Uchochezi wa Mohamed Said na dhihaka kwa Wapigania Uhuru wa Tanganyika na Zanzibar



Gombesugu;
Sijawahi kuleta paper ya Dr Ghassany hapa ikimpinga Sheikh Ameir. Tafadhali soma upya. Ni paper ya Dr. Issa Ziddy. Nayo pia haikuwa ikimpinga Sheikh. Dr Ziddy Siye huyu mwandishi wa kitabu cha Kwaheri uhuru........ Tafadhali kuwa mwangalifu kwa sababu Dr Ghassany awezakuwa miongoni mwa readers wa JF na nisingependa kuonekana nafanya upotoshaji wa kazi kubwa aliyoifanya au kuonekana kuwa namkosea heshima kinyume na alivyoandika. Hata hiyo paper unayosema Tafadhali soma contents zilizowekwa hapo hakuna mahali Dr Ziddy anapingana na Sheikh. Ile paper ilitumika kuonyesha mtafaruku wa kisiasa wakati ule kama alivyoutaja mwenyewe daktari na ambao ulimkumba sheikh Ameir. Please revisit tena na tena ile POST SIYO Dr Ghassany na uwe mwangalifu sana. Japo naona umeshalamba LIKE. Wote hawa huenda wanasoma hizi threads. Hiyo paper ni hiyo hapo.

SHAYKH ˘ASAN B. ‘AMAYR AL-SHIRAZˆ
(1880-1979)ISSA ZIDDY
 

zomba
I know why you laughed. When you saw "genes" you thought I was talking about "genie"- the imaginary spirit popular in Arabian folklore (and your religion).
I would agree that I am dull in general knowledge if that knowledge is about those funny and imaginary creatures. One thing I know that I know and I know that you don't know is "Genetics". Now this is science. Genetics is learnt in classes and not from such novels as that of Moh said (understandably it is a history text book to you) nor from coffee joints in the streets. Ever heard of such terms as heterosis and inbreeding depression, zomba?
 
Last edited by a moderator:
Kadogoo,
Hili suala tulishalijadilia kwa kirefu sana hapa JF. Kwanza si kweli kwamba Nyerere alipeleka majeshi yetu Biafra kuwasaidia Waibo. Hilo la kwanza, pili, ni dhana potofu kuwa uamuzi wa Tanzania kuitambua Biafra ulikuwa na misingi ya kidini. Kilichotokea, kwa kifupi tu ni kwamba baada ya mapinduzi ya Tafawa Balewa, yaliyofanywa na vijana wa kijeshi akiwemo Gowon, ambaye si Muibo, na Ojukwu, Muibo, ndugu zetu wa kaskazini, Wahausa ambao majority ni waislamu, wakadhani kuwa ni Waibo ambao wamempindua Mhausa mwenzao. Walianzisha machinjo ya kulipiza kisasi kwa kila Muibo aliyekuwa katika jimbo lao. Si mwenye duka, mwenye teksi, mwalimu wa darasani, mauaji kama yale yaliyotokea Rwanda 1994 yalifanyika Nigeria. Waibo waliosalimika wakakimbilia kwao, na kwa kuwa hawakuliamini jeshi linaloongozwa na Wahausa, wauaji wao, wakaamua kujitenga. Mwezi Februari 1967, Mwalimu Nyerere alifanya ziara Afrika magharibi ambako alikutana na rais wa Ivory Coast, na pia alikutana na Gowon. Akamwambia Gowon kuwa lazima ajadiliane na Ojukwu wapate muafaka katika mauaji yanayoendelea Nigeria. Gowon alikataa akasema kuwa hawezi kujadiliana na "junior" wake. Arrogance. Tanzania, Zambia,Ivory Coast na nchi nyingine nimeisahau zikaamua kuitambua Biafra. Lengo lilikuwa ni kusimamisha mauaji yaliyokuwa yanaendelea dhidi ya Waibo. Lakini kwa sababu ya international politics, Uingereza iliunga mkono serikali ya Gowon na hatimaye walishinda vita. Lakini the genocide was real na kama wewe ni mtu unayependa kupekua mabuku nakushauri usome kitabu "The International Politics of the NIgerian Civil War, 1967-1970." Kimeandikwa na John J. Stremlau. Nakumbuka siku tulipotangaza kuitambua Biafra ilikuwa ni easter na jumapili Mwalimu Nyerere alikuja nyumbani kwa easter dinner. Alifuatana na Mnanka na Philemon Mgaya. Wakati Mnanka anampongeza kwa uamuzi huo Mwalimu alikuwa akijiuliza loudly, "will Africa understand?" Kwa sababu aliiona hiyo contradiction ya kuunga mkono kujitenga kwa Biafra wakati huo huo unahubiri umoja wa Afrika. Will Africa understand?
 

