Adabu ni kitu chamsingi sana katika mjadala huu, wengi wameadhibiwa hapa kwamjibu wa sheria za jf kwautovu wa nidhamu kama huo unaouonyesha hapa.Mwandishi mwenyewe unayemtarajia ni huyu anayewatukana wapigania uhuru kama alivyofany baba yake.Unadhani ataweza.Laana ya hao wazee itamwandama yeye na baba yake mpaka siku ya mwisho.
Na sidhani kuwa Mohammed atamjibu mjinga kama huyu.
Hilo linauhusiano gani na utumishi wa Mwalimu Nyerere hapa nchini?Vipi Askofu Kibwetele alipowafungia Wakirsto Kanisani kisha akawachoma moto ili waende peponi mbona umewasahau.
Na ukweli huo si wa maandishi tu hata kutoa takwimu za uongo mja anapoteza sifa hiyo. Kumsingizia mtu kitu kisicho cha kweli sifa inapotea,farki na chuki navyo pia vinaondoa sifa kama ulivyosema Mohamed katika nukuu.
Mohamed, kuna umemjibu Mnyambala kuwa wewe hujamdharau au kumdunisha Nyerere popote pale.
Nachelea kusema kuwa kuna wakati unapoteza ''network'' bila kutarajia.
Mfano, unaposema Nyerere aliandikiwa hotuba na kwenda kuisoma tu je hapo unasemaje.
Yaani mtu mwenye master yake anabeba karatasi hadi New York bila kujua kimeandikwa nini.
Kana kwamba haitoshi umekwenda mbali na kuanika wazi Nyerere alikwenda sokoni bila senti na kupewa pesa na Mshume Kiyate, kwamba hata kama ni kweli hilo ni muhimu sana katika historia! hukulenga kumdhalilisha mzee wa watu kweli.
Mohamed kasema Nyerere alianza siasa baada ya kuonana na Sykes, hapa kweli hukulenga kumdunisha au ulilenga nini.
Ni kundunisha kwasababu Nyerere hakuanza siasa wakati alipomuona Sykes alishaanza miaka mingi tu.
Ukasema Nyerere akikanyaga Dar mwaka 1950 wazee wa mjini walikuwa tayari katika siasa.
Maana yake akitoka bush wazee walishaanza siasa! fair enough! lakini ni ukweli kuwa alikuja mwaka 1950 na si 1946? Kwanini umeficha hilo kama lengo si kumdhalilisha ili aonekane zezeta mbela ya wazee wako.
Mo, Umesema Nyerere aliwachukia waislam, lakini hakuna mahali ulipoonyesha Nyerere akisema zaidi ya hisia zako.
Je hilo si kumdhalilisha marehem ukijua hawezi kujitetea bali kubaki na chuki za watu kwa kosa lisilokuwepo.
Orodha ni ndefu, inatosha kusema tu kuwa ngano nzima ilimlenga Nyerere, kwanza kumdhalilisha, kumdunisha halafu kupitia hayo umjengee chuki kwa watu. Hili huwezi kulikana maana tuna nyuzi zako za kutosha kukuvua nguo zilizobaki
Kuhusu suala la Ponda, Mohamed anasema Ponda hajuti hapo alipo! white elephant!
Huyu Mohamed huwezi kumuona hata kwenye maandamano.
Yeye yupo studio akichagiza wenzake. Leo kuna ambao wamehukumiwa mwaka 1.
Wakati wanaelekea Segerea, Mohamed pengine anaandaa brief case ili aende Durban halafu US.
Akirudi huko anawahimiza wenzake waende asikokutaka! Please rejea maneno yako hapo juu '' sifa ya uislam''.
Kiwanja cha Chang'ombe ni cha waislam na mgogoro uliopo ni baina ya waislam.
Hakuna EAMWS wala Nyerere.
