Uchochezi wa Mohamed Said na dhihaka kwa Wapigania Uhuru wa Tanganyika na Zanzibar

Uchochezi wa Mohamed Said na dhihaka kwa Wapigania Uhuru wa Tanganyika na Zanzibar

Jasusi,

Mbona wengi tumesoma shule hizo si ndiyo Waingereza
wakishirikiana na Wamishionari katika elimu?

Sasa tungesoma wapi wakati shule ndiyo hizo za serikali
na misheni?

Si jambo la kushangaza.

Nimepata kuandika paper kuhusu matatizo ya elimu kwa Waislam wa
Tanzania: TheQuestion of Muslim Stagnation in Education in Tanzania
- A Muslim Riddle
(Paper presented at the Conference of the Global
World of the Swahili
Intercultural Dialoguemon the Indian Ocean Zanzibar,
February 20 - 23, 2003).

NB: Nimeshangazwa jana kuna mtu kaniletea link na nimeiona hii paper ikinasibishwa
na BBC.j
Kwa hiyo unakubali kuwa enzi za ukoloni na kabla yake hakukuwepo shule za waislamu. Unakubali kuwa wamisheni ndio walioshughulika kujenga shule. Sasa iweje leo uelekeze lawama zako kwa serikali ya Nyerere ambayo ilichukua jitihada kutoa nafasi ya elimu kwa Waislamu baada ya uhuru kwa kutaifisha shule za misheni? Mbona suala hili linakupa kigugumizi?
 
Mzee wetu anajichanganya tu hapa, hajui asimamie wapi.
 
The master of hyperbole!!

Jakaya Mrisho Kikwete - Rais wa JMT - Muislamu - anakula matunda ya Uhuru
Dr. Ghaib Bilal - Makamu Rais wa JMT - Muislamu - anakula matunda ya Uhuru
Dr. Omar Chande - Jaji Mkuu wa TZ - Muislamu - anakula matunda ya Uhuru
IGP Said Mwema - Mkuu wa Jeshi la POlisi - Muislamu - anakula matunda ya Uhuru
Dr. Abdallah Kigoda - Waziri - Muislamu - anakula matunda ya Uhuru
Dr. Ramadhan Dau - Mkurugenzi wa NSSF - Muislamu - anakula matunda ya Uhuru
Shamsi Vuai Nahodha - Waziri MODANS - Muislamu - anakula matunda ya Uhuru

Tukiuliza hapa watu waanze kutaja maelfu ya Waislamu "wanaokula matunda ya uhuru" wa nchi yao utashangaa jinsi walivyo wengi!
Wapo madaktari
Walimu
Wanajeshi
Maprofesa
Mainjinia
Wanasheria
n.k!!

Kauli yako kuwa atu 'mnakula peke yenu' ni ya ulaghai, inakataa historia na inapuuzia mafanikio ambayo Waislamu na Wakristu wameweza kuyapatta katika miaka hii yote. Lakini pia inapuuzia ukweli kuwa kuna watu wengi tu (Waislamu na Wakristu kama vile wasio na dini vile vile) ambao maisha yao ni magumu na hayo matunda ya Uhhuru hawayaoni. Mamia ya watoto wetu wamefeli na wanaishi maisha magumu barabarani na kwenye vituo vya kutunzia yatima; utashangaa ukikuta siyo wote wanaitwa 'Khalid" au "Salma"!!! Wapo wengi tu kina "Paul" na "Joyce"!!!

Ushahidi huu ni mfano wa Baba anakula wali na mchuzi wa nyama pamoja na watoto wake huku nyama zote anakula mwenyewe na wanawe wali na mchuzi mtupu! Baba akiulizwa watoto nao wamekula wali na nyama? jibu ni ndio! watoto wakiulizwa mmekula? jibu ni ndio lakini bila nyama!

Mwanakijiji,
unadai vigogo hao hapo juu ni Waislamu! mbona ukipewa uwiano wa mgao wa madaraka ulivyo na ubaguzi TZ huwa unasema utajuaje kama Ali ni Mkristo au John ni Muislamu? sasa wewe umejuaje kama Ramadhani Dau au Nahodha na wengine ni Waislamu?
 
