Uchochezi wa Mohamed Said na dhihaka kwa Wapigania Uhuru wa Tanganyika na Zanzibar


Zomba and Nanren; Salamuni. nawaona mmejikatia kijikona chenu cha mnakasha mnatesa hahahaha. Nilitaka kumwambia Nanren kuwa, Quran haina hati milki ya mtu kwa hiyo una haki ya kupata nakala na kusoma pia. Ukitaka pia kujua mambo kama hayo Zomba anayokuambia tembelea websites kama ya Harunyahya.com. Hiyo ni documentaries na ushahidi sio conversion campaigns. Ukitaka kununua nakala yako vizuri zaidi tafuta ya YUSUFALI (japo ni ya kiingereza) kwa vile ina subject index kwenye kurasa za nyuma kwa hiyo haraka unaweza ku-refer, Hiyohiyo ya YUSUFALI ndio yenye the larget global readers moslems and non-moslems among translations. Ya Kiswahili mimi natumia ya Sheikh Saleh Farsy. Ila haina subject index (labda kama wameweka karibuni). Hizi zinauzwa maduka yote ya vitabu vya kiislamu and you can buy your own copy (kama 20,000/=). Baada ya hapo unaweza kumstua huyo Zomba na AYA (hahahahaha). Zomba, kunae Zomba mmoja tulikuwa wote Masange JKT, anatokea Tanga, haswa Korogwe. Kama ni nduguyo msalimu. I hope I have helped.
 
Sasa naanza kumwamini Commando, Dr Salmin Amour, alipodai kuwa naye alitaka kupinduliwa na akina Maalim Seif mwaka ule. Nisichokijua ni vipi jambo hili lingewezekana katika "NCHI" ambayo imo ndani ya nchi nyingine!

Mkuu kuna kazi kubwa sana,

Watu wamepandikizwa chuki ya hali ya juu, kila kitu wanakichukia,

Wanachukia hata mafundisho yasiyo yao, wanauchukia hata uislamu pia, wamejitenga, wao wanajiona ni waislamu safi na wale wanawaona ni mamluki, hii ni hatari kweli kweli!

Mafundisho ya maudhi ya watanzania wenzetu yamegeuka kuwa janga la kitaifa!

Naaam kwakuwa maandishi yao hayanunuliki kwa wingi na vijana wengi wapo katika ulimwengu wa dotikomu, nasi tusimame hapa hapa kuwaambia huo ni uongo na huo ni ukweli!

Tukifanya hivyo tutaokoa watu wengi sana wasiangamie kwa chuki hii!
 

Yericko,
Ukiwa scholar kitu ambacho naamini sasa wewe uko "on job training"
kuna maneno hutakiwi kutumia.

Jiepushe na slogans, partisanship etc. etc.
Epuka maneno "mapinduzi matukufu" na mfano wa hayo.

Langu moja.
Nyerere si wa kundi lilokuja "kuunga mkono."

Jeshi lilovamia Zanzibar limetoka Tanga.
 
Mzee Mohamed,
Maneno "Mapinduzi Matukufu" nimeyatumia mimi na nimekuwa nikiyasikia hivo kutoka kwa wana "Mapinduzi Daima". Bahati nzuri mimi sio scholar. Niruhusu tu niendelee kuyatumia kwa kuwa sisi waumini wa MUUNGANO tunajua bila ya Mapinduzi haya TANZANIA isingekuwepo.

Tanga pia ilikuwa chini ya himaya ya Mwalimu. Usisahau.
 

Yericko,
Ukiwa una taarifa za Okello kupanga mapinduzi hebu mwaga
hapa jamvini tufyonze ilm sote.

Mie nimeweka hapa ya Kipumbwi nyote mmestarehe.
Nimeweka na majina matatu ya wapishi wakuu -
Bwana Mkubwa, Hanga na Kambona.

Sikuishia hapo nikaweka na wasaidizi - Jumanne Abdallah,
Ali Mwinyi Tambwe na nakuongezea lingine huyu mission
yake ilikuwa Unguja - Issa Mtambo.

Skuishia hayo nikaweka na punda wao wa kuwabebea mizigo
mizito - Mohamed Omar Mkwawa, Jimmy Ringo na Victor Mkello.

Kisha nikamalizia na majembe yao ya kazi - jeshi mamluki la
Wamakonde.

Weka taarifa za Okello siyo kutupa majina tu - name throwing si pake
penye ngoma nzito kama hii.
 

Yericko,

Tanga alikuwapo pale Jumanne Abdallah na Ali Mwinyi Tambwe
watu wa Nyerere na ndiyo kisa cha jeshi la Wamakonde kuwa na
fursa ya kujifaragua watakavyo.
 

Nashukuru sana umerudi kwenye mjadala huu ambapo kipengele tulichoingia kinahitaji utulivu na hekima ya juu sana!