Nguruvi and others;
Vitabu ni njia nzuri na kudumu ya kupingana na mada. Tatizo lake huwa ni speed na kitu wanaita REACH. Wasomaji wa vitabu sio wengi sana kama watu wanavyodhani. Audience ipo kwenye Internet. Na ndio maana kila mwenye lake anawahi kwenye websites. Kwa hiyo, one weapon ya kupambana na kuiepushia jamii masuala kama yale ya Arusha na yaliyomfika yule katibu wa Bakwata huko huko ni kupambana nazo huko huko kwenye DOTCOM. kumsubiri publisher wa vitabu, sawa, lakini kama 90% ya vijana wapo kwenye screen ya computer screens na wao ndio target wa cyber campaigns itakuwa kosa baya kuto-engage in their rescue na ku-save innocent lives. Nimeambiwa na rafiki yangu mmoja wa Mwanza mjini kuwa baadhi ya makanisa sasa hivi yanajenga UZIO na kuweka aina ya kufuatilia nani kaja kwenye compound yao!!!!!
 

Surely you do not have enough intellect to understand Genetics as science let alone the Bible verses. So I am not surprised by the trash (your reply).
To help you this time and this time only, just to clear you hazy understanding I'll tell you this: In christianity, even an arab halfcaste born at kariakoo, can become a CHILD of GOD as long as he accepts and abides by the teaching of Jesus Christ. Issues of incest are not applicable and are irrelavant because the "childhood" in this case is spiritual.

Let us not drift much on these issues. I know you are short tempered and you may soon start insulting me and others. BTW, you have been away for a while from this thread, why dont you bring some positive contributions to the issue at hand? We are discussing "uchochezi..."
 
Nguruvi, Joka Kuu, Mag, NanRen Mwanakijiji etc; Nilisahau kutaja kitu kwenye hiyo point ya vitabu. Ni kwamba kwa sasa whatever you post kwenye forum kama hizi JF huwa eventually kinakuwa available kwenye Global Internet Search Engines. Kwa hiyo unapo-post kitu kifanyie maandalizi. Ni gharama nafuu sana ya kupeleka arguments zako to a global audience. Bei ya kitabu kimoja, kwa kijana ni kwamba ka-surf internet kama hizi za voda, tigo, airtel kwa nearly nusu mwaka/mwaka. Kwa maana hio ni muhimu sana unapokuwa unafanya efforts kama hizi hapa kwanza Ku-post kitu ambacho ni kweli au ambacho kina reference wanayoweza kuifuatilia hao audience wako na kuamini kuwa hukusema uongo. Pili ni vizuri kabisa kuonyesha mpaka wa mawazo yako wewe kama wewe na maneno ya chanzo chako. Hii itakulinda in-case ulielewa vibaya. tatu ni kuwa mwepesi kukiri jambo pale ukweli unapojidhihirisha na pengine ilikuwa kinyume na position yako ya awali, inajenga more respect kwa wanao kusoma after all you are human kama wao ila hawatatilia mashaka your ethical values. Lakini at all costs usiingie kwenye mtego wa kutusi mtu/watu across the internet. Unaondoa uhalali wa kusikilizwa na watu wengi wema wa jinsia zote lakini huwa ni un-decided audience.

Kwa hiyo wakati tunahimizwa kuandika vitabu, ni muhimu sana kujua kuwa madhara makubwa ni kwenye hili dirisha la internet. Na ndio maana linafuatwa hata na wabaya. Bahati nzuri hili nalo halibagui na halingoji publishers. Ndimo pa kupambana kwanza humu. Mbabaishaji mwisho wa siku atajulikana tuu na atajiondoa na wengine watasalimika na sumu zake. Ila sio kazi ya siku moja. Inahitaji resilience. Hata anayeharibu jambo wakati mwingine huwa seriously anadhani analijenga. Mpaka matukio yamwambie hapana.
 
