Uchochezi wa Mohamed Said na dhihaka kwa Wapigania Uhuru wa Tanganyika na Zanzibar


Yericko,
We matata sana bwana nani atakuweza.

Ahsante sana.
 
Ritz,
Sikuwezi ndugu yangu. Mkate wa ufuta kwa maziwa ya ngamia umo. Ugali wa Mtama kwa sato pia umo! Tende, halua,..., umo.

WildCard,

Kote huko nimepita mara nyingi nikifika Mwanza au Musoma lazima jamaa zangu wanitafutie sato "Njusi" wakuvuliwa na mshipi na ugali wa kuchanganya muhogo na mahindi hatari kaka.

Karibu pwani muhogo wa nazi na samaki mkunga...

Nasikia kambale akubali nazi...ha haa ha.
 
Ikiwa hii ndio historia fupi yako mwenyewe, pole. Hauwezi kusahau wala kuwasemehe watu kama huyo "Mnyasa" na Mwalimu. Wewe na Mzee Mohamed tunaelewa machungu yenu kwa hawa wazee.
 
huko kote ambako nyerere alithubutu kutia mguu kungekuwa na UKATOLIKI Asingethubutu kukanyaga abadan asilan...
THE BIG SHOW,

..WARENO wa Msumbiji walikuwa WAKATOLIKI na wanachama wa NATO.

..Eduardo Mondlane, Raisi wa kwanza wa Frelimo hakuwa Mkatoliki. Uria Simango, makamu wake, alikuwa mchungaji wa kanisa la Presbytarian.

..baada ya kifo cha Mondlane, Uria Simango aliongoza kwa kipindi kifupi kabla "hajapinduliwa" na Samora Machel. Inasemekana Samora, alikuwa Mkomunisti, asiyeamini mambo ya dini.

..Wako wanaodai kwamba Samora[asiyekuwa na dini] alikuwa akiungwa mkono na Nyerere/Tanzania ktk "mapinduzi" yake dhidi ya Uria Simango[mchungaji wa Presbytarian].

..sasa ilikuwaje Mwalimu Nyerere [Mkatoliki], awape msaada wa hali na mali Frelimo[chama cha Kikomunisti ]kupindua serikali ya Kireno ambao ni Wakatoliki? Kumbuka kwamba Kanisa Katoliki lilishautambua Ukomunisti kama adui wa Ukatoliki.

..kwa mtizamo wangu kujaribu kuhusisha kila alilofanya Mwalimu Nyerere na Ukatoli wake ni kutoitendea haki historia.

cc😡gombesugu, Jasusi, Mag3, Nguruvi3, Wickama, Mohamed Said, Kudi Shauri
 
Last edited by a moderator:

Mkuu hongera sana,

Sasa umefungua mjadala huru, ndio, sasa fikra lazima ziwe huru!

Tunataka kuchambua vema na kuona madhila ya fikra tengano na fikra za kidini!

Leo mapinduzi haya yaliyo na mkono wa Field Marshal au Mungu wa Afrika kama yeye alivyokuwa akipenda kuitwa yanatazamwa kama ni mapinduzi haramu kwamaana yakuwa yalikuwa ni dhidi ya uislamu na sio dhidi ya ukombozi wa Mzanzibar!

Ukimsoma kwenyemstari Mohamed Said, Dr Ghassany na hata Gumbesegu utagundua ndani ya mioyo yao wanakitu kinachowakwaza kila wakijaribu kulitaja jina Julius Nyerere na John Okello katika Mapinduzi ya Zanzibar!

Nimeeleza kwa kirefu katika makala yangu kwenye ukurasa wa nyuma hapo, nikijikita zaidi kuueleza utawala wa Okello baada ya mapinduzi na nimeeleza hatua za mapinzi zilimopita mpaka kuishia,

Lakini na zaidi nimeeleza hatua za ukabidhianaji wa madaraka kati ya Okello na Karume mkubwa!

Sasa tujiulize kwanini Okello anapingwa na kudhihakiwa na akina Ghassany, Mohamed na wengine ilihali ndie mkombozi halali wa wazanzibar?
 
Last edited by a moderator:
JokaKuu, tatizo la kubadili historia ili ku-fit some interest linawasumbua sana watu.
Big Show anasema Nyerere asingetia mguu mahali penye ukatoliki. Watu wamesahau kuwa mwaka 1965 Tanzania iliharibu uhusiano wake na UK kwasababu ya kumtambua Ian Smith wa Rhodesia.

Wanasahau kuwa Nyerere alisimama na akina Mugabe na Nkomo dhidi ya askofu Abel Muzorewa

Na muhimu, bado hawajibu swali ya kuwa kama interest ya Nyerere ilikuwa ni kuua Uislam Visiwani sasa kwanini waislam wa znz wanatukuza mapinduzi yale yale yaliyolenga kuua Uislam.!!

Ni katika spinning za historia kuna mtu kasema ZNZ ni nchi ya kiislam ili tu kujenga hoja kuwa Nyerere aliyekuwa si mwislam alivamia taifa la kiislam. Ubabaishaji huu ndio tunaambiwa tuuandikie vitabu! eti ni ilm, real!

Siku zote hoja za kubumba huwa zinayeyuka kama theluji kwa anayetumia fikra.
Kwa anayefyonza ilm zinaingia nzima nzima kama zilizvyotengenezwa maabara. Historia inatokea haitengenezwi maabara
 
Nguruvi3,

..nina mfano mwingine mdogo.