Kwanza mimi nitakazia kuwa yale ni mapinduzi matukufu yaliyomtoa mzanzibari utumwani na kumpa uhuru wake,

Hilo tu linatosha kuyapa nguvu ya utukufu kwa wanaojua maana ya mapinduzi ya uhuru!

Pili, Umesema wazi kuwa "jeshi" lililopindua lilitoka Tanga,

Kwa maneno hayo nimefurahi kuwa sasa unamtambua Okello kuwa aliongoza mapinduzi hayo, na zaidi unakubaliana rasmi kuwa alikuwa na jeshi tofauti na maneno yako ya awali,


Sasa najenga hoja kulina na majibu yako mkuu wangu,

Katika kipindi hicho cha mapinduzi ya Zanzibar tayari Tanganyika ilikuwa huru, na ilikuwa na jeshi lake la nchi, hivyo Mwalimu Nyerere alikuwa amiri jeshi mkuu wa majeshi yote ya ulinzi nchini,

Sasa naomba kujua hao wapiganaji wa Okello waliotoka Tanga walikuwa wanajeshi wa jeshi la Tanganyika?

Kama sio basi kimanti na kimtazamo wa mapana na marefu Mwalimu hakujiingiza kijeshi katika mapinduzi hayo,

Zaidi ni kuwa Okello aliungwa mkono na wakaazi wengi wa Zanzibar hasa vijana na kupelekea kuunda jeshi la mapinduzi tena lisilo na silaha na likafanikiwa kupata silaha ndani ya purukushani za ngumi kavukavu katika Mapinduzi hayo!
 

Vema sana, inawezekana ulipitiwa lakini hii nilishaileta hapa!

Shushia birauli ya maji mkuu!

Ndani ya Zanzibar Okello alipata umaarufu kwa vijana majabari, ambao wengi katika wao walikuwa ni makuli na wachukuzi w meli zilizoingia na kutoka bandarini Zanzibar, kundi lake hili John Okello lilikutana kwa siri. Okello aliwapa matumaini ya mabadiliko watu wake hawa, wafuasi, ambao wakifanya kazi pamoja kwa muda mrefu, mara nyingine katika mazingira ya hatari, na tayari kufuata amri za kiongozi yeyote ambaye ataweza kuwalipa. Wao walikuwa waasi wanaotafuta makaazi.

Usiku wa tarehe 12 Januari 1964 kundi la watu 300 walikitwaa kisiwa cha Unguja wakiongozwa na mtu asiyekuwa maarufu kipindi hicho, aliyekuwa akiitwa John Okello, John Okello alikuwa akiishi Pemba ambako alitokea Uganda miaka michache tu.

Mchafuko wa kisiasa ulikuwa ukiongezeka ndani ya Zanzibar na Pemba tangu kifo cha Sultani Khalifa katika mwaka 1960. Sultani Khalifa alitawala Zanzibar kwa karibu ya miaka 50, tangu mwaka 1911. Baada ya udanganyifu mkubwa kwa majimbo ya uchaguzi na mseto katika chaguzi kuu mbili za mwaka 1961 vyama vikuu vilishindwa kujipatia wingi wa kura kwa kila kimoja.

Waingereza waliondosha majeshi yao kikiwemo kikosi maalumu cha Kiarishi ambacho kilikuwa kimewekwa karibu na uwanja wa gofu na mpaka wa mji mkongwe mapema mwaka 1963. Wakati mfalme mpya, Jemshid akipandisha bendera ya Taifa huru la Zanzibar tarehe 12 Disemba 1963, aliadhimisha uondokaji wa Gavana wa kiingereza Zanzibar na mwisho wa ukoloni Zanzibar.
Uchaguzi mwingine uliofanyika mwishoni mwa mwaka 1963 ukiipa ushindi mdogo wa kura Muungano wa vyama viwili ZNP na (chama cha kizalendo Zanzibar) na ZPPP (Chama cha watu wa Pemba na Unguja). A.S.P (Chama cha Afro shirazi) kilikuwa kiwe kipo katika Serikali iliyo na chini ya nusu ya wabunge kwa mtindo wa bunge la Kiingereza na Sultani, akiwa kama ni mtawala tu lakini sio mtawala mwenye maamuzi ya mwisho.

Taifa hili la Zanzibar ambalo lilikuwa mwanchana kamili wa Jumuia ya madola na mwanachana mpya wa Umoja wa Mataifa lilidumu kwa siku 33 tu.