JOKAKUU,Kama ndio hivyo, inakuaje Kanisa Katoliki wanataka kumtawaza Julius kama Mwenyeheri Mtakatifu? ina maana Kanisa halina taarifa za Nyerere kuipiga vita? haingii akili Kanisa limtawaze Mkomunisti!
Kadogoo,

..naomba nianze na suala la Biafra kwanza.

..kwa mtizamo wangu Nigeria kulikuwa na vita ya kikabila, siyo vita ya kidini. sidhani kama ilikuwa vita baina ya Wakristo vs Waislamu, kwasababu huo upande unaodaiwa kuwa na Waislamu ulikuwa na wanajeshi Wakristo. Olusegun Obasanjo, Mkristo, alikuwa upande wa federal gov of Nigeria.

..kwa hiyo Nyerere alikwenda kusaidia Waibo, waliokuwa wakichinjwa na Wanigeria wenzao.

..mimi ningekushauri utafute hotuba iliyotolewa na C.Y.Mgonja[waziri wa nchi ofisi ya Raisi ] kuelezea kwanini Tanzania iliamua kuitambua Biafra. naamini kabisa kama uko open minded utakubaliana na hoja zilizotolewa na serikali ya Tanzania.

..Hata mimi nashangazwa sana na hii process ya kumfanya Mwalimu Nyerere mwenye heri na baadaye Mtakatifu. Mimi namuelewa zaidi Mwalimu kama mwanasiasa, yes he was a devout Catholic, lakini sidhani kama alifanya mambo yoyote yale ya "kiroho" au "kitume" kustahili ngazi ya wenyeheri and eventually utakatifu.

..Lakini Mwalimu amepewa sifa nyingi sana, na wakati mwingine hata yeye mwenyewe alikuwa anashangaa. Kuna kipindi India walimpa nishani ya amani na unaharakati wa kuzuia silaha za nuklia[naomba kusahihishwa kama kuna makosa]. Mwalimu katika hotuba ya kushukuru alisema bayana kwamba ameshangaa yeye kupewa nishani hiyo ukizingatia kwamba siyo mara moja ambapo aliunga mkono mapambano ya silaha.

..Umeuliza kuhusu mauaji ya Zanzibar na Mwembechai kama yangeweza kutokea wakati wa Mwalimu. Kwa mtizamo wangu naweza kusema yasingeweza kutokea. Nasema hivyo kwasababu Mwalimu na vyombo vyake vya usalama walikuwa na tabia ya "kunyakua" vinara wa machafuko kabla hawajaleta madhara kwa jamii nzima.

..Mwalimu pia alikuwa haogopi kujibu shutuma zozote zile dhidi ya serikali yake. Kwa mfano, hawa jamaa wanaohubiri mfumo Kristo wasingeachiwa wakatamba nchi nzima kwa miaka kadhaa bila kujibiwa na Mwalimu mwenyewe, au kutiwa kizuizini.

..Mwisho, nadhani Mwalimu alichukia dhuluma kwa namna ya kipekee kabisa. Kutokana na msimamo huo ndiyo maana unaona alikuwa radhi kwenda kinyume na OAU charter kuwatetea Waibo wa Biafra. Ndiyo maana akakubali Tanzania ikose misaada ya kiuchumi toka Uingereza kwa msimamo wetu wa kuwatetea wananchi wa Zimbabwe. Kwa kuchukia dhuluma hakuogopa kutoa msaada wa kijeshi kwa Frelimo waliokuwa wakipambana na Wareno, wanachama wa NATO.

cc: Jasusi, Kudi Shauri, gombesugu, Ritz, Wickama
 
Last edited by a moderator:
Hewaaaa! tawire,tawire baba! muchas gracius

Sitii neno zaidi, umenikumbusha tu akina Nnandi Azikiwe, Chief Obafemi Awolowo, Gen Yakub Gowon,Ironsi, Murtalla Mohomed, Olusegunu Obasanjo, Othman Shehu Shagari, Muhamad Buhari n.k.
Ukiteremka Lagos uwanja wa Murtalla ni kwa heshima yake, sijui ule wa Ibadan waitwaje. Sina ujuzi na hilo.