..mara nyingi tumekuwa tukisikia kwamba KANISA KATOLIKI lilihusika na mauaji ya kimbari ya RWANDA.

..sasa mnakumbuka jinsi Mwalimu Nyerere alivyong'aka kuhusu msimamo wa Tanzania wakati mauaji yale yakiendelea?

..binafsi sidhani kama Mwalimu Nyerere angekaa pembeni wakati mauaji yale yanaendelea Rwanda. He would have done something. Kama siyo kukemea kwa kauli nzito, basi Tanzania wangeingilia kijeshi.

..sasa tukubaliane na propaganda kwamba genocide ya Rwanda iliratibiwa na "Vetikan." Then kwanini Mwalimu Nyerere alikemea mradi wa Kanisa lake??
 
Last edited by a moderator:
Mzee Mohamed,

Abdu Std 10 alimwelekeza Mwalimu aliyekuwa na Masters ya Edinburgh mambo mangapi uliyoyasema na kuandika humu na kwingineko? Au umeanza kuwa "senile"? Au ulikuwa unamkweza Abdu?

Mzee MS; Hujaona maprofessor wamegombana wakapatanishwa na mzee wa kijijini? PhD ni kwamba umesomea fani FULANI SANA sio KWAMBA sasa UNAJUA yote. Usijishushe bwana. Binafsi nakuona una busara za kuongea na watu na hiyo hamna PhD inafundisha na kumpa mtu zaidi ya kipaji na experience. Wanasema Kul-haq.
 
Wewe jamaa unawababaikia sana wazungu halafu sijui kwa nini unawachukia Wazenji.

Ritz; Huwa najilinda sana na wewe. Kuna kitu ulijaribisha kufanya kwenye threads zako za nyuma dhidi yangu as wickama na kutokana nacho nilishaamua wewe ni miongoni mwa nitakaokuwa mwangalifu sana kuwajibu. Binafsi namlilia sana Zali. Pamoja na ukali wake tulibadilishana sana notes kiheshima na hakujaribisha kunifanyia hicho kitu ulichotaka wewe. Stay well.
 
[h=2]MAPINDUZI YA ZANZIBAR[/h]

Usiku wa tarehe 12 Januari 1964 kundi la watu 300 walikitwaa kisiwa cha Unguja wakiongozwa na mtu asiyekuwa maarufu kipindi hicho, aliyekuwa akiitwa John Okello, John Okello alikuwa akiishi Pemba ambako alitokea Uganda miaka michache tu. Ndani ya Zanzibar Okello alipata umaarufu kwa vijana majabari, ambao wengi katika wao walikuwa ni makuli na wachukuzi w meli zilizoingia na kutoka bandarini Zanzibar, kundi lake hili John Okello lilikutana kwa siri. Okello aliwapa matumaini ya mabadiliko watu wake hawa, wafuasi, ambao wakifanya kazi pamoja kwa muda mrefu, mara nyingine katika mazingira ya hatari, na tayari kufuata amri za kiongozi yeyote ambaye ataweza kuwalipa. Wao walikuwa waasi wanaotafuta makaazi.

Mchafuko wa kisiasa ulikuwa ukiongezeka ndani ya Zanzibar na Pemba tangu kifo cha Sultani Khalifa katika mwaka 1960. Sultani Khalifa alitawala Zanzibar kwa karibu ya miaka 50, tangu mwaka 1911. Baada ya udanganyifu mkubwa kwa majimbo ya uchaguzi na mseto katika chaguzi kuu mbili za mwaka 1961 vyama vikuu vilishindwa kujipatia wingi wa kura kwa kila kimoja. Waingereza waliondosha majeshi yao kikiwemo kikosi maalumu cha Kiarishi ambacho kilikuwa kimewekwa karibu na uwanja wa gofu na mpaka wa mji mkongwe mapema mwaka 1963. Wakati mfalme mpya, Jemshid akipandisha bendera ya Taifa huru la Zanzibar tarehe 12 Disemba 1963, aliadhimisha uondokaji wa Gavana wa kiingereza Zanzibar na mwisho wa ukoloni Zanzibar.
Uchaguzi mwingine uliofanyika mwishoni mwa mwaka 1963 ukiipa ushindi mdogo wa kura Muungano wa vyama viwili ZNP na (chama cha kizalendo Zanzibar) na ZPPP (Chama cha watu wa Pemba na Unguja). A.S.P (Chama cha Afro shirazi) kilikuwa kiwe kipo katika Serikali iliyo na chini ya nusu ya wabunge kwa mtindo wa bunge la Kiingereza na Sultani, akiwa kama ni mtawala tu lakini sio mtawala mwenye maamuzi ya mwisho. Taifa hili la Zanzibar ambalo lilikuwa mwanchana kamili wa Jumuia ya madola na mwanachana mpya wa Umoja wa Mataifa lilidumu kwa siku 33 tu.