Majadiliano makali ya kisiasa na maandamano yalikuwa ni matukio ya kawaida siku hizo. Makundi ya watu yaliyokuwa yakiimba na kusifu majina mbalimbali ya viongozi wa kisiasa, huku yakivuka vizuizi vya barabara vilivyokuwa vikilindwa na askari wa kiingereza. Vikundi mbali mbali vilijadiliana juu ya mambo mbali mbali; mfano Haki dhini ya fursa, Wageni dhidi ya wenyeji wa zamani, Ubepari dhidi ya Ujamaa, Wafanyabiashara dhidi ya wamiliki ardhi, Waunguja dhidi ya Wapemba, Waasia dhidi ya pazia la nyuma la vita baridi na harakati za utaifa na kuondosha ukoloni ambazo zilikuwepo kipindi hiki ndani ya Afrika.

John Okello hakuwa na jawabu ya mambo haya nyeti, lakini alikuwa na kipawa cha kutambua kwamba vikundi hivi vinavyoshindana vinatoa nafasi nzuri kwa mtu wa harakati kama yeye Okello.
Hata hivyo, watu kama mia waliojizatiti wangaliwez kutwaa vituo muhimu vya kienyeji vya habari na kambi za Polisi. Mara tu baada ya vituo vya habari na Kambi za polisi pamoja na silaha kudhibitiwa na John Okelo, Ni nani katika visiwa angeweza kumshinda? Jee, wanasiasa wangeliungana na kumshutumu na kumpinga kwa vitendo vyake visivyo halali? Au kama alivyotaraji, wangeendelea kutoaminiana na kutuhumu kwamba kati yao ndio wanaomuunga mkono? Jee, wasingelitaka kukubaliana na yeye, haraka kabla mwengineo hajafanya hivyo? John Okello alichezesha dadu usiku huo wa mwezi wa Januari.

Viongozi wa A.S.P walifadhaishwa na matendo ya Okello (wengi wao, walikuwa hata hawapo visiwani wakati huo). Walikimbilia haraka kuwaunga mkono waasi. Mamia ya wafuasi wa vyama walipigwa na butwaa juu ya wale ambao walikuwa na shuku ya kukata fundo hilo gumu la majadaliano ya kidemokrasia na kukimbilia moja kwa moja kwenye utawala. Hawawalitafuta njia ya kuiandaa jamii kwenda sambamba na kanuni zao. Kanuni siku hizo zilikuwa ni ghali sana kama sarafu ya Marekani. Ubinadamu ulikuwa ni kitu adimu sana.

Baadhi ya viongozi wa ASP baada kuona kwamba serikali itakuwa haina udhibiti na uwezo kujilinda na kutokuwa na imani matokeo ya chaguzi huria zilizofanyika, viongozi hawalitafuta njia za haraka za kuhalalisha udhibiti yale ambayo yaliitwa sasa "Mapinduzi". Makundi ya watu wenye fujo yalikuwa huru. Sheria na amani zilikuwa hazipo katika mitaa ya Zanzibar.
Walimiliki ardhi na wafanya biashara waliburutwa kutoka majumbani na madukani mwao, uporaji na mauaji yalienea mji mkongwe mzima. Kwa kweli mji wenyewe uliporwa.

Waarabu na Waasia , waliokuwa wakiunga mkono vyama vyengine waliuliwa kwa makundi. Kwa usiku mmoja maisha ya watu yasiyovika yalipotea na siku nyengine baadae maelfu ya watu waliikimbia nchi pamoja na kila walichoweza kubeba.

John Okello mwenyewe alijipachika cheo cha Jemedari Mkuu akishirikiana na bataliani zake zenye fujo walianzisha utawala wa vitisho ndani ya visiwa vya Unguja na Pemba. John Okello alitangaza vitisho visivyo vya kawaida na ahadi ya kifo kwa wote watakaojaribu kumpinga yeye. John Okello aliamini alikuwa akipokea maelekezo /dokezo kutoka kwa Mungu na akionyesha uwezo usiokuwa wa kawaida kwa kutumia nambari, kwa mfano tarehe 13 Januari, 1964, alitangaza ujumbe ufuatao." Serikali sasa inaendeshwa na sisi… ikiwa mtakuwa wakaidi na kukataa kutii amri, Nitachukua hatua kali mara 88 zaidi ya hatua ninazozichukua hivi sasa" na "Na ikiwa yeyote atashidnwa kutii amri ya kutotoka nje ya nyumba kama walivyofanya wengine….sitokuwa na njia nyengine lakini kutumia silaha nzito. Sisi, ni jeshi lenye nguvu ya 99,099,000".

