Uchochezi wa Mohamed Said na dhihaka kwa Wapigania Uhuru wa Tanganyika na Zanzibar

Hujielewi wewe...!

Hivi umejaribu kupitia pitia kidog michango ya wenzako na ndugu Moh said kwa ujumla kabla hujabandika mashudu yako hapa??

Umekimbia sana mwishowe umepitilza kwenu..

Pole sana,umejaribu lakini..

Bwana mdogo tulia kwanza hujasoma kilichoandikwa , pili unafikiri mimi ni mgeni na huu mjadala. Wewe kazi yako hapa ni upambe tu huna hoja.
 
Bwana mdogo tulia kwanza hujasoma kilichoandikwa , pili unafikiri mimi ni mgeni na huu mjadala. Wewe kazi yako hapa ni upambe tu huna hoja.

Kwaiyo kucopy na kupaste hayo mashudu ulikofanya ni hoja??

Sisi wale wanaopenda penda sana kucopy na kupaste tunawaita VILAZA..
 
Nyambala ulikuwa wapi aisee na darsa zuri namna hii?
ungekuwepo tangu mwanzo huenda huu mnakasha usingefika huku.
 
Last edited by a moderator:

Mkuu asante sa
 
Kwaiyo kucopy na kupaste hayo mashudu ulikofanya ni hoja??

Sisi wale wanaopenda penda sana kucopy na kupaste tunawaita VILAZA..
jisomee kwanza alichoweka Nyambala ndo utoe comments sio viloja.
nyie ndo mnamuangusha MS.
 
Last edited by a moderator:
Kwaiyo kucopy na kupaste hayo mashudu ulikofanya ni hoja??

Sisi wale wanaopenda penda sana kucopy na kupaste tunawaita VILAZA..

Haya wewe endelea kupiga makofi, unaelewa maana ya nukuu lakini? Unaelewa maana ya historia, unaelewa maana ya facts?
 
Haya wewe endelea kupiga makofi, unaelewa maana ya nukuu lakini? Unaelewa maana ya historia, unaelewa maana ya facts?

We are real not interested with your copy & paste KILAZA..

Tunachokizungumza hapa kimefanyiwa utafiti kabla ya kuandikiwa,hiki nyinyi mnachokiita Ngano,kwaiyo hayo unayokuja nayo wewe hata mtoto wa form one anayaelewa labda kama wewe ulikua hujui,

Kwa ufupi umeonesha Ujinga wako kwa kias kikubwa sana..
 
Umerudi na mulkari kubwa sana mkuu.
 
Kumbe MFIA DINI NAYE YUPO??

BASI NA TUTAZID KUENDELEA KUMPUUZA..

:banplease:

eti hizi ndio hoja!!??? Naona mzee wa gesi umerudi na Id yako kabisa baada yakufunguliwa, mtaendelea kumpuuza wewe na nani? Ngojea nikuulize swali kati ya wewe na Mwanakijiji, nani kampuuza mwenzake? Sio kwamba wewe ndio umepuuzwa?maana tokea umuandame Mwanakijiji sijaona akikujibu hata kidogo, sasa nani hapo kapuuzwa!? Kama sio wewe ndio umepuuzwa...
 
Jazakallahu kheir..
 
Nyambala,

Watu kama wewe ni lulu katika JF.
Ila mimi kwa utu uzima wangu nakupa ushauri mdogo na mfupi sana.

Unapokuja na vitu kama hivi (nyaraka za Hansard) usivichafue kwa lugha mbaya.
Sasa nami nakuwekea hali ya mambo yalikuwaje pale TAA Office, New Street, Dar es Salaam:

TAA HQ, Dar es Salaam 1950

''Baada ya kuunda kamati hii (TAA Political Subcommittee), Abdulwahid alianza kuyaandikia matawi ya TAA ili kuyahuisha.

Jambo kubwa lililomkabili Abdulwahid na ile kamati ya siasa ilikuwani hadhi ya Tanganyika kama nchi ya udhamini chini ya Umoja wa Mataifa.

Abdulwahid alimuingiza katika kamati ya siasa Earle Seaton, mwanasheria kutoka Bermuda aliyekuwa akikaa Moshi ili aishauri kamati kuhusu mambo ya sheria ya katiba.

Aidha alitakiwa kuwashauri jinsi ya kuliendea shauri la kutaka Uingereza itoe uhuru ili Tanganyika ijitawale yenyewe kwa kuwa nchi hiyo haikuwa koloni, bali nchi chini ya udhanini wa Umoja wa Mataifa.

Mwaka wa 1948 Baraza la Udhamini la Umoja wa Mataifa tayari lilikuwa limetuma ujumbe wake wa kwanza kuzuru Tanganyika.

Lakini hakuna jambololote la manufaa lilipatikana kutoka kwa ujumbe huo.''

Nyambala mimi nimeona nikuwekee kwanza haya machache tu kukupa hali ilikuwaje katika fikra ya uongozi
wa TAA pale New Street, 1950.

Nitakuongeza pia kuwa Baraza la Udhamini lilipokuja Tanganyika mwaka 1950 aliyetoa maelezo ya TAA alikuwa
Said Chamwenyewe.

Ukipenda nikuwekee vitu zaidi tafadhali usisite kusema.

Mzee wetu Mohamed anaye copy na ku paste kitabu chake mwenyewe humu tumwiteje?

Soma uone walioturudishia uhuru walisema nini kabla. Angalia pia Mwalimu katajwa mara ngapi na kwa sifa zipi.
 
Mwaka wa 1948 Baraza la Udhamini la Umoja wa Mataifa tayari lilikuwa limetuma ujumbe wake wa kwanza kuzuru Tanganyika.
Lakini hakuna jambololote la manufaa lilipatikana kutoka kwa ujumbe huo.''

Kwa nini?
 
Alikuwa akiitwa Mohamed Saidi Chamwenyewe.
 
Sina sijui kwa nini hapakupatikana jambo la manufaa.
 
Alikuwa akiitwa Mohamed Saidi Chamwenyewe.

Nyambala,
Huna jingine ungependa niongeze?

Unajua Said Chamwenyewe ndiye aliyetumwa na Abdu Sykes kwenda
Rufiji kuiletea TANU wanachama wake wa mwanzo Julai 1954?

Chamwenyewe akienda Rufiji kwa baiskeli njiani akisimama kila kijiji
kutangaza TANU na kuuza kadi.

Baada ya Kura Tatu 1958 akatoka TANU kujiunga na Congress ya Mtemvu.
Baadae alirudi TANU.
 
Mzee wetu Mohamed anaye copy na ku paste kitabu chake mwenyewe humu tumwiteje?

Soma uone walioturudishia uhuru walisema nini kabla. Angalia pia Mwalimu katajwa mara ngapi na kwa sifa zipi.

WC,

Mimi si copy kwa maana ya neno lenyewe.

Mimi ni kama nakufungulia kurasa za kitabu
changu usome niliyoandika.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…