.
Mathalan alipohudhuria maziko ya Abdu Sykes na akatembea kwa miguu nyuma ya jeneza la Abdu kutoka Mtaa wa Lindi hadi Msikiti wa Kitumbini kisha kutoka hapo hadi Makaburi ya Kisutu wasiojua uhusiano wa Abdu na Nyerere hata ndani ya TANU na serikali wakati ule walipigwa na mshangao mkubwa.
Jambo la kustaajabisha magazeti ya TANU chini ya Benjamin Mkaoa hayakupa uzito msiba ule ila walichoandika ni kuwa Nyerere kahudhuria mazishi ya Abdu Sykes.
Hawakueleza chochote katika mchango wake wa kumpokes Nyerere Dar es Salaam wala wa kufadhili TAA hadi TANU wala mchango wake katika kuasisi chama.
Rafiki zake Abdu kama Ahmed Rashad Ali na hata baba yangu wakawa wanasema inaelekea Nyerere hapendi kunasibishwa na historia yake mwenyewe.
Iweje Abdu asiandikiwe taazia sawa na makamu na heshima yake?
Hata binti yake Abdu alikasirishwa na jinsi historia ya baba yake ilivyopuuzwa na hawa wote walielekeza shutuma zao kwa Nyerere.
Sasa hata alipokufa Sheikh Hassan bin Amir Nyerere hakuhudhuria maziko yake, Sheikh Mohamed Ramia, Idd Tulio, Jumbe Tambaza, Dossa Aziz nk.
Swali likaja kuwa ule udugu watu hawa waliomfanyia Nyerere umekwenda wapi?
Mbona picha iliyojitokeza ni kama watu hawa hawakupata hata kujuana?
Ndiyo tena yakafuatia na haya mengine ya hao wote kufutwa katika historia ya kupigania uhuru wa Tanganyika.
Leo gari alotoa Dossa kumpa Nyerere kwa ajili ya shughuli za TANU New Street hakuna ajuae inaulizwa gari ya Chief Thomas
Marealle ambayo iko Butiama.
kama utamsoma Ahali yangu Mohammed Said kwa NIA ya kumuelewa basi utafahamu mengi sana kutoka kwake kwani ameshehemi weledi mkubwa katika historia ya Tanganyika hususan Dar es Salaam ambako kilitua kitovu cha harakati zote za uhuru wa Tanganyika. Lakin kama utamsoma kwa NIA ya kupinga hapo utapata taabu kubwa sana kwani yeye ni mtafiti naa kisa hicho cha miaka ya 50's sio tu amesikia kutoka kwa wazee wake laki naye aliona kwa macho yake. Hivyo utafiti wake ni wa kuona na kusimuliwa na wazee wake. hakuna agenda yoyote hapo zaidi ya UKWELI mtupu uliofichwa.Mzee Mohamed Said, Unachomkosea Mwalimu katika maandiko yako mengi ni kujaribu kuingia hadi akilini mwake na kueleza hisia zake kama vile wewe ni yeye. Hii sio sahihi hata kidogo. Haukuwahi kuwa karibu na Mwalimu. Wazee wako hawa ndio walookuwa karibu naye. Wao ndio waliokusimulia mengi kuhusu Mwalimu. Wewe kwa agenda yako hii ya UISLAM ukachagua ya kuandika na ukayaita historia ya kupigania uhuru wa Tanganyika.
kama utamsoma ahali yangu mohammed said kwa nia ya kumuelewa basi utafahamu mengi sana kutoka kwake kwani ameshehemi weledi mkubwa katika historia ya tanganyika hususan dar es salaam ambako kilitua kitovu cha harakati zote za uhuru wa tanganyika. Lakin kama utamsoma kwa nia ya kupinga hapo utapata taabu kubwa sana kwani yeye ni mtafiti naa kisa hicho cha miaka ya 50's sio tu amesikia kutoka kwa wazee wake laki naye aliona kwa macho yake. Hivyo utafiti wake ni wa kuona na kusimuliwa na wazee wake. Hakuna agenda yoyote hapo zaidi ya ukweli mtupu uliofichwa.