Majadiliano makali ya kisiasa na maandamano yalikuwa ni matukio ya kawaida siku hizo. Nakumbuka nilikuwa naendesha baskeli kuelekea shuleni kupitia makundi ya watu yaliyokuwa yakiimba na kusifu majina mbalimbali ya viongozi wa kisiasa, huku yakivuka vizuizi vya barabara vilivyokuwa vikilindwa na askari wa kiingereza. Vikundi mbali bmali vilijadiliana juu ya mambo mbali mbali; mfano Haki dhini ya fursa, Wageni dhidi ya wenyeji wa zamani, Ubepari dhidi ya Ujamaa, Wafanyabiashara dhidi ya wamiliki ardhi, Waunguja dhidi ya Wapemba, Waasia dhidi ya pazia la nyuma la vita baridi na harakati za utaifa na kuondosha ukoloni ambazo zilikuwepo kipindi hiki ndani ya Afrika.

John Okello hakuwa na jawabu ya mambo haya nyeti, lakini alikuwa na kipawa cha kutambua kwamba vikundi hivi vinavyoshindana vinatoa nafasi nzuri kwa mtu wa harakati kama yeye Okello.
Hata hivyo, watu kama mia waliojizatiti wangaliwez kutwaa vituo muhimu vya kienyeji vya habari na kambi za Polisi. Mara tu baada ya vituo vya habari na Kambi za polisi pamoja na silaha kudhibitiwa na John Okelo, Ni nani katika visiwa angeweza kumshinda? Jee, wanasiasa wangeliungana na kumshutumu na kumpinga kwa vitendo vyake visivyo halali? Au kama alivyotaraji, wangeendelea kutoaminiana na kutuhumu kwamba kati yao ndio wanaomuunga mkono? Jee, wasingelitaka kukubaliana na yeye, haraka kabla mwengineo hajafanya hivyo? John Okello alichezesha dadu usiku huo wa mwezi wa Januari.

Viongozi wa A.S.P walifadhaishwa na matendo ya Okello (wengi wao, walikuwa hata hawapo visiwani wakati huo). Walikimbilia haraka kuwaunga mkono waasi. Mamia ya wafuasi wa vyama walipigwa na butwaa juu ya wale ambao walikuwa na shuku ya kukata fundo hilo gumu la majadaliano ya kidemokrasia na kukimbilia moja kwa moja kwenye utawala. Hawawalitafuta njia ya kuiandaa jamii kwenda sambamba na kanuni zao. Kanuni siku hizo zilikuwa ni ghali sana kama sarafu ya Marekani. Ubinadamu ulikuwa ni kitu adimu sana.

Baadhi ya viongozi wa ASP baada kuona kwamba serikali itakuwa haina udhibiti na uwezo kujilinda na kutokuwa na imani matokeo ya chaguzi huria zilizofanyika, viongozi hawalitafuta njia za haraka za kuhalalisha udhibiti yale ambayo yaliitwa sasa "Mapinduzi". Makundi ya watu wenye fujo yalikuwa huru. Sheria na amani zilikuwa hazipo katika mitaa ya Zanzibar.
Walimiliki ardhi na wafanya biashara waliburutwa kutoka majumbani na madukani mwao, uporaji na mauaji yalienea mji mkongwe mzima. Kwa kweli mji wenyewe uliporwa.

Waarabu na Waasia , waliokuwa wakiunga mkono vyama vyengine waliuliwa kwa makundi. Kwa usiku mmoja maisha ya watu yasiyovika yalipotea na siku nyengine baadae maelfu ya watu waliikimbia nchi pamoja na kila walichoweza kubeba.

John Okello mwenyewe alijipachika cheo cha Jemedari Mkuu akishirikiana na bataliani zake zenye fujo walianzisha utawala wa vitisho ndani ya visiwa vya Unguja na Pemba. John Okello alitangaza vitisho visivyo vya kawaida na ahadi ya kifo kwa wote watakaojaribu kumpinga yeye. John Okello aliamini alikuwa akipokea maelekezo /dokezo kutoka kwa Mungu na akionyesha uwezo usiokuwa wa kawaida kwa kutumia nambari, kwa mfano tarehe 13 Januari, 1964, alitangaza ujumbe ufuatao." Serikali sasa inaendeshwa na sisi… ikiwa mtakuwa wakaidi na kukataa kutii amri, Nitachukua hatua kali mara 88 zaidi ya hatua ninazozichukua hivi sasa" na "Na ikiwa yeyote atashidnwa kutii amri ya kutotoka nje ya nyumba kama walivyofanya wengine….sitokuwa na njia nyengine lakini kutumia silaha nzito. Sisi, ni jeshi lenye nguvu ya 99,099,000".

Vitisho vyake na uwezo wake wa kuvitekeleza viliwatia hofu raia, hasa makundi mbali mbali ya jamii zilizo ndogo. Tarehe 14 Januari, 1964 alitangaza maneno haya ya kufadhaisha" Huyu hapa ni Jemedari Mkuu wa Unguja na Pemba…Nafikiria kuelekea kijiji cha Mtendeni kukiangamiza ikiwa watu wa hapo hawatafuata amri. Baada ya dakika 40 nitawamaliza nyote hasa Wangazija", " na kwa vijana wote wa kiarabu wanaoishi Malindi; Nitapita Malindi nikiwa nimesheheni silaha ambazo mimi mwenyewe ndie nizijuazo. Nataka kuona kila mmoja abakie na chupi na kulala chini. Nataka kuwaona wao wanaimba... Baba wa Waafrika. Mungu Mbariki yeye na malengo yake na yale ya Jemedari Mkuu"

Wakati unyanyasaji uliposima jamii za tamaduni tofauti za Zanzibar zilikuwa zimeparaganyika. Taifa la chama kimoja lilitangazwa. Lakini bado jTaifa hili likihofia uwezekano wa kufufuka upinzani kutoka kwa wapinzani waliokimbia nchi. Wanamapinduzi hawa baadae walijihakikishia udhibiti zaidi baada ya kusaini mkataba wa muungano wa Tanganyika. Hii ingeruhusu maelfu ya marafiki wa kisiasa wa Tanganyika kuingilia kati upinzani wowote wa baadae katika visiwa hivi. Askari polisi wa Zanzibar walibadilishwa kwa askari polisi kutoka Tanganyika ambao ni watiifu kwa chama na pazia la siasa za utengano ziliwakumba wazanzibari ambazo zilitakiwa kudumu kwa zaidi ya miaka 20.