Aliyeuza ni mwislam na aliyenunua ni mwislam, walioshindwa kukaa kitako na kujadili kwa maadili na muongozo wa Quran tukufu, sunna na hadithi ni waislam. Imeelezwa watu wakihitilafiana wafanye nini?
Haijaelezwa watu wakihitilafiana warushe mawe hovyo! wala haijaelezwa haki ni lazima itafutwe kwa fujo na vurugu.
Misinterpretation ya dini ni tatizo kubwa sana.
Ndiyo ile ile ya mtu kumwambia mwenzake jifunge mabomu utaenda peponi wakati yeye hataki kujifunga bomu hilo ili awahi kwanza.
Ni yale yale ya kudanganya watu wasipeleke watoto shule za mfumokristo wakati ambapo Kadinali Pengo akiita ALUMNI wa St Joseph Dar es Salaam Mohamed atapelekewa barua.
Ni yale yale ya kusema kiingereza ni lugha ya mfumokristo wakati MO kila uchao anaongea lugha hiyo na marafiki zake. Tena si kuwa anaongea tu amefikia mahali anaandika kitabu kwa lugha hiyo. Hajaandika historia ya wazee wake kiarabu!
Mohamed, waeleze watu wako kwanza warejee na kuangalia muongozo unasema nini na wala si kutafuta mwamvuli wa majani ya mgomba kwa kutumia mfumokristo.
Tatizo ni la waislam, wanaogombana ni waislam kwasababu ya mali za wakfu za waislam.period
Serikali haiwezi kukaa kimya watu wakitoana rogo hovyo eti kwa kuheshimu dini wakati hao wenye dini hawaieheshimu kwa kuanzia. Bila kukaa chini na kutafakari tatizo ni nini na chanzo chake ni nini, likimalizika la Chang'ombe litafuta la nyumba za wakfu ABCD na huko ni mapanga na pinde. Je ndiyo swifa ya Uislam ulioisema hapo juu.
Hahaahaa Mohamed Said kwa ngano wewe ni nooooooma!Nguruvi,
Umeandika maneno mengi sana.
Ni vigumu kukujibu nukta kwa nukta.
Umezungumzia maandamano kuwa sishiriki maandamano.
Hunijui...
Na wala sina haja ya kukueleza.
Umezungumza mimi kupanda ndege kwenda nchi za nje na kuwaacha ndugu zangu.
Hili nitakujibu.
Maandamano ya kwanza tumetokea Mtoro 1993.
Mabucha ya nguruwe.
Siku chache kabla nilikuwa nimetoka safari...Dar- Paris - Le Havre - Paris - London - Cardiff - London -
Dar - Zanzibar.
Zanzibar ndiyo sakata la OIC nilikwenda kuchapa majibu kwa Kanisa na Serikali katika Khayria Press na
mimi ndiye nilikuwa nilorudi na majibu hayo ambayo tuliyagawa kwa Wabunge wakati huo Bunge linakaa
Karimjee Hall.
(Nina paper nzima kuhusu OIC Insha Allah kama wanaukumbi watapenda nitaiweka jamvini.)
Nimefika Dar nimearifiwa mkutano wa dharura wa kuwawekea dhamana masheikh wetu waliokamatwa kwa
kuvunjwa kwa mabucha ya nguruwe.
Sina haja ya kukeleza nini kilitokea siku ile katika msikiti wa Mtoro ambao mimi nikiswali pale toka utoto wangu.
Sheikh Waziri Ramadhani ex - police officer ndiye aliyewasomea Waislam Qur'an na alichagua aya mnasaba na
hali iliyokuwapo siku ile.
Ilisomwa dua kubwa na tuliondoka kwa maandamano kuelekea Central Police.
Mbele yetu ndugu yetu tukimwita kwa jina la Darwesh alikuwa amebeba bendera ya kitambaa cheusi imeandikwa:
Lailaha Ilallah Muhammad Rasulullah.
Allah siku ile alijibu dua yetu pale pale.
Tumeondoka msikitini jua kali.