Hakika nafurahiiswa sana na weledi wako na majibu yako muruwa na wengi tunanufaika na darsa lako. Kama nilivyowahi bainisha huko awali kuwa Y Nyerere hajafanya utafiti wowote katika maandiko yake ndio maana yanakuwa na mashaka mashaka na kutofahamu vizuri hata wale anaowazungumzia majina yao na hata familia zao. nashukuru kwa msaada mkubwa unaompa kwa nia ya kumsaidia na hiyo kama atakuwa ametulia itambidi nae afanye utafiti wa kina na kuleta hoja mbadala kama atazipata. Shukran kwa darsa lako na Allah akuzidishie zaidi na zaidi
Wewe ni mpuuzi kama hujui kitu nyamaza,
Yericko kawaumbueni kwa uongo wenu!
Watu tunaongopeana sana humu wakati mwingine. Uliza tu swali hili dogo: Mwingereza alipigana na Mtanganyika yupi katika huko wanakoita "kupigania uhuru" wa Tanganyika? Tanganyika haikuwa koloni la Mwingereza. Mwalimu na wenzake walifanya kazi rahisi na ndogo sana ya kuikumbusha UN kwamba sasa tuko tayari kujitawala WATANGANYIKA wenyewe. Mwingereza wala hakuleta ubishi wowote.Mkuu naomba utupe 'darsa' kwa faida ya wengi,kunaweza ibuka mkanasha mwingine hapa ninavyoona
Asante sana mheshimiwa, kwakweli nimesoma hii makala nzuri na nimefarijika sana!
Yericko wewe ni mwanahistoria wa kweli uliyekuja kuzima kelele za wadini kama Mohamed Said.
Asante sana kkwa elimu hii isiyopatikana chuoni au popote pale isipokuwa JF
karibu sana mkuu, tunahuisha kwa kifupikipifupi historia ya uhuru wetu!
Wewe ni mpuuzi kama hujui kitu nyamaza, Yericko kawaumbueni kwa uongo wenu!
Ni kupembuka gani huko unakodai?. Kwani kwa wasomi tunajibu TAFITI kwa TAFITI na wala sio TAFITI kwa kejeli au maneno ya mitaani. sasa nilichobainisha ni kuwa Unachoandika wewe kina mashaka mashaka na hakina utafiti wa aina yoyote ndio maana unakosema majina na hata status za watu mfano shaikh Idrisa bin Saad n.k Mimi nakushauri kama msomi fanya tafiti kidogo na wewe na kuja na paper ambayo utaweza kuitetea kwetu ili upingane na Mohamed said. Huo ni ushauri wangu kwako.Ndugu yangu, bado hujapembuka katika mizania ya historia, Tumia mda mwingi kujisomea hayo niliyokupa yatakupembua na kukupevusha! Nilichokupa ni ushiriki wa kanisa katika harakati za ukombozi Tanganyika ambayo Mohamed Said aliyaghiribu katika kitabu chake,
mbona povu linakutoka,vumilia utapona japo dawa chungu.Waite na wengine mje msome kwa mwanahistoria Mohamed Said,watu wanastafidi sana hapa jamvini.Mwenzio Yeriko kaja kulitetea kanisa nalo eti lilipigania uhuru wa tanganyika.Teh teh teh kazi kwelikweli,kapewa jina la sheikh hata hajulikani kajaribu kufananiza lakini kaumbuliwa
In his last act in before his death in London, Prof. Malima took wudhu (ablutions) as if he was getting ready for salat (prayers).
Around 01:25 hrs in the morning he laid down in bed. At around 01:30, precisely five minutes, he rose suddenly as if from a deep
dream and said softly and pleasantly, "Alhamdulillah.' (All praise and gratitude is for Allah). He then fell back again in a sleeping
posture. He was gone. Polycarp Pengo head of the Catholic Church Dar es Salaam Region, issued a statement calling Prof. Malima
a " highly dangerous individual who had to be contained" for his decision to stand as presidential candidate outside CCM.