Vitisho vyake na uwezo wake wa kuvitekeleza viliwatia hofu raia, hasa makundi mbali mbali ya jamii zilizo ndogo. Tarehe 14 Januari, 1964 alitangaza maneno haya ya kufadhaisha" Huyu hapa ni Jemedari Mkuu wa Unguja na Pemba…Nafikiria kuelekea kijiji cha Mtendeni kukiangamiza ikiwa watu wa hapo hawatafuata amri. Baada ya dakika 40 nitawamaliza nyote hasa Wangazija", " na kwa vijana wote wa kiarabu wanaoishi Malindi; Nitapita Malindi nikiwa nimesheheni silaha ambazo mimi mwenyewe ndie nizijuazo. Nataka kuona kila mmoja abakie na chupi na kulala chini. Nataka kuwaona wao wanaimba... Baba wa Waafrika. Mungu Mbariki yeye na malengo yake na yale ya Jemedari Mkuu"

Wakati unyanyasaji uliposima jamii za tamaduni tofauti za Zanzibar zilikuwa zimeparaganyika. Taifa la chama kimoja lilitangazwa. Lakini bado jTaifa hili likihofia uwezekano wa kufufuka upinzani kutoka kwa wapinzani waliokimbia nchi. Wanamapinduzi hawa baadae walijihakikishia udhibiti zaidi baada ya kusaini mkataba wa muungano wa Tanganyika. Hii ingeruhusu maelfu ya marafiki wa kisiasa wa Tanganyika kuingilia kati upinzani wowote wa baadae katika visiwa hivi. Askari polisi wa Zanzibar walibadilishwa kwa askari polisi kutoka Tanganyika ambao ni watiifu kwa chama na pazia la siasa za utengano ziliwakumba wazanzibari ambazo zilitakiwa kudumu kwa zaidi ya miaka 20.

Leo hii siasa hizi za utengano hazipo tena, kumalizika kwa vita vya baridi na kuelekea kwa uchumi wa kisasa umeweza kuifungulia Zanzibar milango kwa ulimwengu wa nje. Uchaguzi wa vyama vingi ulifanyika mwaka 1995, 2000, 2005,2010 na mwingine unatarajiwa 2015.

Viongozi wa kweli na wenye kujali hali za watu wameibuka Tanzania na hii imewafanya wakimbizi waliokimbia wakati wa mapinduzi kurejea visiwani. Uvumilivu na amani wa watu wa aina tofauti, ambayo ni tabia ya maisha ya wazanzibari, sasa hivi unajitahidi kurejea katika mitaa ya mji mkongwe.
 
Nakumbuka Jeshi la Tanganyika liliasi mwaka huo 1964. Nisaidieni ilikuwa tarehe na mwezi gani. Wakati Tanganyika na Zanzibar vinaungana sikumbuki kama tulikuwa na jeshi huku bara.
 

Assalamu alaykum Yaa Gombesugu.


mashaA'llah hakika wewe si msahaulifu. Kwali nimesheheni nondo nyingi sana za kiuchumi ambazo nimezifanyia Tafiti za kitaaluma katika Coast of East Africa nimeanzia Mbombasa , Lamu, Dar , Mtwara na Lindi na kuonyesha fursa mbalimbali walizonazo ikiwemo matumizi sahihi ya bandari, Ardhwi nzuri walizonazo kwa kilimo cha mazao ya chakula na biashara na hata kubainisha kwa kina kile Wakoloni walichobaini na kukiendeleza ambacho baada ya uhuru wa Tanganyika husda na choyo za viongzi waliamisha fursa hizo na kuziondoa katika mpango wa maendeleo na balaa lake sasa ndio linaoneka.

Naona nisimwage mchuzi nasubiri uzi Ya'akhiy.

Tumeambiwa na Alllah Fas'bir swaburran jamiila. nami nisubiri.

maa salaam
 
Nakumbuka Jeshi la Tanganyika liliasi mwaka huo 1964. Nisaidieni ilikuwa tarehe na mwezi gani. Wakati Tanganyika na Zanzibar vinaungana sikumbuki kama tulikuwa na jeshi huku bara.
Uasi wa jeshi la Tanganyika ulifanyika Januari 20, 1964. Siku nane baada ya mapinduzi ya Zanzibar. Kufikia wakati tunaungana jeshi letu lilikuwa linapitia mabadiliko, likipewa mafunzo na wanajeshi wa Kinigeria na kuunda Jeshi la Wananchi wa Tanganyika.
 

Yericko,

Awali unatakiwa kujua kuwa unaposema Zanzibar unaamanisha visiwa viwili tofauti ambavyo ni Unguja na Pemba. Na vile vile unatakiwa kujua kuwa kutoka Unguja kwenda Pemba ni mbali sana kuliko Unguja kwenda dar es salaam. Pemba ipo karibu na Tanga.

baada ya kukupa huo mwangaza kidogo wa NENO ZNZ, rejea kuhusu vyombo duni vya wakti ule vya usafiri kutoka Unguja kwenda Pemba. Suala je Okello huyu aliweza kutawala mpaka Pemba?

Binafsi sipendi sana kuzungumzia mapinduzi hayo na siwezi kuyaita matukufu kwani yaliniachia majonzi ya kupoteza baadhwi ya ahali zangu na kwetu mpaka leo siku hiyo tunafanya hitma kuwakumbuka.