Tunafika Uhuru na Titi Street mawingu yanatanda na mvua ikaanza kunyesha.
Tulipambana na polisi Clock Tower na mabomu ya machozi yalirindima.
Ile mvua na upepo ukawa unapeperusha mabomu yale mbali na Waislam.
Nilikuwapo pale.
Mwenzangu alikamatwa na ndiyo ikawa sababu ya yeye kufungwa na kupoteza kazi bank.
Mimi baada ya mapambano yale nilirudi nyumbani kubadili nguo na kujitayarisha zaidi nikaja Mtoro.
Mnazi Mmoja nikakutana na rafiki yangu akanisihi nisende msikitini Mtoro kwa kuwa FFU wamezingira msikiti.
Nilimjibu kuwa nachelea kukimbia vita Allah ananiona.
Sikuweza kufika msikitini kwa kuwa Mtaa wa Mahiwa, Livingstone, Narung'ombe yote ilikuwa imefungwa...
Huwa sipendi kusema haya lakini nimeona nikueleze unijue.
Uoga si katika sifa zangu na ndiyo maana unaona nimeingia hapa na jina langu kamili bila kificho.
Wakuogopewa ni Allah SW pekee na Yeye kaweka ahadi kuwa atakaemuogopa atamfanya asiogope
chochote duniani.
Nami natamani niwe katika wale wasiomwogopa yeyote katika binadamu.
Nadhani tumefahamiana.
Mengine ulosema ni yale yale majibu ni yale yale tunazungusha humo kwa humo.
Nguruvi,
Cheza na watu saizi yako.
TAMKO LA PAMOJA LA MKUTANO MKUU WA DHARURA WA JUKWAA LA WAKRISTO TANZANIA
1.Utangulizi
Jukwaa la Wakristo Tanzania (TCF) linajumuisha Taasisi Kuu za Makanisa nchini kama ifuatavyo:-
Jumuiya ya Kikristo Tanzania - CCT
Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania - TEC
Jumuiya ya Makanisa ya Kipentekoste Tanzania - PCT
Kanisa la Waadventisti Wasabato – SDA (Watazamaji)
Katika Mkutano wake Mkuu wa Dharura uliofanyika katika Kituo cha Mikutano na Mafunzo cha Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania (TEC) Kurasini, Jijini Dar es Salaam, tarehe 8 Machi, 2013; Wajumbe walitafakari kwa undani juu ya kuzorota kwa mahusiano baina ya Dini mbili za Ukristo na Uislamu nchini Tanzania, pamoja na mauaji na mashambulizi ya viongozi wa dini; na hatua zilizochukuliwa na Serikali dhidi ya uhalifu huo unaotekelezwa na Waislamu wachache. Katika taswira hiyo, Kanisa lilitathmini juu ya wajibu, utume, na sauti yake ya kinabii kwa taifa letu kuhusiana na mambo hayo.
2. Hali halisi ilivyo hivi sasa hapa nchini kwa mtazamo wa Kanisa
Ushahidi wa kihistoria na kimazingira unaonyesha wazi kuwa kwa sasa Kanisa nchini Tanzania limo katika kipindi cha mateso ya kimfumo (systematic persecution), kama vipindi vingine 10 vya mateso katika Historia ya Kanisa hapa duniani. Pamoja na mateso haya ya kimfumo, tunatambua wazi kuwa wanaotekeleza haya ni kikundi kidogo tu cha Waislamu wa Tanzania, kama wale wengine wa Barani Afrika (k.m. Boko Haram kule Nigeria). Waislamu walio wengi hawafurahii mambo yanayotokea. Wao pia wanaitazamia Serikali kuthibiti hawa wachache wanaochafua dini ya Kiislamu na kuwafanya Waislamu wote waonekane kuwa maadui wa Ukristo, jambo ambalo siyo kweli.
