Uchochezi wa Mohamed Said na dhihaka kwa Wapigania Uhuru wa Tanganyika na Zanzibar


Uko wapi?
 

Basi ndugu yangu tuvunje mfupa wa fitna. Iweke hapa hiyo habari yaishe.
 
Darsa, si "darasa".

Darasa,Darsa yote sawa,sema Darsa ni neno la kijiwezi kama vile kusema napiga msala kumaanisha unasali,ni sala wala sio swala
Hoja hapa sio nani anajuwa kiswahili,sory bro
 
إِنَّ الَّذِينَ كَفَرُواْ سَوَاءٌ عَلَيْهِمْ أَأَنذَرْتَهُمْ أَمْ لَمْ تُنذِرْهُمْ لاَ يُؤْمِنُونَ
Hakika wale walio kufuru ni sawa kwao ukiwaonya au usiwaonye, hawaamini (Qur2:06)
خَتَمَ اللَّهُ عَلَى قُلُوبِهِمْ وَعَلَى سَمْعِهِمْ وَعَلَى أَبْصَارِهِمْ غِشَاوَةٌ وَلَهُمْ عَذَابٌ عَظِيمٌ

Mwenyezi Mungu amepiga muhuri juu ya nyoyo zao na juu ya masikio yao, na juu ya macho yao pana kifuniko. Basi watapata adhabu kubwa. (Qur2:07)

JEURI YA FIRAUNI ILIVYOSHINDWA

Firauni alitakabari na kujitangazia uungu.Kwa hofu ya kutokea mtu mwengine kuupinga uungu wake akawa anawachinja watoto wote wa kiume waliozaliwa kwenye nchi ya Misri.Kwa hekima za Mwenyezi Mungu hakuweza kumchinja Mussa (A.S) na bila kujua akamlea ndani ya nyumba yake.
Musa (A.S) alikuwa ni Mtume wa Mwenyezi Mungu aliyepewa miujiza.Miujiza yake mikubwa ilikuwa kwenye fimbo yake.Akapewa amri aende yeye na nduguye Haruna kwa Firauni wakampe khabari za kuwepo Mwenyezi Mungu aliye mkuu na muumba wa kila kitu.Hii ikawa mwanzo wa ugomvi wake na Musa (a.s).Miujiza ya Musa (a.s) akaita ni uchawi tu.Ikiwa ni uchawi yeye aliamini ana wachawi wakubwa zaidi na wengi.
Upatu ukapigwa kote mjini watu waje uwanjani kushuhudia uchawi wa Musa (a.s) utakavyopondwa pondwa na kumaliza madai yake ya utume.Wachawi wa Firauni wakakusanywa na kualikana.Siku ilipofika Firauni akakaa kwenye kiti chake cha enzi kushuhudia pambano baina ya Musa a.s dhidi ya wachawi wa Firauni.
Uwanja ulikuwa umejaa kweli hata pa kutia mguu hakuna.Wachawi wa Firauni wakaanza pambano kwa kutupa fimbo zao zilizogeuka nyoka wa kutisha.Zamu ya Musa a.s ilipofika akatupa fimbo yake ikageuka joka kubwa likameza wale nyoka wote wa wachawi wa Firauni.
Wachawi hapo hapo wakageuka kuwa waumini wa Musa a.s..Firauni akafedheheka kwa kushindwa kuthibitisha kuwa Musa a,s ni mchawi.
Akahamaki na kuwaambiwa wachawi wake kwanini wamemuamini Mus a.s kabla ya idhini yake.Wachawi wakajibu IMANI KWA MWENYEZI MUNGU HAIHITAJI IDHINI KUTOKA KWA YEYOTE.
ukweli waliouona kwa macho yao unatosha.
Mwenye kujua kiarabu angalia VIDEO HAPA
 

Kama wewe unavyouchukia Uislam na Waislam.
 

Asanta Ami ama kweli Farao alitakabari na kuvuka mpaka ati yeye ndie Mungu mkuu! Kuna bwana moja alikuwa mtawala anaeogopwa na kutukuzwa ile mbaya mpaka akafikia kusema anauwezo wa kuishi hata miaka 100! muda mfupi baada ya kutamka hayo ghafla kaugua na roho kumtoka! Mungu aiweke roho yake mahala panapostahili! AAmin!
 