  • Thanks
Reactions: Ami
Za saa hizi mkuu Said, hivi Mh.Kambarage alipo hacha kazi pale Mwakanga na kujikita katika mambo ya siasa full time, kumbuka wakati huo alikuwa na familia changa yaani mkewe, watoto na mama yake mzazi wote hao walikuwa wanamtegemea! Sasa swali nani alikuwa anampatia hela za kijikimu kimaisha yeye na familia yake kwenye wakati mgumu aliyo kuwa nao.

Ni nani aligharimia safari yake ya kwanza ya kwenda UN. Ndio hayo mkuu wangu.
Padre Art Wille alikuwa akimlipa shilingi mia sita 600/= Mwalimu Nyerere akiwa tangu alipoamua kuacha kazi pale Pugu,

Mzee Nyerere aliwahi kusema kuwa Art alikuwa ni bosi wake muhimu,

Kumbuka Art alikuwa ni Padre wa kikatoliki akihudumu katika shirika la Maryknoll ambalo ndilo liliratibu safari ya kwanza ya Mwalimu pale UNO.
 
Kwa hiyo unakubali kuwa enzi za ukoloni na kabla yake hakukuwepo shule za waislamu. Unakubali kuwa wamisheni ndio walioshughulika kujenga shule. Sasa iweje leo uelekeze lawama zako kwa serikali ya Nyerere ambayo ilichukua jitihada kutoa nafasi ya elimu kwa Waislamu baada ya uhuru kwa kutaifisha shule za misheni? Mbona suala hili linakupa kigugumizi?

Jasusi,
Tutazungushana hadi asubuhi.

Historia ya Nyerere na Waislam leo ni mashuhuri.
Hakuna asiyeijua.
 
Gwalihenzi, nionyeshe mahali mzee MS amesema yeye ndiye mwenye"historical knowledge"peke yake ya AA na TANU baba ficha upumbavu wako onyesha busara zako angekuwa na majivuno asinge jadiliana na vilaza kama wewe huku jf
Wewe mtoto, nilishakuambia kwamba hutumii akili yako na ndio maana unatukana hovyo humu jamvini. Hivi ni nani anayeonesha upumbavu? ni mimi au huyo mzee wako Mohamedi Said ambaye kwako wewe unamuona kama vile mtume! haya soma huu upumbavu wake hapa chini na kisha utoe hukumu sahihi juu yake;
WC,

Unataka tubishane kwa kitu ambacho waliasisi wazee wangu
na mie kuijua historia yake?

Hivi wewe utaijua AA kuliko mimi mjukuu wa waasisi hawa?
Hivi wewe utaujua undani wa TANU kunishinda?

Huo ni muhali.
Sasa umeuona upumbavu wa mzee wako? Ati kwakuwa AA na TANU waliasisi wazee wake, basi ni yeye tu (Mohamed Said) anayeujua undani wake! wengine hawawezi kujua! Kwani kuasisi chama ilikuwa ni miliki ya wazee wake tu? akina Cecil Matola hawakuwepo na hawakujua AA, Nyerere ambaye alikikuwa raisi wa kwanza wa TANU hakuijua TANU? Vipi taarifa za vyama hivyo igeuke kuwa miliki ya mzandiki Mohamedi Saidi?
 
Wewe mtoto, nilishakuambia kwamba hutumii akili yako na ndio maana unatukana hovyo humu jamvini. Hivi ni nani anayeonesha upumbavu? ni mimi au huyo mzee wako Mohamedi Said ambaye kwako wewe unamuona kama vile mtume! haya soma huu upumbavu wake hapa chini na kisha utoe hukumu sahihi juu yake;Sasa umeuona upumbavu wa mzee wako? Ati kwakuwa AA na TANU waliasisi wazee wake, basi ni yeye tu (Mohamed Said) anayeujua undani wake! wengine hawawezi kujua! Kwani kuasisi chama ilikuwa ni miliki ya wazee wake tu? akina Cecil Matola hawakuwepo na hawakujua AA, Nyerere ambaye alikikuwa raisi wa kwanza wa TANU hakuijua TANU? Vipi taarifa za vyama hivyo igeuke kuwa miliki ya mzandiki Mohamedi Saidi?

