Kadogoo;5981465]Mimi pia point yangu hujaielewa! ktk kila viongozi 10 nchi nzima Waislamu takriban 2 kati ya wenzao 8 nani wanaofaidi matunda ya uhuru? mfano hai angalia baraza la mawaziri Waislamu ni wangapi? wakristo? na wapagani? sasa wewe unatutajia Rais na makamu wake ati wanafaidi matunda! mbona huendi mbali zaidi kwani matunda ya uhuru sio Urais na Umakamu! angalia Mawaziri, manaibu na makatibu wakuu na manaibu wao! Wakuu wa Mikoa, wilaya, katibu tawala mikoa, wakurugenzi na vigogo wote wa mashirika ya umma na Serikali, Mabalozi, MaRPC wa mikoa na wilaya, wafanyakazi Serikalini na mashirika ya umma! viongozi wa Jeshi, Polisi na Magereza!, najua jibu lako litakuwa: utajuaje kama huyu ni Muislamu au dini nyingine? au utasema, ajira inazingatia taaluma na sio dini! au pia huenda ukajibu hivi: hata mamilioni ya Wakristo hawana ajira na hawafaidi matunda ya uhuru! wote tunasota sawia!
kama ni hivyo unashauri tuitoe CCM na kuwapa Chadema ili wananchi wote wafaidi matunda ya uhuru?
Kadogoo, hapa ndipo huwa nasema, Mohamed amefaulu sana kuwafanya watu wafikiri kidogo kuliko kufikiri sana. Wakishafanikiwa kufikiri kidogo inahitaji nguvu kidogo sana ili kuweza kuwasha moto kwasababu wakati huo fikra zitakuwa zimefungika na watu wanaangalia katika upenyo mdogo.''Narrow angle''
Abdul Sykes kama alivyokaririwa na Mohamed alisema ''nia ya uhuru ni kumkomboa mwafrika kutoka madhila ya ukoloni''.
Hakusema kuwakomboa watu wa aina fulani.
Matunda ya uhuru si uwaziri, RPC, ukuu wa wilaya au mikoa n.k. Matunda ya uhuru ni yale yanayomwacha Mtanganyika huru kujitafutia maendeleo yake kama mwanadamu mwingine bila kufungwa pingu.
Ni yale yanayomsaidia mwanadamu kuamua hatima ya maisha yake na kwa mipango yake popote alipo na kwa wakati wowote.
Matunda ya uhuru hayaangalii ni nani mkuu wa wilaya ya Kilwa, yanangaalia kwanini wanafunzi 300 wa shule ya sekondari ya Kilwa wameaacha shule na shule hiyo kufungwa.
Matunda ya uhuru ni yale ya mpango wa maendeleo wa mwaka 1963 ulizingatia sana ujenzi wa Hospitali ya Kinyonga pale Kivinje na kwingineko ambako huduma zilikuwa duni wala si kupata mkuu wa mkoa kutoka kivinje.
Nikichukua mfano wako nisioutaka hata kuufikiria, hivi baraza la mawaziri likiwa na asilimia 98 waislam, hiyo itakuwa imemsaidiaje mwislam wa Mjasani Tanga, Nyakanga, Kamunyonge na kule Mikindani?
Ni mawazo ya aina hiyo yanayofanana na yale ya utafiti wa wanafunzi wa kuingia Faculty of art ya UDSM ulihotimisha kuwa waislam ni asilimia 20 tu. Utafiti huo haouonyeshi ni kiasi gani waislam walichaguliwa kujiunga na vyuo vya ufundi vya kati n.k.
Kwamba Faculty nzima ikiwa na asilimia 100 waislam basi matatizo ya waislam wa Mkuzi, Kwasadala, Isevya na Tunduru yatakuwa yamekwisha. Ukishafikiria hivyo basi ujue matunda ya uhuru hutayapata na wala huna mpango wa kuyapata.
Kadogoo, hivi wewe ulishawahi lini kununuliwa sukari na waziri kwasababu tu ni mwislam?
Ukienda kariakoo wateja wananunua nyanya na viazi bila kuonyesha ID kama wanunuavyo sukari na unga madukani.
Wapi unapata ushahidi wa kusema matunda ya uhuru yanaliwa na wachache?
Matunda ya uhuru ni wewe kuwa huru kufanya yale yanayosaidia familia yako na taifa na wala si uwaziri, katibu mkuu n.k.