Kutokana na hali hiyo, mkutano mkuu wa dharura wa Jukwaa la Wakristo umeyaangalia maeneo makuu yenye migogoro ikiwa ni pamoja na:
2.1. Mgororo wa nani anastahili kuchinja kitoweo Hivi karibuni hapa nchini tumeshuhuduia mgogoro juu ya uchinjaji wa mifugo ambayo nyama yake inapaswa kuuzwa kwa watu wa imani mbalimbali wakiwemo Wakristo na Waislamu. Tunafahamu kwamba sheria ya nchi yetu inaweka bayana juu ya usalama wa nyama hizo kiafya, lakini sheria haielekezi kuwa dini fulani ndiyo waumini wake wanapaswa kuchinja mifugo hiyo. Kwa misingi hiyo Kanisa linatamka kuwa:-
a) Hoja ya dini moja kudai kuhodhi (exclusive right) uchinjaji wa mifugo kwa misingi ya imani yake ni kinyume cha haki ya uhuru wa kuabudu ambayo amepewa kila mtu ndani ya nchi hii kikatiba katika Ibara 19.
b) Kwa kuwa kuchinja wanyama na ndege ni Ibada kwa Waislamu, Kanisa litambue na kuheshimu jambo hilo. Lakini pamoja na kutambua haki ya Waislamu kujichinjia wanyama na ndege kama Ibada kwao, Wakristo wasilazimishwe kula nyama zilizochinjwa kwa misingi ya Ibada za Kiislamu. Kwa kuwa wananchi wa Tanzania ni wa dini mbalimbali na mila za makabila mbalimbali, tunaitaka Serikali itamke wazi kuwa kila raia ana uhuru wa kufuata imani yake katika suala la uchinjaji.
c) Kuhusiana na jambo hili tunashindwa kabisa kuelewa msimamo wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Viongozi wengine waandamizi wa Serikali. Wakati wa Serikali ya awamu ya pili chini ya Rais Mstaafu Ali Hassan Mwinyi, ambaye pia ni Muislamu, ulipotokea ugomvi wa mabucha ya nyama ya nguruwe Dar es Salaam, Rais huyu Mstaafu kwa kulinda Katiba ya nchi ambayo aliapa kuilinda, alisema mwenyewe kwa nguvu zote kuwa kila mtu ana uhuru wa kula anachotaka na mtu wa dini moja asimhukumu mtu wa dini nyingine kwa kile anachokula. Baada ya Rais Mstaafu kukemea jambo hili, hali ikawa ya amani na utulivu. Kwa nini Serikali yetu ya sasa inapata kigugumizi kuhusiana na suala zima la nani achinje?
d) Kwa mantiki hiyo hapo juu katika kipengele cha a-c, Wakristo wanaitaka Serikali iweke utaratibu wa kugawana machinjio na mabucha kati ya Wakristo na Waislamu ili kila Mtanzania awe huru kujinunulia kitoweo mahali anapotaka. Sambamba na kuitaka Serikali kufanya hivyo, tunawakumbusha Wakristo wote Tanzania kuelewa kuwa watakuwa hawajavunja sheria yoyote ya nchi wakiamua kujichinjia kitoweo chao wenyewe. Kuhusiana na tangazo hili kwa Wakristo wote, tunaitaka mihimili ya dola (Serikali na Mahakama) kuheshimu Katiba ya Nchi yetu, na kipekee kuhusiana na jambo hili Ibara ile ya 19.
e) Kwa upande mwingine, kwa kuwa tayari zipo bidhaa za vyakula katika nchi hii ambazo zina nembo ya ‘halal' na nyingine hazina nembo hiyo, huu ni uthibitisho kuwa vyakula hivyo vimegawanywa kwa kufuata misingi ya imani za kidini. Kwa hiyo, madai ya kugawanya machinjio na mabucha kwa kufuata misingi ya dini sio jambo jipya kwa sasa katika nchi hii.