Mkubwa nimekwambia nionyeshe mahali amesema niyeye tu anajua hitoria ya AA na TANU hujanioyesha humuelewi mzee au ni kiburi chako, huyu mzee humuwezi mfano wako na mzee MS ni sawa na mtu kupiga kichwa ukuta halafu unasikitikia ukuta badala ya kusikitikia kichwa chako upo hapo Dingi.
 
Hayo ndio matatizo ya ushabiki wa kijinga, huoni wala husikii chochote dhidi ya Mohamedi! basi baki na ututusa wako mjinga wewe.
 
Mkubwa nimekwambia nionyeshe mahali amesema niyeye tu anajua hitoria ya AA na TANU hujanioyesha humuelewi mzee au ni kiburi chako, huyu mzee humuwezi mfano wako na mzee MS ni sawa na mtu kupiga kichwa ukuta halafu unasikitikia ukuta badala ya kusikitikia kichwa chako upo hapo Dingi.

Boko Haram,
Hakuna kitu kisichokuwa na mmiliki wake.

Ushahidi wa kuwa mimi najua kushida yoyote humu kuhusu TANU uko mwingi.

Nimeweka humu mambo mengi kuanzia nyaraka hadi picha nilizopewa na wazee
wangu kuhusu chama cha TANU.

Katika nyaraka hizo zimo hadi nyaraka za Nyerere mwenyewe.

Katika hali kama hii nani atasimama na mimi tushindane kuhusu kuijua historia ya
uhuru?

Hilo achilia mbali.
Nani hapa jamvini aelezaye historia ya TANU?

Nimeeleza kuwa baba yangu alikuwapo wakati wa harakati na kaona kila kitu kwa
jicho lake anakumbuka hadi siku alipomuona Nyerere kwa mara ya kwanza nyumbani
kwa Abdu Sykes Stanley Street mwaka 1952.

Hivi ni vitu vya kawaida ni historia ya watu ambayo haina sababu hata kidogo ya hata
kwa mbali kumghadhibiosha mtu na kuanza kutoa lugha zisizopendeza za ''uzandiki'' nk.

Ni mimi peke yangu kiasi nimevutia watazamaji 100,000 historia katika JF.
Wenyeji wananambia hii haijapata kutokea.
 
WildCard, hata usisumbue akili yako...huyu mchochezi Mohamed Said ni mtu wa ajabu sana na hatari lakini taratibu wengine tunaanza kuigundua janja yake na hila zake...kamwe si bure.

  • Kwa makusudi kabisa hamtambui kiongozi mkuu mwanzilishi na Raisi wa kwanza wa AA mwaka 1929, Mwalimu Cecil Matola wala msaidizi wake Makamu wake Ramadhani Ali! Cha ajabu anamtambua katibu wake Kleist Sykes na kumpa heshima zote za uasisi eti toka akiwa Burma!
  • Kwa makusudi kabisa hamtambui kiongozi mkuu muasisi na Raisi wa kwanza wa TAA wa kuchaguliwa mwaka 1950 Dr. Vedasto Kyaruzi wala Makamu wake! Cha jabu anamtambua katibu wake Abdulwahid Sykes mtoto wa Kleist Sykes na kumpa sifa zote za kuongoza mabadiliko ndani ya TAA!
  • Kwa makusudi kabisa hamtambui kiongozi mkuu muasisi na Raisi wa kwanza wa TANU mwaka 1954 Mwalimu Julius Kambarage Nyerere wala Makamu wake John Rupia na badala yake sifa zote zinaelekezwa kwa katibu Abdulwahid Sykes, kipenzi cha wengi aliyekuwa na mvuto wa pekee!
Sasa hapa swali linakuja, kwa nini ameamua kupindisha mambo hivyo? Huyu Mohamed Said, mtoto wa Kimanyema, mbona anawatetea sana hawa Wazulu ambao hata kwenye Uislaam hasemi waliingia lini na kwa sababu zipi? Ana uchungu gani? Uhusiano kati ya koo hizi mbili unatokana na nini?