Leo hii siasa hizi za utengano hazipo tena, kumalizika kwa vita vya baridi na kuelekea kwa uchumi wa kisasa umeweza kuifungulia Zanzibar milango kwa ulimwengu wa nje. Uchaguzi wa vyama vingi ulifanyika mwaka 1995 na mwengine unatarajiwa kufanyika mwaka, 2000. Viongozi wa kweli na wenye kujali hali za watu wameibuka Tanzania na hii imewafanya wakimbizi waliokimbia wakati wa mapinduzi kurejea visiwani. Uvumilivu na amani wa watu wa aina tofauti, ambayo ni tabia ya maisha ya wazanzibari, sasa hivi unajitahidi kurejea katika mitaa ya mji mkongwe.
 
Wickama,

Ndugu yangu niwe radhi kama nimekukwaza kwa "Mipini" yangu tuendelee kusemezana huu mnakasha tu mie najifunza mengi kutoka kwenu.

Pamoja na ukali wake tulibadilishana sana notes kiheshima na hakujaribisha kunifanyia hicho kitu ulichotaka wewe. Stay well.
Chini hapa nakuwekea mpini wa Hamed Mazruy alivyokuwa anamjibu Joseph Mihangwa.
[h=2]Okello na Mapinduzi ya Zanzibar: Ukweli na uzushi[/h]
Licha ya mgeni kutoka Uganda, John Okello (aliyekaa katikati), kuonekana mstari wa mbele katika mapinduzi yaliyofanyika Zanzibar mwaka 1964, dhima na nguvu yake ilikuwa na nafasi gani katika uhalisia?