Ritz
Sivalon na Van Bergen wakiandika habari za pwani ndio unaamini?
Mushi akiandika, inakuwa si kweli, sasa kwanini tuamini ngano za Mmanyema Moh Said kuhusu Tabora, Bukoba, Musoma, Mbeya??????
Tafakari! Jichukulie hatua!

Nanren,

Mushi ameishakupa habari za kina Affande Plantan, Dr James Kwegyir Aggery, Rawson Watts, Idd Faiz, Idd Tosiri, Mshume Kiyate, I. C. Chopra, Dossa Aziz, Ahmed Rashad Ali, Mtoro Rehani, Abdul, Kandoro, Sheikh Haidar Mwinyimvua, Zibe Kidasi, Ali Ponda, Bilal Waikela, Jan P Van Bergen, Sivalon J, Smith P. Frg
 
Last edited by a moderator:

Lawama zinakuja sababu kitabu kimeandikwa kivukoni na kutambulika kama historia rasmi ya wapigania uhuru! Kambona hakuandika kitabu bali aliwataja hao wazee ili kushawishi wakazi wa Dar wakiunge mkono chama chake tena aliwataja kwa majina lakini Nyerere alipowaaga Wazee wa Dar mwaka 1985 ktk hotuba yake hakuwataja wapigania uhuru kwa majina bali aliwaita Waislamu watupu! Mohamed Saidi kaandika kitabu ili kukanusha kitabu kilicho andikwa kivukoni! hoja sio kuwataja bali kuandika kitabu! nacho kimeandikwa na MS lakini hamkiamini! lakini Kambona na Nyerere wamewataja mnaamini kizungumkuti hicho!
 

Tatizo mnapenda kumeza ngano nzima nzima muulize huyo Mag3 alioleta ngano za Mushi.

Tumia akili yako tu Mushi anasema kabla ya uhuru madhebu ya Wakirsto yalikuwa yanashinda kusomesha. Swali baada ya uhuru Tanzania tulikuwa na wasomi wangapi wenye elimu ya chuo kikuu.

Watu wanapokea ngano za Mushi sababu Mkristo mwenzao.
 

Na tunakataa "fix" za Sivalon na Van Bergen kwa vile hao ni waislam?¿¿¡??!!
 
Mjadala mnautatiza makusudi kabisa ili usiishe, wenda kwa lengo la kuujazia maoni ambayo kimsingi naona yanajirudia, au kuonyesha jinsi gani watanzania tunavyopendelea mijadala ya uchochezi wa dini.

Mtoa mada anakanusha kwamba baba wa taifa hakuwa na chuki, ugomvi wala matatizo na uislamu, lakini anakubali kwamba kuna waislamu wa kipindi hicho ambao walitaka kupindisha ukombozi wa taifa, na kutaka kuufanya wa kidini zaidi, kwa maana ya kwamba hiwe UISLAMU KWANZA, mwalimu aliwawajibisha watu hao, kwa kufanya hivyo, huyu bwana Mohamedi Said anadai wazee wake wameonewa? Hemu afikirie vizuri, hasiruhusu hisia na matamanio yake kumperekesha kiasi cha kuuacha ukweli uende zake na kuukombatia UPOTOSHAJI.

Swali dogo tu, kama baba wa taifa, mwl.Nyerere angekuwa anapendelea upande wa kikristo, unadhani angewaweka waislamu katika nafasi nyeti na za muhimu katika utawala wake? Mkitaka majina nitawaorodhesha, lakini ni imani yangu wengi mnawafahamu.

Kingine, miaka ya nyuma mtakubaliana na mimi kwamba shule nyingi zilikuwa za makanisa, kama historia inavyojieleza, na waislamu wa miaka ya chini na 1990 walikuwa hawajapata MUHAMKO wa elimu dunia, wengi walipinga vikali vijana wao kwenda kwenye mashule ya kiseminari, kwa kuhofia kuchanganyika na watu wenye imani potofu (huu ndio ulikuwa mtazamo wao hao wazee wa miaka hiyo), kingine walikuwa hawataki vijana wao wale vyakula haramu, mfano Nguruwe maarufu kama kitimoto au mdudu.