2.2 Uchomaji wa Makanisa ulioambatana na vitisho na mauaji ya viongozi wa KanisaKanisa linalaani vikali mauaji ya kidini yanayoendelea kufanywa pamoja na vitisho (systematic persecution) kwa viongozi wa Kanisa na Wakristo wote kwa ujumla.
Mtiririko wa matukio mbali mbali ya nyuma yanatudhihirishia kuwa kumekuwepo na mpango wa muda mrefu wa haya yanayotokea sasa hivi. Tarehe 15 Januari 2011, kundi la Waumini wa Kiislamu walipokutana katika ukumbi wa Diamond Jubilee, miongoni mwao walikuwamo mashehe, walijadili hali ya nchi ya Tanzania kuongozwa kwa mfumo wa kidini. Mkutano huo ulihitimishwa kwa kutoa tamko dhidi ya kile kilichoitwa mfumo Kristo katika nchi yetu!
Japo Serikali na vyombo vyake vya usalama wa Taifa vimekuwa vikipata taarifa za vitisho dhidi ya viongozi wa Kanisa, mauaji, kuchomwa kwa nyumba za ibada, pamoja na maneno ya uchochezi kupitia mihadhara, vipeperushi, CD na vyombo vya habari vinavyomilikiwa na taasisi zinazofahamika, hata hivyo Serikali kwa kiasi kikubwa imeshindwa kuchukua hatua kwa wakati muafaka na wanasubiri hadi maovu yatendeke ndipo ati waanze kufanya uchunguzi. Kwa Serikali yetu inaonekana wazi kuwa katika hili ile methali kwamba "Kinga ni bora kuliko tiba" haina maana yoyote. Hii ni kuonyesha udhaifu mkubwa wa vyombo vya usalama wa Taifa au pia kwamba vyombo hivi vinafurahia kutoweka kwa amani nchini mwetu, jambo ambalo linalifanya Kanisa nchini Tanzania liamini kwamba matukio haya yanayoendelea kutokea ni dalili kuwa Serikali ina agenda ya siri dhidi ya Ukristo.
Kutokana na hayo Jukwaa la Wakristo Tanzania linatamka kama ifuatavyo:
a) Tunatambua kwamba ni jukumu la Serikali kuwatendea raia wake kwa usawa na bila ya ubaguzi kwa mujibu wa Ibara ya 12 na 13 ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Viongozi wa Kanisa wanatamka kwamba Serikali imeshindwa kuheshimu Katiba juu ya hizi haki za raia wake na kupelekea waamini wa dini ya Kikristo kukosa imani na Serikali iliyoko madarakani, hasa kuhusu ulinzi na usalama wao na mali zao kama inavyoagizwa kwenye Ibara ya 14 ya Katiba ya Jamhuri wa Muungano wa Tanzania. Kama Serikali inaona haiwezi kuwahakikishia wananchi usalama wa uhai wao na mali zao, na hivyo kuwafanya waishi maisha ya hofu inayotokana na vitisho, basi kwa mujibu wa Katiba ya nchi yetu, hakuna sababu ya Serikali iliyoko madarakani kung'ang'ania kuongoza nchi.
b) Kwa kuwa ulinzi wa raia ni haki ya kikatiba na kisheria, Serikali inatakiwa iwalinde raia wake. Kama Serikali imeshindwa kuwalinda raia wake, Kanisa linataka Serikali ikiri hivyo ili Kanisa liwaambie wananchi waiwajibishe Serikali na Viongozi wanaoifanya Serikali ishindwe kutimiza wajibu wake.
Jukwaa la Wakristo linasema:
Kama Serikali haitachukua hatua za makusudi dhidi ya mambo haya yaliyoainishwa hapo juu, Kanisa litachukua hatua ya kuwaambia waamini wake kwamba Serikali iliyoko
Sawa Tumeskia..
Heshima yako mkuu - naona kama Walutheli hawakushiriki, walishtukia nini!! Any clue?