Sioni faida kuyazungumzia kwa sasa kwani yananikumbusha mbaali sana.

Kuna Mwandishi mmoja maarufu Znz na hata Bara na pengine Afrika akiitwa Al marhum Ali NABWA ndie ninayeweza mkumbuka aliyenivusha mimi nikiwa mdogo na mama yangu kutupeleka kiyanga Mwera kutoka shanghani siku ya 20 baada ya mapinduzi.

naomba niishie hapa kwani niliyoyaona naomba yasijitokeze tena hivi sasa.

Inna Lillahi wainna illaihi Rajihunna.

 
Nakumbuka Jeshi la Tanganyika liliasi mwaka huo 1964. Nisaidieni ilikuwa tarehe na mwezi gani. Wakati Tanganyika na Zanzibar vinaungana sikumbuki kama tulikuwa na jeshi huku bara.

Maasi yale yalikuwa ni 20/01/ 1964,

Jeshi tulikuwa nalo tulilorithi kwa muingereza, hata mkuu wake wa jeshi alikuwa ni mzungu!
 

Pole sana ndugu yangu, tena pole sana kwa masaibu yalokukumba katika harakati za ukombozi wa Mzanzibar!

Pamoja na madhila yoooote hayo bado yatabaki kuitwa ni mapinduzi ya Okello yaliyozaa Zanzibar hii ya leo, na wazanzibar wote watabaki kuyaheshimu na kuyatukuza kama wafanyavyo sasa!

Huo ndio ukweli mchungu lakini ni dawa!
 
Nakumbuka Jeshi la Tanganyika liliasi mwaka huo 1964. Nisaidieni ilikuwa tarehe na mwezi gani. Wakati Tanganyika na Zanzibar vinaungana sikumbuki kama tulikuwa na jeshi huku bara.

WC!
Januari 20, 1964.
 

Sitapenda kuzungumzia hili kwani naona tunarudi pale pale unapo penda kumsifia Okello ili uonyeshe kuwa yeye alikwa shupavu.

Kifupi mila, desturi na sirka za waZnz wote ni upole na ukarimu. Huko hakukuwa na magomvi wala watu kuuwana au hata kukatana mapanga kama ilivyo mikoa ya mara na mengine kula kanda ya Ziwa.

Okello alichukuliwa kama mtu katili sana mwenye haiba ya kutisha na umbo lake na hivyo alitumika kama nembo ya kutisha watu lakin si yeye aliyefanya mapinduzi.

Unajua mpaka leo ukiwa Unguja fujo zozote zikitokea basi eneo la kwanza kuzungukwa na majeshi ni mji mkongwe. na hata kipindi hicho kulikuwa na vikosi viwili vikubwa viliingia Mitaa ya mji mkongwe na viongozi wake wnafahamika kufanya unyama huo. Okelo aliweza kupita na kutoa vitisha siku ya pili baada ya mapinduzi.

Ok nilikuwa ytu nakupa high light usimpe swifa ambazo hakuwa nazo.
Inna Lillahi wainna illaihi Rajihunna.
 
Kwa niaba ya Alyh Bab, gombesugu, basi chukuwa huu mpini walaahai...kutoka kwa Harith Ghassany.
Kwaheri Ukoloni, Kwaheri Uhuru: Zanzibar na Mapinduzi ya Afrabia