Ukishaweza kufikiria out of the box tayari una matunda ya uhuru, ukiamua kuamini hadithi za wafanyabiashara wa magazeti na vitabu hakika una tatizo na miaka 20 ijayo utakuwa pale pale unadai matunda ya uhuru wakati wenzako wanaoshughulisha vichwa wapo kivulini wana menya na kula
We unaona hapa hakuna tatizo? Kwanini Waislamu ndio wenye kuandamana kila wakati tangu enzi za Mwinyi, Mkapa na sasa Kikwete? au wanadanganywa na akina MS na Wenzake?
Kuandamana hakujawa suluhu ya tatizo hata siku moja. Kuandamana ni njia tu ya kuonyesha hisia lakini si suluhu.
Nakuhakikishia kuwa sehemu kubwa ya waandamanaji huwa hawajui kwa kina wanaandamana kwanini.
Tazama watu wanaokwenda segerea kwa maandamano hakuna mwenye uelewa wake aendae huko.
Ni hawa vijana waliopigika wanaotafuta mahali pa kuteremsha hisia zao kama vijana wengine.
Tofauti ni kuwa wao wanatumia dini badala ya uhalisia wa maisha.
Leo ukiitisha maandamano kuhusu hali ngumu ya maisha utapata watu wa rika zote na imani zote kwasababu dhiki ni across the board.
Kadogoo, kutembea ni sehemu muhimu sana ya elimu. Pengine hilo ndilo linanifanya nijiulize kila siku hivi kuna tofauti gani ya umasikini wa pale kwa father Libaba Nyangao,kule Nandembo, Peramiho, Mchukwi,bumbuli, Magila, Ikizu, Kisiwani Same, Mashati, Oloi toktik, Haidan ukilinganisha na Nanjilinji, Lusanga, Mkongo, Mtimbira, Mlimba n.k.?
Jibu ni hakuna ! maana yake ni kuwa afadhali ipo kwa mtu na wala si watu!
Namshukuru sana mungu kwa kuniwezesha kuishi maeneo ambayo ni lazima mtu ajiulize kabla hajanijengea hoja za uwaziri, ukatibu mkuu, takwimu za UDSM n.k. kwasababu nimeishi na kuona mtoto akifariki kwasababu tu wazazi hawamudu kununua dawa ya sh 1600.
Na wala si katibu kata, tarafa, mkuu wa wilaya au mkoa, waziri aliyesimama na wazazi hao wakibeba mtoto wao wa miaka 6 kwa machungu kwenda kufanya maandalizi ya mazishi.
Leo tunaambiwa matunda ya uhuru ni majina ya John, Hussein,Rose na Halima!
Kwamba ukiitwa majina hayo hatakama huamini yanatokana na nini basi uwezekano wa matunda ya uhuru kukufikia ni asilimia 100.
Watu wazima wamekaa katika majamvi wakifundisha ujinga huu tena kwa bidii na wakitokwa jasho
kwanini ni viongozi wa Kiislamu na waislamu ndio wanakamatwa na kufungwa jela?
Hivi nchi itakuwaje ukiwa na akina Ilunga kila mahali.
Kwamba mtu anahubiri kumtoa roho mtu mwingine, kwasababu tu kavaa msalaba au Baragahashia basi huyo aachwe.
Uongozi ni responsibility na si kila mwehu ni kiongozi. Hatuwezi kuacha nchi ivurugwe na wapuuzi kwasababu tu ni viongozi wa dini.
Dini gani inaamuru kumtoa roho mwanadamu mwingine?
Kiongozi asiyejiheshimu akamatwe hadharani, avuliwe msalaba au baraghashia na atupwe katika karandinga!period
kwanini Polisi huingia Misikitini na viatu wanapiga waumini wakiswali na kuwasweka rumande bila hata dhamana?
Na kwanini wahalifu wakimbilie misikitini au makanisani? Huko misikitini kuna watu wanaiba viatu na wanaadhibiwa ndani ya misikiti tena bila kusikilizwa. Labda ujiulize kwanini wahalifu walkimbilie misikitini kwanza!
ulishasikia Polisi wanavamia Makanisa na kupiga waumini wakiabudu?
Nadhani kuna upungufu wa kulielewa hili. Katika miaka 70 namwanzoni mwa 80, kule Sumbawanga kuna kanisa la watchtower. Si kuwa Polisi waliingia na kukamata viongozi bali kanisa hilo lilipigwa marufuku kabaisa. Mgogoro wa Meru n.k.
Kitu cha muhimu hapa si kulinganisha nani anafanya maovu, muhimu ni kwanini maovu yanatokea tena kwa kupangwa ndani ya nyumba za ibada ziwe za kikristo au kiislam.