Kwa hali hii basi, wengi walijikosesha nafasi nyingi na fursa zilizojitokeza kipindi hicho, huku wakristo wakisoma kwa bidii na kuzipokea fursa kwa kasi, hali iliyopelekea leo wako wengi makazini, yote haya ni kwa sababu walipata mwamko mapema.

Waislamu tusitafute mchawi nani kwenye huu mfumo uliopo, ni mlimbikizo wa makosa ya wazee wetu miaka mingi imepita sasa, naweza kusema, wachawi wa tatizo hili ni sisi wenyewe waislamu, hakuna swala la Mwl. Nyerere.
 

Kadogoo
Sehemu kubwa ya stories za Moh Said kuhusu matukio na majina ya watu, zinaweza kuwa factual na hatuna tatizo nazo. Kasheshe ni pale anapopandikiza chuki za kidini kwa kusema
"inasemekana"...,
"After Mkapa beat a muslim Kikwete in the CCM nomination, hymns were heard"
"The church declared islam as its enemy"
"christian lobby did this or that"
"It was not unconnected to christian lobby"
"Kuna mfumo kristo umefanya na vile".

Statements hizi na nyingine nyingi zisizo na ushahidi (za kufikirika) ndio msingi wa kumpinga. Sisi tunajua kuwa He is on a mission to enrage/radicalize muslim youths.
 
Last edited by a moderator:

Kwa hiyo wewe ulitaka Waislamu wasome ktk shule hizo ili wale vyakula haramu! na kama unakubali vyakula vilikuwa haramu kwanini Shule inaruhusu kupikwa chakula haramu? halali imekuwa bidhaa adimu?
 
Kadogoo
Sehemu kubwa ya stories za Moh Said kuhusu matukio na majina ya watu, zinaweza kuwa factual na hatuna tatizo nazo.

Kama ni hivyo unakubali kuwa Nyerere sio muasisi wa TANU? unakubali kuwa waasisi wengi wa TAA na TANU na wapigania uhuru walikuwa Waislamu? kitabu cha Kivukoni kinamtaja Nyerere ndie mwanzilishi wa Tanu na nyote mnaamini hivyo! kwanini tunawadanganya wa TZ kwa kuwalisha historia hewa?

Mohamed Said kaandika historia halisi lakini mnamwita mdini na mchochezi! sasa thibitisha udini na uchochezi wake!
 
Kama wewe unavyouchukia Uislam na Waislam.
Ritz,
Siwezi kuuchukia uislam wa sina uwezo wa kuwa na chuki na waislam.
Ila na chuki kubwa na mafisadi na mfumo wao wa kulindana, ambao kwao hawaangalii dini kabila wala langi.
Matatizo ya nchi hii hayasababishi na uislam wala ukristo ila serikali ya ccm.
 

Nyerere aliasisi TANU. Kama walikuwepo wengine hiyo ni sawa tu. Lakini sikubali kuwa Nyerere hakuasisi. Chama kimezaliwa 7.7.1954, Rais wa kwanza wa chama asiwe muasisi? Doesn't make sense!
Kuwa wengi walikuwa waislam, ninakubali kuwa wanaharakati hao HASA WA PWANI, wengi wao walikuwa na majina ya kiislam. Sina uhakika sana na uislam wao. Mimi binafsi nina ndugu zangu wapagani ambao wana majina ya kiislam na wengine ya kikristo.

Uchochezi wa Moh Said utauona ukipitia thread hii toka mwanzo, bila jicho la udini. Ningekusaidia ku-extract points zetu zinazomuonesha kuwa ni mchochezi. Bahati mbaya natumia simu.
 
Lawama zinakuja sababu kitabu kimeandikwa kivukoni na kutambulika kama historia rasmi ya wapigania uhuru!

Unaamini kweli ilikuwa ni 'historia rasmi ya wapigania uhuru'. Nani kakuambia kuwa historia ni lazima iwe rasmi ili iwe history?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…