HATA kama hupendi kusoma vitabu; hiki si cha kukosa. Kwanza kimeandikwa kwa Kiswahili fasaha; lugha yetu mama inayoanza kufifishwa na kuchujwa na kizazi kisichosoma vitabu siku hizi. Pili, kimepikwa na mtaalamu halisi. Dk Harith Ghassany alizaliwa Zanzibar akapata shahada ya udaktari wa Falsafa Chuo Kikuu cha Harvard, Massachussets, Marekani. Harvard ni chuo cha kale sana; kilianzishwa mwaka 1636 na kwa muda mrefu kimeorodheshwa na magazeti, watalaamu na chama cha vyuo vikuu duniani kuwa cha kwanza duniani.
Fani yake kuu ni utafiti. Dk Ghassany ambaye anasema alitafiti kitabu hiki muhimu kuanzia 2004 hadi 2009 alikuwa awali Profesa Msaidizi Chuo cha Udaktari na Sayansi za Afya , Chuo Kikuu cha Sultani Qaboos, kilichoko Muscat, Oman, Uarabuni. Nilipomhoji kutokea Marekani anakoishi, Dk Ghassany alifafanua lengo la kuandika kigongo hiki chenye kurasa 500: Nia yangu ni kuziondoa fitina za upotoshaji wa historia ili uhusiano mkongwe baina ya Wazanzibari, baina ya Wazanzibari na Watanganyika (Watanzania) na baina ya Waafrika na Waarabu, upate kuendelea kutiririka na kuimarika kwa maslahi ya kujenga amani na neema kwa faida ya walio wengi na vizazi vya baadaye vya pande zote. Sijawahi kusoma kitabu kinachomhusu kila Mtanzania kama hiki.
Licha ya kuhadithia, kinatafakari maswali mengi. Je, neno Afrika asilia yake nini? Vipi tukaitwa Tanzania? Vipi Wazanzibari wengine hawautaki Muungano? Mapinduzi ya Unguja yalianzia wapi? Nani hasa alihusika? Je, viongozi waliopindua ndiyo waliotawala? Ndani ya sura ya pili, inayohusu Mirengo ya Kizalendo na Mapinduzi, ukurasa 23, mwandishi anatueleza bila kupepesa macho: Msomaji anatakiwa awe makini kabisa na hata kabla hajaendelea kusoma inampasa afahamu kuwa viongozi wakubwa wa Chama cha Afro Shirazi kama marehemu, Mzee Abeid Amani Karume, marehemu Mzee Thabiti Kombo Jecha au Sheikh Aboud Jumbe hawakushiriki katika mipango halisi ya mapinduzi ya Zanzibar. Si kitabu cha kisasi chenye azma ya kusakama wakuu wa nchi na mashujaa wetu wa zamani kibwege; au kuwachafua. Dk Ghassany anakiri hana kabisa mshawasha wa kutaka kuja kuwa mwanasiasa au mgombea kiti cha urais. Zamani Mwalimu Julius Kambarage Nyerere alipenda kutuambia wasomi tusisahau tulikotoka. Kambarage alimlinganisha msomi na kijana aliyetumwa na kijiji chenye njaa kukitafutia ahueni kisha arudi kuwasaidia wanavijiji wenzake.
Dk Ghassany ni msomi wa kabila hilo. Katimiza wajibu wake. Anasema kitabu kilikuwa kigumu kukiandika na pia kigumu kukisoma. Moja ya msingi mahsusi wa kazi za historia ni kutukumbusha watu tuliowasahau na mafunzo yake.
Tunamkumbuka John Okello? Je, Oscar Kambona, mpinzani mkuu wa hayati Nyerere na ujamaa aliyeishia uhamishoni hapa London, alihusikaje katika mapinduzi ya visiwani? Je, nini kilitokea wakati wa maasi ya wanajeshi wa Tanganyika mwaka huo huo wa 1964? Je, silaha za mapinduzi ya Zanzibar zilitoka wapi? Je, vyama vingine kama Umma Party cha hayati Abdulrahaman Babu vilifanya nini? Kassim Hanga ni nani? Je, kwanini Kassim Hanga akanyongwa miaka michache baada ya mapinduzi ya Unguja, 1964? Je, aliyekuwa zamani kiongozi wa Algeria, Ahmed Ben Bella (ambaye yu hai) alihusikaje? Je, wanamapinduzi maarufu wa Cuba Fidel Castro na Che Guevara walihusika? Kwanini shirika la Upelelezi la Marekani, CIA lilikuwa likiogopa sana Unguja? Je, vipi maelfu ya Wazanzibari wamezagaa ulimwenguni wakiishi Ulaya, Marekani na Uarabuni, baada ya kuikimbia nchi yao? Je, mwanajeshi maarufu Kanali Ali Mahfoudh alifanya nini? Maswali mengi yamejibiwa si tu kwa utafiti maridadi alioufanya mtaalamu huyu bali pia kupitia midomo ya waliohusika.
Kitabu kimejazana hati za siri, za kiserikali na pia mahojiano na wazee hai walioshika mapanga enzi hizo. Wengine wao kama Victor Mkello (aliyekuwa zamani mmoja wa viongozi wakubwa wa Chama cha Wafanyakazi na TANU wanahadithia kinauga ubaga ama walivyotiwa ndani, walivyosakamwa na nani alifanya nini katika ngazi za juu. Hiki si kitabu cha mchezo. Kuna pia mchango wa mzalendo na mwanahistoria mwingine Mohamed Said (aliyeandika vitabu viwili vinavyohusika na historia ya TANU, kimojawapo Uchaguzi wa mwaka 1958 katika kutafiti habari kibao.
Alivyokuwa mkweli, mbali ya utafiti na picha lukuki; Dk Ghassany aliwaonyesha viongozi wa sasa Unguja na bara muswaada wa kitabu kabla ya kuutoa. Anasema : Mustakbali utakuwa mzuri iwapo utajiri wake mkubwa wa kihistoria wa kijiografia wa Zanzibar na Tanzania utatumika kuuimarisha Muungano wake na Tanganyika baada ya Baraza adhimu la wawakilishi kuipitia na kuifanyia marekebisho katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kuyalinda maslahi ya Zanzibar na kuonyesha njia mpya ya Muungano wa Jamhuri ya Tanzania. Unguja na Pwani kijumla ndiko lilipo chimbuko la lugha ya Kiswahili. Kama kazi ya fasihi ya lugha hii tukufu, kitabu kitakusaidia msomaji (hata uwe si mpenzi wa mambo mazito ya kihistoria na kisiasa) kuboresha ujuzi wako wa Kiswahili fasaha, hasa vijana. Kwa watu wa makamo na wazee, wataalamu na wapenda nchi yetu watapata changamoto na jopo la kufanya majadiliano, kupitia mambo ambayo tuliyasikia tu mitaani miaka 40 iliyopita.