Hiyo ndiyo habari ya Biafra. Kwa wale wa Musoma, eneo la Kamunyonge kuna National housing za zamani kidogo zilizoungana na soko la Matumbi. Eneo hilo lote linajulikana kama Kamunyonge, lakini wakati nyumba zile zinahamiwa ndio kiswa cha Biafra kilikuwa moto ndio maana pakaitwa Biafra. Kamunyonge ilikuwa eneo la mashine ya maji kuelekea Buhari hadi eneo la mlima wenye mawe mawili yaliyobebana.

Nyumba zile za biafra akiishi pia mzee Kirigini aliyekuwa waziri. Mzee Herman Kirigin baba yake ndiye alikuwa mwalimu wa Nyerere. Huyu mzee mkewe akiwa Mwalimu na mwanae ndiyo mbunge Rose Kirigini.

Eneo hilo pia aliishi mbunge wa zamani Abel Mwanga Kyagunya. Mwanga aliwahi kuwa naibu waziri wa elimu.
Huyu akiwa msomi na aliwahi kutoa kitabu cha english cha kufundishia shule za msingi kama sikosei.

Maeneo hayo akikaa marehemu mzee Mutaragara Chirangi, mzee aliyetoa mchango mkubwa sana wa maendeleo ya michezo na jamii kwa ujumla katika mji wa Musoma

Tuendelee na mnakasha! nikiwakumbuka wazee wangu.
 
JokaKuu,
Nadhani kijana alipaswa kwanza asome historia ya Uhuru wa Nigeria, mgawanyo wa makabila ambayo ni kama 300 lakini makubwa ni Igbo, Hausa-Fulani na Yoruba. Halafu aangalie mgawanyiko wa nchi kwa maeneo kama north, sothwest na Southern region

Baada ya hapo aangalie mgawanyo wa madaraka na mauaji ya viongozi. Kisha aulize kama Biafra ilikuwa suala la kidini au kikabila.

Hii ni kama hadithi ya znz ambayo imepotoshwa na sasa mapinduzi yanachukua mkondo wa kidini zaidi ya uhalisia wa kile kilichotokea. Wapo wanaosema znz ilikuwa shwari kabla ya mapinduzi na muungano. Watu hawa wanasahau kuwa katika miaka hasa ya 1957 siasa za znz zilikuwa moto sana kuliko inavyodhaniwa.

Siasa hizo zilichagizwa sana na urangi na wala si dini kwasababu wengi wao walikuwa ni waislam na hivyo hawakuwa na sababu ya kuchukiana. Chuki iliyokuwepo ni ile ya rangi ambayo hadi sasa bado ipo.
Unaposikia akina Karume wanaitwa Wanyasa na akina Maalim Sultan ujue hapo hakuna Uislam bali urangi.

Suala la Nigeria limekuwa miscontrued ku-fit political interest than the fact on the ground. Hili ndilo tunalosema kuwa likiachiwa ipo siku tutaambiwa kuwa Dar ilikuwa nchi imeharibiwa na fulani.

Nina wasi wasi kama kijana ametumbukiza mrija kufyonza ilim katika kibuyu sahihi.
Pengine mrija ume slip na kuingia katika karo. Hata hivyo dhima yetu ni kuwasaidia

Kwa sisi JF ilm ni dhamana akiita mtu unampa.
 

Tupe Ilm kwa nini Kanisa Katoliki limemtangaza Nyerere mwenye heri halafu baadae kuwa Mtakatifu Nyerere.

Sisi tunapata Ilm kutoka kwenu magwiji wa historia.

Kwa faida ya wanajamvi tupe Ilm.
 

Ever read about "god" or rather "son of God" being possessed, and its in the Bible?

Nanren, we learn about Genetics in Madrassah, pre-school, we are much much far better learned in the matter more than you can contemplate.

Enjoy:


DNA AND THE BEGINNING OF GENETIC HISTORY
The term DNA is an abbreviation of the genetic material in living things. The beginning of the science of genetics dates back to genetic laws drawn up by the scientist Mendel in 1865. The date, a turning point in the history of science, is referred to in verse 65 of Surat al-Kahf, or verse 18:65.
When the appearance of the letters D-N-A (Dal-Nun-Alif in Arabic) side by side in places in the Qur'an is examined, they appear most frequently in verse 65 of Surat al-Kahf. The letters D-N-A appear side by side three times in this verse, in a most incomparable manner. In no other verse of the Qur'an do the letters "DNA" appear consecutively so often.