SINA tabia ya kusutana, kubishana au hata kujibizana na wasomaji wa makala zangu wenye kutoa maoni tofauti na yangu. Ninaamini kwamba kila mtu ana uhuru wa kutoa maoni yoyote ayatakayo hasa pale maoni hayo yanapokuwa ni ya ufafanuzi au uchanganuzi wa matukio ya kihistoria.
Kufanya ufafanuzi lakini ni tofauti na kuuelezea ukweli hasa ule ukweli wenye kuhusika na tendo ama vitendo fulani.
Nimekuwa nikisubiri kwa shauku kubwa hitimisho la makala za mwandishi mwenzangu wa Raia MwemaJoseph Mihangwa kumhusu John Okello.
Mfululizo huo wake wa makala zake kuhusu Okello na Mapinduzi ya Zanzibar ya mwaka 1964 ulikuwa ni majibu ya maandiko yangu juu ya mada ya Okello. Kwenye sahafu (safu) ya leo nataka kuyajibu baadhi ya yaliyomo kwenye majibu yake.
Kuna baadhi ya Wazanzibari wanaoona kwamba hakuna faida yoyote kujadili yaliyopita hasa sasa wakati wa mchakato wa Katiba mpya. Lakini wanakosea kwani tunaposonga mbele ni lazima tujue si tu hapa tulipo lakini pia tulikotoka. La sivyo tutajikuta tunajikwaa kila tunapopiga hatua.
Kuna tatizo kubwa kumtathmini Okello na dhima yake katika Mapinduzi ya Zanzibar. Sababu yake ni kuwako kwa simulizi zenye kukinzana kuyahusu Mapinduzi hayo na walioshiriki kwenye matukio yaliyoanzia Januari 12, mwaka 1964.
Migongano ya simulizi hizo yanamfanya mtu afikirie kwamba labda mapinduzi hayo yalifanywa na maruhani na kisha ndipo wanaadamu nao wakaingia. Ndio maana wengine chambilecho Sheikh Thabit Kombo, aliyekuwa Katibu Mkuu wa Afro-Shirazi Party (ASP), wanaifikiria historia ya Zanzibar yote kuwa ni uongo mtupu.
Lazima niseme hapa kwamba baadhi ya wanaotoa simulizi mbadala huwa hawana nia njema na Zanzibar. Simulizi zao huupotosha ukweli ili ziweze kuwa na mishiko. Mihangwa si miongoni mwao. Yeye ni mwandishi mahiri mwenye kuandika baada ya kuridhika kuwa amefanya uchunguzi wa kina kuhusu mada inayohusika.
Nimekuwa nikiyafuatilia maandishi yake kuhusu Zanzibar kwa muda mrefu na kwa maoni yangu huyu ni mwandishi mwenye kutupenda laisa kiasi sisi wazawa wa Zanzibar.
Lakini kwa vile yeye si mzaliwa wa Zanzibar na wala hajakuwako Visiwani (hasa Unguja) wakati wa Mapinduzi kwa kiwango kikubwa amekuwa akiwategemea wengine kwa masimulizi yake. Pingine hao ndio waliompotosha.
Sitothubutu kusema kwamba ubara wake umeugubika utaalamu wake kwa sababu hakuteleza kuyaeleza ya Zanzibar tu kama alivyomuelezea Othman Sharif kuwa alikuwa Mkomunisti wakati bwana huyo akijulikana kwa chuki zake dhidi ya wenye siasa za mrengo wa kushoto.
Mihangwa ameteleza kwa mengine pia. Kwa mfano, amemuelezea Idi Amin kuwa ni Mlangi, mtu wa kabila la Lango, ilhali tunajua kwamba alikuwa Mnubi wa kabila la Kakwa.
Tukiliacha hili la Okello, ambalo hakika Mihangwa halielewi, maandishi yake mengine kuhusu Zanzibar hayakirihishi kama ya wenzake wengi wa Bara. Mara kadha wa kadha kabla ya kuundwa kwa Serikali ya Umoja wa Kitaifa huko Zanzibar alikuwa akiwavua nguo watawala wa Visiwani kwa kufuata kisiri siri sera za kibaguzi zilizopitishwa na Mkutano Mkuu wa ASP mwaka 1973 kule Pemba.
Kwa kiwango Fulani Mihangwa amesaidia kuwaelimisha Wabara wenzake kuhusu mgongano wa maneno na vitendo vya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.
Juu ya hayo lazima tumkumbushe Mihangwa kwamba Che Guevara, mzawa wa Argentina, hakwenda Cuba kama mfanyakazi mhamiaji kama alivyokuwa Okello. Che alikuwa msomi aliyeshirikiana na akina Fidel Castro, Raul Castro, Camilo Cianfuegos na Wacuba wengine waliokuwa uhamishoni kwenda Cuba kwa dhamira thabiti ya kufanya Mapinduzi ya kuikomboa nchi hiyo kutokana na udikteta wa Batista.
Wala Che hakuwahi kujaribu kudai na kupora haki ya kutawala na uongozi kama alivyofanya Okello Zanzibar. Wacuba walimtunuku Che nyadhifa za uongozi kwenye serikali yao mpya kwa ridhaa yao na kwa heshima kubwa. Walimfanyia hayo kwa vile walitambua mchango wake adhimu kwenye Mapinduzi yao.
Kiashiria kingine cha mapenzi ya Wacuba kwa Che ni pale Wacuba walipokwenda Bolivia alikouawa Che na kulisaka kaburi lake na kisha kuirejesha Cuba maiti yake kwa mazishi ya kitaifa. Kumfananisha Che na Okello ni kumtukana Che bila ya kiasi.
Okello alionyesha chuki kubwa kwa Wazanzibari na kujisifu kwa kuwaua wengi mbali na kujaribu kupora hatamu za utawala kutoka viongozi wa ASP. Ukweli ni kwamba Okello anafaa kulinganishwa na jamaa yake Joseph Kony wa Lords Resistance Army ya kule Uganda na sio kumweka pamoja na Major Ernesto ‘Che' Guevara.
Laiti Okello angalikuwa hai basi yakini angelijiunga na LRA kwani ni muumini wa dini ya Ukristo uchwara wa kuendesha mauaji ya kikatili sawa na mhalifu Kony.
Okello mwenyewe alizidi kuipotosha historia pale alipolalama kuwa Waafrika wa Zanzibar wamemfukuza baada ya yeye kwenda Visiwani kuwasaidia kuwashinda Waarabu waliokuwa wakiwachinja. Hapo ndipo tatizo linapoanza na hicho ndicho kielelezo au kiashirio cha uzushi unaobatizwa kuwa ‘historia ya nyumbani'.