Kumbe hukujuwa uzito wa tusi lako kwa wazee hao uliposemaAdabu ni kitu chamsingi sana katika mjadala huu, wengi wameadhibiwa hapa kwamjibu wa sheria za jf kwautovu wa nidhamu kama huo unaouonyesha hapa.
Mods wapo makini wanakuona kile ukisemacho.
Hii adhabu ya mods ikinipata sishangai.Tumezoea ya kule Mbagala,Mwanza na Changombe.Naomba kuwajua hao waislamu wanafiki ambao mzee huyo wa Tabora aliwataja wote hapo mahakamani.
Mzee Said, kwanini wewe hukwenda na kuwa shahidi wa kuwatetea hawa vijana walioambatana na Ponda? Kwanini mmemshakizia Mzee Waikela kufanya kile ambacho wewe ulitakiwa kukifanya? Ungeweza kuwa 'expert witness' kutokana na ujuzi wa 'historia' ya mgongano ndani ya Waislamu nchini.
Shehe Waikela ndiebkasema pale mahakamani kuwa kulikuwa na waislamu wanafiki, na Mohamed amesema wazi kuwa Mzee Waikela aliwataja, nami nikaomba atutajie hapa jamvini.Kumbe hukujuwa uzito wa tusi lako kwa wazee hao uliposema
Hii adhabu ya mods ikinipata sishangai.Tumezoea ya kule Mbagala,Mwanza na Changombe.
Wameshiriki kupitia CCT na PCTHeshima yako mkuu - naona kama Walutheli hawakushiriki, walishtukia nini!! Any clue?
Hawa wazee ni hazina kubwa ya ukweli kwa Tanzania waliobakia.Ami,
Jana nilikuwa mahakamani kusikiliza kesi ya Sheikh Ponda.
Kilichonifikisha pale ni kumsikiliza Sheikh Bilal Rehani Waikela ambae alipanda kizimbani
kutoa ushahidi wake upande wa washtakiwa.
Sheikh Waikela amekuja kutoka Tabora.
Hakika mahakama jana walisikia ambayo si wengi wamepata kuyasikia katika maisha yao
yote.
Sheikh Waikela ameanza kwa kutaja umri wake wa miaka 87 na akaieleza mahakama kuwa
ameanza kuutumikia Uislam mwaka 1940 akiwa katika Anjuman Muslim na ilipokuja East
African Muslim Society ( EAMWS) akawa kiongozi.
Akaeleza pia yeye ni muasisi wa Mabaraza ya Misikiti Duniani makao makuu yake Makka.
Akasema yeye Tabora ni mtu wa tatu kujiunga na TANU na katika Tanganyika ni mtu wa 264.
Sheikh Waikela akaeleza kuwa yeye alikuwa bega kwa bega na Nyerere katika kuipigania uhuru
wa Tanganyika na akimchukua Nyerere ndani ya gari yake Tabora na wakila chakula nyumbani
kwake.
Waikela aliichekesha mahakama aliposema wakati ule alikuwa kijana ana fedha na akicheza tennis.
Akaeleza kuwa Gavana Edward Twinning aliingiza fitna nchini kuhusu Waislam kutaka kuwachonganisha
na Wakristo katika suala la elimu ili avunje juhudi za TANU kudai uhuru.
Nyerere alimsihi Waikela kuwa katika hutuba zake ajitahidi sana kuliweka suala hilo vyema ili pasiingie
mtafaruku na nchi ikawa kama India na Pakistani Waislam na Wahindu wakagawana nchi katika misingi
ya dini.
Waikela akasema hilo walilifanyia kazi na hali ikabaki shwari hadi uhuru ukapatikana.
Matatizo yakaja baada ya uhuru kupatikana.
Waikela akaieleza Mahakama jinsi Sheikh Hassan bin Amir alivyomtahadharisha kuhusu njama zilizokuwa
zinapikwa serikali dhidi ya EAMWS na akamweleza kuwa wanafiki ndiyo wanaotumiwa.