Kwa nini anafanya sana jitihada za kuwaengua viongozi wa juu waanzilishi wa AA, TAA na TANU na badala yake anawapa sifa wasaidizi wao? Toka lini Katibu anakuwa na nafasi ya juu kuliko Raisi/Mkurugenzi? Kwa mfano;

  • Amewahi kudai kuwa pamoja na msomi Mwalimu Cecil Matola kuwa Raisi muasisi wa AA hakuwa chochote bali ni katibu wake Kleist Sykes aliyepanga na kuiendesha AA.
  • Amewahi hata kudai kuwa mwaka 1950 ni katibu wa TAA Abdulwahid Sykes ndiye alimteua bosi na Raisi wake Dr Vedasto Kyaruzi kwenye kamati iliyoandaa mikakati na malengo ya TAA.
  • Amewahi kudai kuwa pamoja na Mwalimu Nyerere kuchaguliwa kuwa Raisi muasisi wa TANU mwaka 1954 ni katibu wake Abdulwahid Sykes ndiye aliyesimamia mipango yote ikiwa ni pamoja na kumuandalia hotuba aliyoisoma UN.
  • Amewahi kudai kuwa pamoja na Makamu wa TANU mwaka 1954 kuwa mfanya biashara mkuu mwenye uwezo mkubwa kifedha, John Rupia lakini ni Abdulwahid Sykes na ndugu zake ndio waliokuwa wakitoa fedha zao kuiendesha TANU.
  • Amewahi kudai kuwa pamoja na Mwalimu Nyerere kulipwa mshahara mkubwa wakati huo, hakuweza kujitosheleza hata kwa nauli achilia mbali kununua mboga hadi mchuuzi wa Kariakoo Mshume Kiyate alipomfadhili.
  • Amewahi kudai kuwa pamoja na msomi Mwalimu Nyerere kuanza siasa toka akiwa chuoni Makerere kwenye miaka ya 1940s ilibidi apigwe msasa, kupewa shule na kufundishwa ustaarabu na wazee wa Gerezani kuhusu siasa!
Huyo ndiye Mohamed Said anayepiga lecture ughaibuni kuhusu harakati za kudai uhuru wa Tanganyika na wazee wake walivyosahauliwa na kunyanyaswa baada ya uhuru na Mwalimu Julius Nyerere! Kwa nini, huyu Abdulwahid Sykes anayemuongelea sana na kupiga kelele, watoto wake wako kimya! Je kulikoni?

Mohamed Said ni mjanja sana, katoka mbali toka wakati wa WARSHA na MSAUD akiwa na Pro. Njozi na Dr. Dau. Bahati mbaya nyumba waliyoijenga ya theluji wanashuhudia kwa macho yao ikianza kuporomoka kwani jua linaanza kujitokeza! It is just a matter of time, njama na hila zake zote zitaanikwa.

THERE IS NO HONOURABLE WAY OF DENYING THE TRUTH..
THERE IS NO GENTLE WAY OF DESTROYING IT,
THERE IS NOTHING GOOD IN OPPOSING IT EXCEPT ITS REALIZATION..
upokee tuh huo ukweli hata kama ni mchungu ndugu yangu..
 
NYERERE, KARUME WATAJWA KESI YA WAFUASI WA PONDA

Baba wa Taifa, Hayati Mwalimu Julius Nyerere
Shahidi wa utetezi na Mwanzilishi wa Baraza la Misikiti Tanganyika, Bilali Waikela (87), amedai mahakamani katika kesi inayomkabili Sheikh Issa Ponda na wenzake 49, kwamba Baba wa Taifa, Hayati Mwalimu Julius Nyerere na Rais wa kwanza wa Zanzibar, Shekhe Abeid Karume, walivunja Umoja wa Waislamu wa Af...rika Mashiriki.

Waikela alidai kuwa umoja huo ulianzishwa kwa lengo la kuwatetea na kuwasaidia Waislamu na kwamba Tanzania ilipata kiwanja cha Chang’ombe Marcas kutoka kwa aliyekuwa Rais wa Misri.