Ndugu yangu Mwanakijiji:Waislamu wana dukuduku na simanzi! chama chako kinamikakati gani ya kujibu hoja zao?
Nadhani tumewahi kumuuliza Mohamed duku duku ni lipi na anafikiria suluhu ipi.
Hakika hajaweza kuja na jibu isipokuwa lile la serikali kutakiwa kutoa majibu. Kinachoshangaza ambacho ni uchochezi wa dhahiri ni kuwa Mohamed yupo kila mhalai kuelezea madhaila ya waislam, hajawahi kusema suluhisho liweje.
Kitu ambacho ni cha hatari sana ni kuchagua wataalam kwa kutumia imani zao.
Hutuwezi kuwa na Daktari kwasababu tu ana jina la John au Hussein.
Utaalam unasomwa na hivyo imbalance itakuwepo endapo jamii fulani itadhani kuwa kupata Chartered account unatakiwa uteuliwe.
Kuwa, mwalimu unatakiwa uteuliwe, na kuwa profesa kama Safari au Mikidadi unatakiwa uteuliwe.
Hili hiliwezakani na kwa msingi huo huwa najiuliza kwanini mtu afikirie kuwa tatizo la waislam ni mawaziri 20 na siyo milioni zaidi ya 20! This kind of mentality ni hatari sana Kadogoo kwasababu imelenga kupoteza jamii na si kuisadia.
Ni nzuri kwa mtu anayeuza vitabu lakini si nzuri kwa jamii husika
hangamkieni kura za Waislamu 2015 sio mbali la sivyo baada ya uchaguzi tutakuona ukija na makala mengine ya kuwasuta Waislamu kwa kuwauliza nilini CCM........................!
Mentor wako Mohamed anasema waislam wananong'onezana wamchague nani.Huyu ni mtu na degree zake na paper ulaya na marekani!!!!
Kwamba imefika mahali hatufikiri nani atatusaidia kuondokana na maradhi, ujinga na umasikini tunafikiria kuchagua mtu kwasababu ana kanzu kuubwa au msalaba mkuubwa!
Hapa ndipo nasema matunda ya uhuru hayatapatikana maana kama yangekuwa yamepatikana mawazo ya kijima kama haya yasingepewa nafasi.
Kadogoo labda hapa nichukue nafasi ya ''uwakili '' kwa Mwanakijiji.
Wakati wa Nyerere waislam walisema CCM haifa na hakukuwa na chaguo ila kuishi nayo kutokana na mfumo wa siasa wakati huo. Fair enough!Wakati wa Mwinyi waislam wakasema CCM safiii maana ndicho kimeleta uhuru wa nchi hii na wapinzani ni mamluki tu.
Wakati wa Mkapa wakaja akina CUF na siku ya Ijumaa ikawa ndiyo siku ya maandamano ya CUF na kila linalohusu CUF.
Kwamba sera zake zinatoa haki kwa wote. Haaki ! sawa!
Wakati wa Kikwete CCM ndicho chama kinacholeta mabadiliko na hivyo wakanong'ezana kuichagua.
Kwa mwendo huo, haihitaji mtaalam kujua kuwa Waislam na siasa ni vitu seasonal.
kwamba leo huyu mbaya kesho yule yule mzuri.
Mbaya wa wazee wa Mohamed ni CCM leo ndiye anapiga baragumu mbaya huyo huyo achaguliwe.
Kwanini inakuwa seasonal politics? Jibu ni rahisi sana, waislam wameacha kujitambua kama wao wamekabidhi akili zao kwa kikundi kidogo kuamua wao waweje na wafuate nini.
Kwa mtu mwenye akili haiwezekani ageuzwe mara kadhaa kama nyuzi ya kushonea nguo na asihoji, vipi leo mnasema hivi kesho mnasema vile kulikoni.
Nimalizie kwa kukujibu kuwa tatizo letu ni viongozi si dini. Ukimchagua mtu kwa jina umejidhalilisha na kudhalilisha utu wako.
Nani kasema Ukiwa John lazima uwe Mkristo? au ukiwa Yusuph lazima uwe mwislam.
Majina na imani ni vitu viwili tofauti, hivi ni imported things kutoka Ulaya na Uarabuni ndivyo vimefunga akili na macho yetu kupigana na ujinga maradhi na umasikini tumebaki tukidhani John au Hemedi waziri ataleta neema majumbani kwetu na wala siyo sisi kutafuta neema kwa fursa ya uhuru.