The number of this exceptional verse in which the term DNA appears so strikingly is 18:65. These numbers are an expression of the date when the science of genetics began. This cannot be regarded as a coincidence. Because only in verse 18:65 of the Qur'an do the letters "DNA" appear three times consecutively. This is something miraculous, because the scientific world only came up with the name DNA (Deoxyribo Nucleic Acid) comparatively recently.
In Surat al-Kahf, which refers to DNA and the year 1865 when the science of genetics began, DNA is repeated 7 times, as is RNA (the Arabic letters Ra-Nun-Alif). Like DNA, the RNA molecule is a molecule giving rise to genetic structure. For that reason, the appearance of DNA and RNA an equal number of times in this Surat is further proof that these molecules were referred to in the Qur'an hundreds of years ago. (Allah knows the truth.)

Read more: Miracles of the Qur'an - Modern Science Reveals New Miracles of the Qur'an
 
Tupe Ilm kwa nini Kanisa Katoliki limemtangaza Nyerere mwenye heri halafu baadae kuwa Mtakatifu Nyerere.

Sisi tunapata Ilm kutoka kwenu magwiji wa historia.

Kwa faida ya wanajamvi tupe Ilm.

Katika hili nitakujibu kwakifupi tu ndugu yangu,

Ili kanisa likufanye mwenye heri na kisha mtakatifu ni lazima ufuzu vigezo vyalo!

Vigezo ni vingi sana lakini nakupa viwili tu muhimu:


1) Ni yule aliyeitumikia jamii ya dunia kwa kujitolea kwa hali na mali,

2) Ni yule aliyeamini mafundisho yalo na kuenenda sawasawa nalo, (mtiifu)

Katika hayo lakwanza huzingatiwa zaidi!
 
JOKAKUU,Kama ndio hivyo, inakuaje Kanisa Katoliki wanataka kumtawaza Julius kama Mwenyeheri Mtakatifu? ina maana Kanisa halina taarifa za Nyerere kuipiga vita? haingii akili Kanisa limtawaze Mkomunisti!

Kadogoo; Nitachangia kidogo hapa japo ni mada ambayo nadhani wenzangu wa imani husika wana mwanga mzuri zaidi. Kwa Kanisa katoliki mtu anapopewa utakatifu inakarabia kwa kiasi na heshima waislamu wanawayowapa Maswahaba. Katika ukatoliki kupata utakatifu huwa inapitia mlolongo mwingi sana wa kuchunguza kama kweli aliyependekezwa anastahili (kuna kesi hadi 25-30 years mtu hajapata). Wakati mwingine hapati kabisa. Lakini lazima apendekezwe na kanisa la nchini kwake kasha cheo kinatoka kwa papa. Sasa lazima ujue kuwa kwa kanisa lolote la kikatoliki duniani ni heshima ya kipekee kuwa na muumini katika eneo lake akapata cheo hicho. Sawa na shule iliyotoa watoto wa DIV 1 tupu. Hii heshima wakati mwingine inashindaniwa na makanisa. Nani asiyetaka sifa??? Angalau wapate mtu wa daraja hilo kwa vile hii inawapandisha daraja angalau kisaikolojia mbele ya umma wa kikatoliki duniani. Huenda Uganda wale vijana waliochomwa moto kwa kuingia ukiristo wameshapendekezwa pia (sina uhakika)

Sasa unapokuja kwenye mchango wa mtu kama Julius tayari unaona wanajamvi ambao ni pengine wakiristo wakisita kuwa hata wao wanashangaa kidogo. Lakini kwa kanisa kumbuka Julius aliandika vitabu vya sala za kikatoliki hadi kizanaki sio mchango mdogo. Huwezi jua vimeingiza wangapi kwenye dhehebu hilo. Pia japo aliamua kuwa mjamaa na alidumu na imani yake hakuwa Mkomunisti kama ulivyodanganywa. Siku zote aliwashangaa wakomunisti.