Kwanza naomba kujua, Je unatambua Okello ndie aliyeongoza mapinduzi yale?
Huu mpini mwingine kutoka kwa Ahmed Rajabu.
[h=3]Siku John Okelo alipotimuliwa Zanzibar[/h]
Ahmed Rajab
YAFUATAYO ni masimulizi mafupi ya kipindi kifupi cha Mapinduzi ya Zanzibar ya Januari, 1964 yaliyoipindua serikali ya ubia ya chama cha Zanzibar Nationalist (maarufu Hizbu) na kile cha Zanzibar and Pemba Peoples Party (ZPPP). Tunaangazia nini hasa kilitokea usiku wa Jumamosi Januari 11, yaliyojiri siku ya pili yake na mwezi mzima wa Januari, mwaka 1964 .
Tumeyakusanya masimulizi haya baada ya kuzungumza na walioshiriki katika Mapinduzi hayo ambao baadaye walisaidia kudhibiti madaraka na kuunda taasisi zilizoziba pengo la Serikali iliyopinduliwa ya Waziri Mkuu, Muhammed Shamte Hamadi.
Usiku wa manane wa Januari 11, makada wapatao 200 wa Umoja wa Vijana wa Afro-Shirazi (Afro-Shirazi Youth League) walielekea kwenye kambi ya polisi ya Ziwani, nje kidogo ya mji huko Unguja.
Wakiongozwa na Yusuf Himid wapinduzi hao hawakukabiliwa na upinzani walipofika Ziwani ila waliikuta ghala ya silaha iko wazi na wakazinyakua silaha na kukimbia nazo hadi kwenye uwanja ulio nje ya jengo la Raha Leo.
Hapo ndipo palipokuwa makao makuu ya Mapinduzi kwa siku chache na ndipo wapinduzi walikokuwa wakipewa silaha. Studio za redio ya Serikali pia zilikuwa hapo.
Moja ya sababu zilizoyafanya Mapinduzi yafanikiwe haraka ni uamuzi wa viongozi wa Serikali iliyopinduliwa  Sheikh Muhammed Shamte na Sheikh Ali Muhsin Barwani  kuwataka wafuasi wao wasitumie nguvu kuyapinga.
Hivyo, mbali na mapigano yaliyozuka saa za asubuhi ya Jumapili Januari 12, mbele ya Steshini ya Polisi Malindi, hapajazuka mapigano Unguja kati ya waliopindua na waliopinduliwa. Pemba nako pia hakukuwa na upinzani ijapokuwa kisiwa hicho kilikuwa ngome ya vyama vya ZNP na ZPPP.
Wengi wa wapiganaji waliokuwa kwenye Stesheni ya Polisi ya Malindi walikuwa wakuu wa polisi Wakiingereza. Wakipigana na makada wa Umma Party ambao ndio pia waliouteka uwanja wa ndege, bandari pamoja na kituo cha mawasiliano ya nje cha Cable & Wireless, kilichokuwa kwenye jengo ambalo sasa ni Hoteli ya Serena Mji Mkongwe.
Kwa hakika, kinyume cha baadhi ya watu walivyoandika hapakutokea mauaji ya kimbari. Aliyeanzisha uvumi huo alikuwa John Okello aliyeandika kwenye kitabu chake kuhusu Mapinduzi ya Zanzibar kwamba watu zaidi ya elfu kumi waliuliwa. Okello aliongeza kwamba aliamrishwa na Yesu Kristo kuwakomboa Waafrika wa Zanzibar kutoka kwa wageni.
Tutamrejelea Okello na wengine waliokuwa Raha Leo baadaye. Kwanza tukumbushe kwamba mkesha wa Januari 12, mwaka 1964, Zanzibar haikuwa na jeshi. Kulikuwa polisi waliokuwa wakiongozwa na Waingereza. Wengi wa askari polisi walikuwa raia wa Tanganyika. Serikali iliyopinduliwa ilikataa kuandikiana mkataba wa kijeshi na Uingereza kwa sababu ikihisi mkataba kama huo utaonekana kuwa wa kikoloni.
Hatuwezi kusema ni nani hasa aliyepiga risasi ya mwanzo au ya mwisho katika Mapinduzi. Naitoshe tusemapo kwamba kwa vile hakukuwa na upinzani, Serikali iliyokuwa madarakani iliporomoka kama nyumba ya karata.