Kwenye makala yake ya mwisho juu ya kadhia ya Okello, Mihangwa amemalizia kwa kuibua maswali muhimu kuhusu uhasama mkubwa uliojitokeza upande wa baadhi ya wakuu wa ASP dhidi ya Makomredi, yaani wafuasi wa Abdulrahman Babu na chama cha Umma Party.
Hii ni mada nzito lakini lazima tuigusie. Hali ya kutoaminiana kati ya Makomredi na wakereketwa wa ASP imekuwepo wakati wote chini kwa chini tangu kilipoundwa chama cha Umma Party mwaka 1963.
Juu ya kuwepo hali hiyo ilibidi pia wakati ule pawepo na aina ya ushirikiano kati yao katika kukabiliana na wapinzani wao yaani vyama vya Zanzibar Nationalist Party na Zanzibar and Pemba Peoples' Party.
Haja hiyo ndiyo iliyopelekea pawepo umoja uliovishirikisha vyama vya ASP na Umma, vyama vya wafanyakazi pamoja na Jumuiya ya Wanafunzi.
Kiini cha kuwepo hali hiyo ya kutoaminiana ni ule msimamo wa itikadi ya kikabila wa takriban viongozi wote wa ASP wa kuwaepuka kisiasa Wazanzibari wenye asili ya kiarabu sembuse waliotokana na damu ya Hizbu. Mtazamo huu wa aina ya ‘kikaburu' ndio uliokuwa msimamo na unaendelea hivyo hadi leo kwa upande wa wahafidhina wa iliyokuwa ASP.
Wabara wasioitakia kheri Zanzibar wamekuwa wakiipalilia moto hali hii iliwaweze kuidhibiti Zanzibar kwa maslahi yao. Kwa hiyo dhana ya Umma Party ya kuyasuka Mapinduzi ili yawe na mtazamo wa kitabaka pekee badala ya ‘ugozi' (ubaguzi wa kikabila na wa rangi) ilisambaratishwa muda wote tangu kuanzia miaka ya mwanzo ya mwongo wa 1960 na akina Othman Sharif, Jamal Ramadhan Nasib na Mdungi Usi.
Baadaye usambaratishaji huo uliendelezwa na wanapinduzi kina Seif Bakari, Abdalla Said Natepe na kaumu yote ya ile ijulikanayo kama ‘Kamati ya Watu 14.' Hao ndio waliomshinikiza Sheikh Karume kutowashirikisha Makomredi kwenye uongozi wa nchi.
Siku zote walikuwa wakimtisha Mzee Karume kuwa Makomredi walikuwa na njama na jamaa zao Wakiarabu za kuutokomeza utawala wa Waafrika. Hatimaye walifaulu pale Karume alipowatimua kutoka kwenye serikali kina Badawi Qullateinna Ali Sultan na kubwa lao Babu kudondoshwa na Julius Nyerere.
Kuna siku ambapo Brigadia Yusuf Himidi aliwasikitia baadhi ya wafuasi wa Umma Party waliokuwa naye kwa kuwaambia: "Eh jamaa fitna nyingi zimepita kutugombanisha." Hakumtaja mtu lakini ilikuwa wazi kwamba mafatani walikuwa baadhi ya wahafidhina wa ASP.
Tatizo kubwa la Zanzibar ni kwa Wazanzibari kukubali kuhadaiwa na wanasiasa uchwara kuendelea kuwa wafungwa wa historia ya kisiasa iliyoigawa jamii katika makundi ya kikabila na kinasaba.
Jukumu linalotukabili sasa ni namna ya kutafuta njia za kuuyayusha urathi huu muovu unaoigawa jamii ya Wazanzibari na unaoutia sumu ufahamu au utambuzi wa pamoja wa Wazanzibari.
Okello alifurushwa Zanzibar kwa sababu alikuwa akileta matatizo. Alikuwa ni adha lakini hakuwa kitisho cha kisiasa. Angelikuwa ni kitisho cha kisiasa basi isingekuwa rahisi kumng'oa nchini kama alivyotolewa.
Wala si peke yake kati ya wageni waliokuwa wakifanya fujo aliyefukuzwa Zanzibar. Mwengine alikuwa Engine kutoka Kenya. Naye pia alitimuliwa baada ya kukamatwa huko Maruhubi, kwa amri ya Sheikh Karume, na kikundi cha Makomredi wakiongozwa na Ali Mshangama.
Mwengine aliyekuwa akiitwa Mfarinyaki alikamatwa Chwaka na Komredi Hamed Hilal aliyempeleka gerezani Kiinua Miguu. Amri za kukamatwa Mfarinyaki aliitoa Yusuf Himidi akiwa mkuu wa jeshi. Kwa nini hajawahusisha wanajeshi wengine na wapinduzi wa ASP, haijulikani. Labda Yusuf Himidi alikwishang'amua kwamba wenzake walikosa nidhamu, wakijihusisha zaidi na wizi wa ngawira, wakati Makomredi walikuwa na nidhamu ya hali ya juu.
Hatujui pia kwa nini Karume alihiyari kuwatumia Makomredi kuwatimua akina Okello, Engine na wapinduzi wengine waliokuwa si wenyeji wa Zanzibar.
Yumkini Karume aliamua kuwatumia Makomredi kumfukuza Okello badala ya kuwahusisha akina Said Washoto, Mohamed Abdalla Kaujore, Seif Bakari, Khamis Darwesh na wengine wa Kamati ya Watu 14 kwa sababu alihisi wangelisitasita na pengine kuibua mgogoro. Said Abdallah Natepe aliwahi kuhadithia kwamba waliwahi kumjadili Okello miongoni mwao na hata pakatolewa wazo la kumuua.
Sheikh Aboud Jumbe amekiri kwenye kitabu chake ‘The Part-nership' kuwa alikuwa hawajui na hakupata kuwaona baadhi ya waliokuwemo kwenye Kamati ya Watu 14, wakiwa pamoja na Okello.
Nakiri kwamba ni taabu kuamini ya kuwa Okello aliibuka ghafla Raha Leo kutoka halaiki ya watu waliokuwa wamekusanyika hapo. Lakini pia tuna uhakika kwamba Okello hakuwa na uwezo wala heshima anayobandikwa nayo na Mihangwa.
Hatusemi hivi kwa sababu Okello hakuwa Mzanzibari. Tunasema hivi kwa sababu huo ni ukweli huku tukikubali kwamba kuna haja ya kuiangalia upya nafasi yake Okello katika mchakato mzima wa maandalizi ya Mapinduzi.
Nimalizie kwa kukumbusha jingine. Nalo ni kwamba kadhia niliyoieleza ya kutimuliwa Okello kutoka Zanzibar haikuwa ya mwanzo ya kufukuzwa Okello. Mara ya kwanza alifukuziwa kutoka uwanja wa ndege wa Dar es Salaam na kusindikizwa hadi Nairobi na Oscar Kambona, aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Nje wa Tanganyika.
___________________________________________________________
 