Sheikh Waikela aliwataja Mahakamani wanafiki hao kwa majina mmoja baada ya mwingine.
Akaeleza mkutano wa EAMWS katika Ukumbi wa Aga Khan Girls mwaka 1963 alipomsomea Nyerere risala
ya Waislam kuhusu fitna iliyokuwa ikienezwa nchini dhidi ya Waislam na Uislam.
(Risala hii kwa sasa ni maarufu inajulikana kama ''Moto wa Waislam Ukiwaka.'')
Anasema hotuba hii ndiyo iliyosabaisha yeye kuwekwa kizuizini mwaka uliofuatia 1964 na alipotoka jela alipewa
hati ya kifungo ambayo Sheikh Waikela aliieleza Mahakama kuwa ameitundika nyumbani kwake ukutani kama
pambo.
Mahakama ilifahamishwa kuwa mmoja wa washitakiwa ni binti yake aitwae Dentation Waikela ambae alizaliwa
baba yake ikiwa jela.
Sheikh Waikela akaeleza jinsi Nyerere alivyowawezesha kundi la Adam Nasib kwa fedha na ushirikiano wa serikali
kupita majimboni kuwashawishi Waislam kujitoa EAMWS lakini hawakufanikiwa.
Katika majimbo 20 ni majimbo 8 tu ndiyo yaliyokubali kujitoa.
Hata hivyo serikali ilikatumia nguvu na kuitisha mkutano wa wanasiasa Waislam Iringa na Bakwata ikaanzishwa na
serikali ikaweka askari wenye silaha katika ofisi zote za EAMWS na kuzifunga na makufuli na minyororo.
Binafsi Sheikh Waikela akaeleza Mahakama kuwa alihongwa shs: 40, 000 na Geoffrey Sawaya aliyekuwa Mkurugenzi
wa Makosa ya Jinai, hongo ambayo aliikataa.
Hao waliokubali hongo ile ndiyo walioshirikiana na serikali katika kuiweka BAKWATA madarakani.
Kuhusu kiwanja cha Markaz Chang'ombe anasema kile kiwanja ni mali ya EAMWS na madhumuni yake ilikuwa ni kujenga
Chuo Kikuu.
Kwa hakika alisema mengi na mwisho alimuomba hakimu awape Waislam haki yao.
Mzee wangu Mohamed Said ,
Nianze kusema andiko langu halikukusudia kukebehi au kukejeli wala hakuna sehemu ya maandishi yangu nimewahi kukejeli maandiko yako ingawa yamejaa uongo mwingi.
Nirejee kwa Sheikh Rehani Waikela,Umesema mwenyewe katoka Tabora kaja kutetea wavamizi wa kiwanja Chang'ombe.
Nilitegemea Sheikh Waikela angefanya yafuatayo:
(a) Kwamba BAKWATA hawakuwa na uhalali wa kukiuza
(b) Kwamba EAMWS ni wamiliki wa kiwanja hicho,BAKWATA ni wavamizi wanastahili kushitakiwa either kwa kosa la kughushi nyaraka au kuuza mali wasiyomiliki kihalali.
(c) Kwamba Sheikh Waikela angeishawishi Mahakama EAMWS bado ipo inafanyakazi zake kwa mujibu wa sheria za nchi na angetoa hati kuthibisha uwepo wa taasisi hiyo.
(d) EAMWS ni wamiliki halali wa kiwanja hicho na kwamba taasisi yake ilitoa kibali kwa washitakiwa wajenge msikiti eneo hilo.....
Sheikh Rehani Waikela badala ya kujikita katika utetezi kama kweli alikuwa na utetezi,kaanza histohisia ya uhuru wa Tanganyika.Katumbukiza udini kama sehemu ya utetezi.Ohoo nilifungwa mara niliwekwa kizuizini sasa huo ndio utetezi halafu watu wenu wakifungwa mtasema wameonewa kweli au ndio mtausingizia mfumo kristo.Sana sana Sheikh wenu kaenda mahakamani kujipaiza mwenyewe badala ya kuwatetea walimchangia nauli toka Tabora mpaka Dar.Kanifurahisha kweli pale aliposema alikataa hongo ya sh 40,000/= utamaduni ule ule kama wa Mohamed Said kusingizia marehemu.