Mengine ni ya binafsi, hatuwezi kujua michango mingine toka kwake kwa kanisa lake. Na hiyo alikuwa anafanya wajibu wake kama Mkatoliki. Kwa hiyo kwa vile ni utaratibu wa madhehebu hayo ni bora kubakia na imani kuwa wanaendesha masuala haya kama taratibu zao zinavyowataka.

Hatari ni kuwa wapo wanaotaka kuweka sumu kuwa huenda process hiyo ya kumfanya mwenye kheri hadi mtakatifu ni kwa vile Julius alihujumu au kuua waislamu/uislamu hapa TZ na East Africa. Kama kigezo ni mauaji ya waislamu au kuwahujumu tuu, basi wale Wareno wote waliopiga makombora misikiti ya Kilwa na kuwauwa waislamu pale Kilwa wangefanywa watakatifu.
 

Enjoy the free darsah, you might open your eyes a bit, if you want the truth:
[video=youtube_share;NGinvU_b_ug]http://youtu.be/NGinvU_b_ug[/video]

Talking about uchochezi? have you forgotten who brought this issue? go back few posts if you have that short a memory.
 

zomba
Asante sana kwa kunifanya nicheke saana asubuhi hii. Siku imeanza vizuri.

Tatizo ni moja tu:

Kuna waislam ninawaheshimu hapa jamvini na hata mitaani kwetu, na haitakuwa busara kuijibu hiyo post yako wakati najua nitawaudhi na wengine. Na kwasababu mambo yenyewe hayahusiani na historia au uchochezi wa Moh, basi naomba kukubali kushindwa katika hoja hizi.

Turudi kwenye historia.
 
Last edited by a moderator:

Mimi na maswali mawili kwako kwa faida ya wanaukumbi ungetupa majibu kutokana na bandiko lako.

1) Waislam wa wapi wanawaita maswahaba watakatifu, hii umeipata wapi tupe dalili, katika Uislam ni makosa makubwa kumuita binanadamu mwenzako mtakatifu hiyo sifa ni ya Allah peke yake.

2) Unataka kutuambia Kanisa Katoliki limemuita Nyerere mwenye heri na mtakatifu sababu aliandika vitabu vya sala za Kikatoliki kwa Kizanaki. Ni watu wangapi ambao wameitwa watakatifu na wenye heri kutokana na kuandika vitabu vya sala kutokana na lugha zao.

Cc.. gombesugu, Kadogoo,
 
Last edited by a moderator:

Unaweza kunitajia marais wangapi duniani ambao ni Wakatoliki ambao wamekidhi vigezo ivyo na kutangazwa wenye heri kisha watakatifu.
 

Mkuu Yericko; Haki ya Mungu, Naona ya Zenj yameisha. Okello na magobore yake ya kipolisi kamaliza mnakasha. Kwa spidi hii huenda tukafikia kwanini watu wanazika kwa kuchoma wenzao moto, au kuchuna ngozi, hewa imejaa hamu ya visasi. One mistake one goal, kiasi watu hawajipi muda wa kusoma na kuelewa nini mwenzao kaandika!!!!!! yaleyale ya zenj. hahahahahah
 
Wanaukumbi nafurahi kiasi naoa mjadala unaelekea ukingoni hoja mbali mbali zimejibiwa kiustaharabu na kwa ufundi wa hali ya juu sana.Nimefurahi kuona jambo moja likijitokeza wazi pasipo na shaka yoyote kwamba sumu iliyokuwa ikimwagwa kwa muda mrefu hatimaye imepata majibu stahiki.Ni wajibu wetu sote kuhakikisha masuala ya mazito kama haya yanapojitokeza yasiachwe yakisambaa kwa muda mrefu yakaharibu jamii yetu.

Nawashukuru wote waliojitolea muda wao mwingi na kushughulisha akili kwa faida ya VIZAZI VYA SASA NA VIJAVYO hapa pia napenda angalizo na Wickama lizingatiwe sana hii mitandao ina nafasi kubwa na pana kuliko hata vitabu ambavyo kwa sehemu kubwa havisomwi na vijana wengi ukilinganisha na mitandao.
 
Last edited by a moderator:

Hiyo video ya mapinduzi na hayo magombore unayofanya kama ushahidi wako imerekodia mwaka 1964?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…