Last edited by a moderator:
Hapana. Mimi siko hapa kushinda mdahalo.Mimi niko hapa kupinga upotoshaji wa makusudi au wa kutokijua kama vile ulivyomhusisha Kennedy na Nyerere na kifo cha Lumumba. Na for your information Martin Luther King, jr. was not Catholic. Hawa ni Mabaptists. Ni vitu vidogo kama hivi ambavyo siwezi kustahilimi vinapopotoshwa.
 
Ritz,

Nikukumbushe tu kuwa ukisoma maelezo hayo ya bwana Hamed Mazruy, picha ya mwanzo na mwisho unayoiona ni ileile ya Dr Ghassany na Mohamed Said,

Hayo yalikuwa ni mawazo yake, na sio mawazo ya wazanzibar!

Wazanzibar mpaka leo wanayaheshimu mapinduzi matukufu ya Okello,

Labda tuchukue fulsa hii kumfahamisha bwana Hamed Mazruy na wengine kuwa Oscar Kambona hakumfukuza Okello hadi uwanja wa ndege mjini Dar es Salaam kama inavyosomeka,

Hii ni chuki tena chuki ya wale ambao hawakuupenda utawala wa mkono wa chuma wa Okello katika nchi mpya!
 

Nyerere Against Islam in Zanzibar and Tanganyika
"Without any question, the manner and the implications of the union between Tanganyika and Zanzibar is the most misunderstood aspect of Tanzania's political development. It may not matter very much when foreigners get confused, but unfortunately there are many times when Tanzanians themselves appear to misunderstand it."
Tanzanian who knows "the manner and the implications of the union" after British colonialism in East Africa.
Former Tanzanian President Julius Nyerere. - Dar es Salaam Government Printer, July 1970. p. 3.

When the former Tanzanian President Julius Kambarage Nyerere made the above address to his National Assembly that "the union between Zanzibar and Tanganyika is the most misunderstood aspects of Tanzanian's political development" proved that he is the only Tanzanian who knows "the manner and the implications of the union" after British colonialism in East Africa.

During the British colonialism, Zanzibar was the only intellectual center for Islamization of East African countries under the Zanzibar Sultanate. The Gofu and the Barza Mosques allowed students from the East African countries for the Islamic education. The Zanzibar Muslim Academy also offered the greatest hope for the vibrancy of Islam in East Africa. Nyerere, a devout Catholic saw that the Islamic Zanzibar state, a threat to Christianity. He masterminded a clandestine movement for the so called Zanzibar Revolution under the leadership of John Okello, a radical Christian from Uganda. It was not only a prelude to the creation of Tanzania, but a continuation of crusade against Islam and extension of Christian colonialism.
Source: Mwalimu Nyerere - Articles, Transcripts and Legacies | Julius Nyerere; Life Times Legacy :A S-omg::usa:
 
Ndugu yangu Gombesugu;
Baada ya Salaam nakupa pole kwa mashaka haya uliyoyaongea ya kule zenj na kwenye familia yako. Binafsi kama ulifuatilia sana haya mazungumzo niliyakwepa mno tangu awali. Nilifanya hivyo kwa vile unapokuwa na issue ambayo watu 13000 wameuliwa kwa sababu ya kabila/rangi yao lazima uwe sensitive na feelings za wenzako. Mada hii aliichokonoa sana ZALI. Lakini kama unakumbuka, ni kwamba wengi tulimwambia na-afungue thread nzima ya issue hii ikashindikana. Na always nilikuta quotes ananilenga sana juu ya suala la Zenj (Only God knows why).

Binafsi sina tatizo na Zenj. nimesoma sana vitabu vya scholars wa Zenj wakiwamo wakina Marhum Ali Muhsin na mwingine naye Aliyeandika kitabu kizuri sana juu ya zenj.....kinyang'iro. Na kutokana na details za what I read ndio maana sikutaka kabisa kuvutwa kwenye hii debate. Na ndio maana nimesema time and again ikitokea a voting opportunity nita-vote hawa mabwana wawe na kwao. I just feel that way. Majirani wema ni wale wenye roho zilizotuama. Umesema kweli sana kuwa hawa tunaowaita waarabu huku kwetu pia huwa wanapata shida sana wakiwa na wenzao wa arabuni kwa vile wenzao wanaita waswahili. Nina ndugu yangu hakuamini macho/masikio yake akiwa chuoni uingereza(UK) alipojikuta analazimika kumtuliza machozi na kumpa-company Mzungu wa south Africa (kaburu) kwa vile vijana wa UK walimwakia moto huyo kaburu kuwa "you bloody African". Mwisho wa siku kaburu kamkimbilia jamaa yangu kuwa hawa jamaa wabaguzi sana 'am suffering a lot'. Na ndio maana tangu awali nimesema jamani ardhi hii sii yetu, twapita. Isiwe kigezo cha kujifanya ni watukufu kutokana na ulipojaliwa kuishi.

Gombesugu, mada hii haikupaswa kuwa ya kuwajengea watu hisia za loss za familia zao. Hapa watu walitakiwa kuwa wakweli kuwa tukio Fulani lilitokea na siku hiyo Gombesugu ndiyo alikuwa in-charge. Kama vile Siku Fulani palifanywa harusi. Na MC alikuwa Fulani. Tuna tatizo la kukubali nani alikuwa MC. Kuna mawazo hapa kuwa kamati za harusi ndio zilikuwa MC wala sio Gombesugu.