Waikela ambaye ni shahidi wa 48 wa upande wa utetezi katika kesi hiyo alidai kuwa, umoja huo ulifutwa baada ya Karume kudanganywa kuwa wana mpango wa kufanya mapinduzi na kuwarudisha Waarabu Zanzibar.

“Mwalimu Nyerere ndiye aliyemtuma Karume afanye hivyo na mwaka 1964 nilifungwa baada ya kukataa kupokea Shilingi 40,000 ili nikubali kuvunja umoja huo, na Kassim bin Juma, Adam Simba na Salehe Masasi waliotumiwa kuhamasisha watu kuvunja umoja huo,” alidai.

Alidai kuwa ofisi za umoja huo zilifungwa hadi mwaka 1968 lilipoundwa Baraza la Waislamu Tanzania (Bakwata) na kukabidhiwa ofisi pamoja na mali zote kikiwamo kiwanja cha Chang’ombe markazi kilichokuwa kimejengwa shule ya Waislamu.

CHANZO: NIPASHE, 21st March 2013See More
 
Boko Haram,
Hakuna kitu kisichokuwa na mmiliki wake.

Ushahidi wa kuwa mimi najua kushida yoyote humu kuhusu TANU uko mwingi.

Nimeweka humu mambo mengi kuanzia nyaraka hadi picha nilizopewa na wazee
wangu kuhusu chama cha TANU.

Katika nyaraka hizo zimo hadi nyaraka za Nyerere mwenyewe.

Katika hali kama hii nani atasimama na mimi tushindane kuhusu kuijua historia ya
uhuru?

Hilo achilia mbali.
Nani hapa jamvini aelezaye historia ya TANU?

Nimeeleza kuwa baba yangu alikuwapo wakati wa harakati na kaona kila kitu kwa
jicho lake anakumbuka hadi siku alipomuona Nyerere kwa mara ya kwanza nyumbani
kwa Abdu Sykes Stanley Street mwaka 1952.

Hivi ni vitu vya kawaida ni historia ya watu ambayo haina sababu hata kidogo ya hata
kwa mbali kumghadhibiosha mtu na kuanza kutoa lugha zisizopendeza za ''uzandiki'' nk.

Ni mimi peke yangu kiasi nimevutia watazamaji 100,000 historia katika JF.
Wenyeji wananambia hii haijapata kutokea.
Wewe ni mzee mpuuzi na muongo wa kutisha sana! hayo majivuno na majigambo yasiyo na maana wala ukweli wapelekee watu wako wa kwenye mihadhara yako ambao wanakuona kama mtume wao. TANU ilikuwa "mass party"ikiwahusisha watanganyika wengi sana ambao kwa kila siku waliongezeka idadi. Iweje wewe useme ni wewe pekee ndie unayejua historia ya uhuru.?
Mara ngapi humu jamvini umeoneshwa uongo na uzandiki wako, na wewe kwa aibu sana ukaishia kudai kuwa umeandika historia ya wazee wako na hivyo wengine waandike ya kwao? vipi sasa unakuja na majivuno ya kipumbavu ati wewe pekee ndie unayejua historia ya uhuru?
Unakuja na swali la kipumbavu ati "ninani hapa jamvini aelezae historia ya TANU?", Mohamed, mara hii umesahau kuwa ulidai kuwa uliandika historia ya wazee wako waliosahauliwa na sio historia ya TANU? umekosa mshipa wa aibu katika umri wako mkubwa? Mara ngapi umeoneshwa ushiriki wa watu wengine nje ya Gerezani na Tandamti katika harakati za TANU kupigania uhuru ukabaki ni vilio vya kipumbavu vya historia ya wazee wako?
Mohamed Said, nakwambia wazi kabisa kwamba wewe huna unalolijua kuhusu historia ya uhuru wa Tanganyiaka zaidi ya uzandiki, uzushi, uongo, uchochezi, fitina, majungu na kuwakatisha tamaa vijana wa kiislam wa Tanganyika wasijiamini ili wewe uwatumie katika kujipatia umaarufu wakipumbavu ambao kwa umri wako mkubwa hautakuwa na manufaa yoyote zaidi ya kuchukiwa na wapenda amani wa nchi hii.
 