Hawa wazee ni hazina kubwa ya ukweli kwa Tanzania waliobakia.
Laiti serikali ingekuwa inatafuta ukweli basi kwa upande wa historia ya waislamu na kudhulumiwa kwao sheikh Waikela angewakilisha wale wengi waliotangulia.
Kwa upande wa muungano basi serikali ingetosheka kuwa haukuwa wa haki na ulikuwa ni ujanja na njama kwa kumsikiliza Hassan Nassor na mwenzake Abdulla Rashid.
Tatizo serikali imeshikilia kulinda mzimu hivyo ina vitu vyake mfukoni inavyopania kuvichomeka katikati ya matatizo yaliyopo nchini.
Kwanini hawa wazee wamepewa umru mrefu.Kwanini Mohammed na Alghasany wameweza kuandika historia si bure na si uhodari wao pekee.Hiyo ni mipango ya Mungu subhaanahu wa taala na huruma zake kwa walimwengu ili ukweli ujulikane na uongo ushindwe.
Ndio maana nazidi kumuasa sheikh wangu Mohammed azidi kushukuru na asijali kejeli za wanaJF waliotumwa na mfumokristo kukandamiza historia ya waislamu ili warudie uluwa wao ulio hatarini kupotea Tanzania baada ya kugundulika kwamba sasa waislamu wameamka.Wao wameogopa historia ya Mohammed zaidi na kusahau mambo mengine mengi yanayowapa ushujaa waislamu kujitetea.
Mohamed, hivi maandamano ya kuvunja mabucha yalianzia kwa Mtoro?Nguruvi,
Umeandika maneno mengi sana.
Ni vigumu kukujibu nukta kwa nukta.
Umezungumzia maandamano kuwa sishiriki maandamano.
Hunijui...
Na wala sina haja ya kukueleza.
Umezungumza mimi kupanda ndege kwenda nchi za nje na kuwaacha ndugu zangu.
Hili nitakujibu.Maandamano ya kwanza tumetokea Mtoro 1993.Mabucha ya nguruwe.
Nguruvi
Cheza na watu saizi yako.
Wameshiriki kupitia CCT na PCT
Habari za saa hizi Yericko, kuna dossier naitayarisha kuiwasilisha kwenye uzi huu, sasa kuna vitu vidogo vidogo vinahitajika ili niweze ku-tie loose ends.
Hivi Yericko mzee wako aliwahi kukufafanulia ni nani au shirika gani lilichangia hela nyingi kama nauli ya kumuwezesha Mh.Kambarage kwenda UN kwa mara ya kwanza, wakati wa harakati zake za kudai uhuru. Najua kuna baadhi ya raia wa kawaida walio changa walicho kuwa nacho - lakini mimi niko interest na aliye toa lion's share, Asante.
Ami,
Insha Allah.
Tutaelimishana taratibu.
Uzi huu naambiwa na wenyeji haujapatapo kutokea.
Nina mengi.
Mohamed, kuna swali hili naona unajaribu kulikwepa. Nikukumbushe kuwa umelileta wewe hivyo ufafanuzi tafadhali.Mohamed, hivi maandamano ya kuvunja mabucha yalianzia kwa Mtoro?
Mohamed, kuna swali hili naona unajaribu kulikwepa. Nikukumbushe kuwa umelileta wewe hivyo ufafanuzi tafadhali.
Maandamano ya kuvunja mabucha yalianza Msikiti wa Mtoro?
Kumbe hukujuwa uzito wa tusi lako kwa wazee hao uliposema
Hii adhabu ya mods ikinipata sishangai.Tumezoea ya kule Mbagala,Mwanza na Changombe.