Huko kwenye hizo CIA reports tumepelekwa kwa lazima. Huko kwenye video za Mapinduzi za kina Okello tumelazimishwa Gombesugu. Believe me, sio hobby. Kumbe ufanyeje....wakati sisi hatuna wazee wetu kila mahali? Hii ni forum inayohitaji ushahidi. Utautoa wapi kama sio Www.com: The Best Search Links on the Net Hakuna anayekataa MAELEZO YA MZEE MS na Dr Ghassany. Hawa ni hazina ya mengi. Mwenyezi Mungu awalipe ujira mwema. Lakini binadamu huwezi jua YOTE. Huwezi kupuuza pia wengine wanasemaje au wameandika nini ukashika moja tuu. Glass ikijaa maji nusu ni kweli ina hewa nusu pia. Usikatae.

Video inaonyesha bunduki kongwe kama za magereza (enzi hizo) na zingine zina namba kwenye vitako (tunachosema ni kuwa hizi bunduki ni chakavu jamani haziwezi kuwa zile alizotaja Dr. Ghassany au hata hao CIA wenyewe kuwa kuna silaha zilitoka Algeria. Sababu ni kuwa Huwezi kuiuzia nchi nyingine silaha za hivyo tena zina namba kwenye vitako na kwa madhumuni yaliyotajwa. Tumeambiiwa zilinunuliwa, sio zawadi). Sisi twasema hizi ni zile tunazoambiwa ziliporwa baada ya wanaume kuzipiga kavukavu kituo cha polisi. Za Algeria (hizo mpya na nzuri) zilikuja baadae wakati tayari Zenj kuna Field Marshall. Mashaka yapo hapo ndugu yangu.


Pole kwa mashaka ya 1964 Gombesugu. Pole sana. Na kwa wengine pia. Haya yanawakuta wengi. La msingi wape hao unaokutana nao moyo kuwa waishi maisha yao kadri wanavyoweza na wamshukuru M\Mungu kwa zawadi ya kuwa hai na familia zao. Hii ni mitihani ya maisha na Mwenyezi Mungu ndiye anayejua yaliyo mbele.
 
Mkuu sikajiji

Kwa mtazamo wa wewe unataka kuniambia kuwa Mwalimu Nyerere aliinjinia mapinduzi yale kwalengo la kupambana na uislamu?
 
Mkuu Jasusi, njia rahisi ya kukubaliana na upotoshaji ni kusema ''andikeni vitabu''.
Kwamba watu wauache upotoshaji uendelee kwasababu kusema huu ni upotoshaji kuna haribu mission.

Watu wanaamini kuwa mapinduzi ya ZNZ yalipandikizwa na Nyerere kwa kutumia wamakonde wa Kipumbwi. Well, kama ni hivyo kwanini wzn wanaofahamu kuwa hizo zilikuwa njama za kuua Uislam wameuyakubali na kuyatukuza.

Kuna mahali tumeuliza Nyerere aliunga mkono Palestina na Polisario kwa misingi gani? Hakuna jibu kwasababu jibu ni kisu chenye ncha mbili kitakata nyuma na mbele. Mjadala umeishia hapo! haya ndiyo matatizo ya historia ya maabara.

Huko nyuma kuna aliyeleta hoja ya Biafra, Nigeria kuwa Nyerere aliunga mkono wakatoliki. Tukauliza hivi karibuni Tanzania imeunga mkono Sudan Kujitenga, je hapo napo inakuwaje! Nyerere hayupo. Hoja za maabara zinakufa.

Tumeambiwa mahali penye ukristo Nyerere hatii mguu, tukauliza vipi Msumbiji, Zimbabwe na SA nako huko wapo wa aina gani! hoja ikafia ndani ya test tube huko maabara.

Tukaambiwa Nyerere aliingilia mambo ya Seychelles kumsaidia Albert Rene wakati wa jaribio la Mapinduzi.
Tukauliza na Comoro nako nani amepeleka askari kumsaidia Zambi, hoja za kufinyanga zikafa.

Kuna upotoshaji kuhusu mgogoro wa Znz, kwa kuanzia tunaambiwa ZNZ ni taifa la kiislam. Inawezekana sielewi mahali naomba msaada, hivi zanzibar ni taifa la kiislam au taifa lililokuwa na waislam wengi. Naomba ilm

Mkuu tukikaa kimya kama ilivyokuwa takribani miongo miwili iliyopita tutakuwa hatuwatendei haki vijana wanaofyonza ilm, tutakuwa tumewatelekeza katika makaro wakifyonza maji ya uani. No way!
 

Mkuu wa Chuo,
Mishikaki unaweza kutumiwa lakini nyama ni HALAL! wala?
 

Yericko,

Naona tunatoka nje ya mada au Hili la uchochezi limekwisha? Tuanze mambo ya Znz.

Kama ni hivyo ni vizuri tuanze uzi huo maalum ili tutoe darsa kwani wengine tunajua mengi sana kuhusu hilo.

 

Yericko,
Kama Okello ni baba wa Zanzibar na Tanganyika baba ake nani? mwaka huu tutasikia mengi! upinzani dhidi ya wapigania uhuru wa Tanganyika sasa umehamia Zanzibar! issue ni kupinga tu! yaani kuna watu nchi hii wamejazwa kupinga, kuandamana, kugoma na kufanya fujo mitaani, ndani ya bunge na sasa JF!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…