Dah sawa mkubwa sio makosa yako ni aliyekuleta mjini
 
Boko Haram,
Hakuna kitu kisichokuwa na mmiliki wake.

Ushahidi wa kuwa mimi najua kushida yoyote humu kuhusu TANU uko mwingi.

Nimeweka humu mambo mengi kuanzia nyaraka hadi picha nilizopewa na wazee
wangu kuhusu chama cha TANU.

Katika nyaraka hizo zimo hadi nyaraka za Nyerere mwenyewe.

Katika hali kama hii nani atasimama na mimi tushindane kuhusu kuijua historia ya
uhuru?

Hilo achilia mbali.
Nani hapa jamvini aelezaye historia ya TANU?

Nimeeleza kuwa baba yangu alikuwapo wakati wa harakati na kaona kila kitu kwa
jicho lake anakumbuka hadi siku alipomuona Nyerere kwa mara ya kwanza nyumbani
kwa Abdu Sykes Stanley Street mwaka 1952.

Hivi ni vitu vya kawaida ni historia ya watu ambayo haina sababu hata kidogo ya hata
kwa mbali kumghadhibiosha mtu na kuanza kutoa lugha zisizopendeza za ''uzandiki'' nk.

Ni mimi peke yangu kiasi nimevutia watazamaji 100,000 historia katika JF.
Wenyeji wananambia hii haijapata kutokea.

Mwanzoni pale nilipata huzuni na kuhisi ya kwamba utatuacha na kuondoka zako,ila nimefarijika kwa uwepo wako hadi dakika hii,kwa kweli mengi nimenufaika kwa elimu yako,,

Nawaonea huruma hao aliowasema boko haramu wanaojaribu kupiga kichwa ukuta na kuishia kuusikitikia ukuta badala ya kusikitikia vichwa vyao..
Hawakuwezi na hawatakuweza..
 
Ushahidi huu ni mfano wa Baba anakula wali na mchuzi wa nyama pamoja na watoto wake huku nyama zote anakula mwenyewe na wanawe wali na mchuzi mtupu! Baba akiulizwa watoto nao wamekula wali na nyama? jibu ni ndio! watoto wakiulizwa mmekula? jibu ni ndio lakini bila nyama!

Mwanakijiji,
unadai vigogo hao hapo juu ni Waislamu! mbona ukipewa uwiano wa mgao wa madaraka ulivyo na ubaguzi TZ huwa unasema utajuaje kama Ali ni Mkristo au John ni Muislamu? sasa wewe umejuaje kama Ramadhani Dau au Nahodha na wengine ni Waislamu?

inaonekana umeshindwa kuelewa point niliyokuwa najaribu kuionesha; Mwalimu wenu hapa wa mantiq amesema wanaokula matunda ya Uhuru ni "nyinyi peke yenu"; manake ni kuwa hakuna Muislamu anayefurahia matunda ya Uhuru isipokuwa Wakristu. Kwenye mantiq ukiweza kuonesha inconsistency kwenye moja basi hoja nzima inaanguka isipokuwa kama imekuwa qualified. MS hajui kuqualify sentensi ndio maana nimesema mahali huko nyuma huyo aliyemfundisha Mantiq angecharazwa viboko!

Lakini la pili ni kuwa utaona nimewataja wale tu ambao wamejitambulisha na kuonesha imani yao ni Waislamu; Dau, Kikwete na wengine sijawasingizia; wamejitambulisha hivyo hadharani na wengine tunafahamu historia yao katika harakati hizi za kupinga 'dhulma' huku wao wakila na kufurahia matunda ya uhuru! Lakini kama wanaokula matunda ya Uhuru ni Wakristu 'peke' yao basi hawa wengine wote ambao wanajitambulisha kuwa ni Waislamu na wanakula matunda ya Uhuru kwa hakika si Waislamu bali ni Wakristu waliojifisha!
 
Back
Top Bottom