Tuwarejelee sasa waliokuwa Raha Leo, makao makuu ya Mapinduzi kwa siku chache. Kwanza tumuangalie Okello ambaye sauti yake ndiyo iliyokuwa ikivuma kwenye Redio Zanzibar.
Hatuna uhakika nani alimpeleka Okello Raha Leo. Wengine wanasema ni Yusuf Himidi. Wengine wanasema ni Seif Bakari aliyetoa rai atumiwe kutoa matangazo kwenye redio kwa vile sauti yake ilikuwa na lafudhi ngeni ya kutisha.
Uhakika tulio nao ni kwamba Okello alipotokea Raha Leo na mabastola yake, Aboud Jumbe alishtuka na akauliza: Nani huyu? Katokea wapi?
Kijana huyo aliyekuwa na umri wa miaka 27 hakujulikana kabla ya Mapinduzi. Alikuwa mtu asiyejua kuandika wala kusoma na akili zake zikimtosha mwenyewe. Hakuwa na sifa za uongozi na wala hakushiriki katika vuguvugu lolote la kisiasa.
Akijibandika cheo cha kijeshi cha Field Marshall ni yeye aliyetangaza kwamba serikali ya ZNP/ZPPP imepinduliwa.
Kwa hakika, kazi hiyo ya kutangaza kufanikiwa kwa Mapinduzi kwanza alipewa Ramadhan Haji, mmoja wa wapinduzi. Lakini alikataa. Jina la Okello lisingelisikika lau Ramadhan Haji angekubali kutangaza kwamba Serikali imepinduliwa na kwamba wapinduzi waliidhibiti nchi.
Waliokuwa wakiongoza mambo Raha Leo tangu Mapinduzi yaanze, hadi Jumatatu Januari 13, walikuwa Aboud Jumbe, mmoja wa viongozi wa chama cha Afro-Shirazi (ASP), Thabit Kombo (Katibu Mkuu wa ASP) na Badawi Qullatein wa Umma Party. Muda wote huo, Sheikh Abeid Amani Karume (kiongozi wa ASP), Abdulrahman Babu (mwenyekiti wa Umma Party) na Abdalla Kassim Hanga (ASP) walikuwa Dar es Salaam.
Mnamo siku hizo hizo liliundwa Baraza la Mapinduzi na Baraza la Mawaziri lililokuwa na mamlaka kamili ya kuiendesha Zanzibar. Mabaraza hayo mawili yalikuwa taasisi kuu za Serikali ya kimapinduzi ya Jamhuri ya Watu wa Zanzibar. Na sio ile iitwayo Kamati ya Watu Kumi na Nne ambayo baadhi ya watu wanasema kuwa ndiyo iliyoandaa Mapinduzi.
Okello akipenda kujigamba kwamba ndiye aliyeyapanga na kuyaongoza Mapinduzi. Alikuwa akitoa matamshi ya kushtusha na ya ajabu-ajabu kwenye Redio Zanzibar. Kwa mfano, siku moja alidai kwamba alipwe mshahara mkubwa zaidi ya aliokuwa akilipwa Rais Karume. Siku nyingine akasema kwamba kasri zote alizokuwa akitumia sultani kupumzikia apewe yeye.
Kuna siku aliyotoa hukumu kwamba mzee mmoja wa zaidi ya miaka 60 afungwe kwa miaka 99. Alisema kama huyo bwana atakufa gerezani basi mwanawe afungwe ili kuendeleza kifungo na mwanawe akifa basi mjukuu wake afungwe mpaka itimie miaka 99.
Nyakati nyingine aliwaonya watu wazitie moto familia zao na wao wenyewe mpaka wafe kabla ya majeshi yangu kuja. Alikuwa akitoa vitisho visivyowahi kamwe kusikika Zanzibar.
Kuna siku alitangaza kwamba wakazi wa eneo moja ambako alikuwa apite, wajipange foleni barabarani wakiwa wamevaa chupi tu.
Okello alikuwa ni adha, kitisho, kichekesho na fedheha kwa Zanzibar. Viongozi wapya wa nchi walichoka naye na wakaamua kumchukulia hatua. Salim Rashid, mmoja wa viongozi wa Umma Party aliyekuwa katibu wa Baraza la Mapinduzi anasema kwamba, kwanza alilizungumza suala la Okello na Sheikh Karume. Halafu akalizungumza na Brigadia Yusuf Himid na mwisho yeye, Yusuf Himid na Kanali Ali Mahfoudh wakalitafutia dawa.
Ilisadifu kuwa siku moja Okello alisafiri kwenda Dar es Salaam akifuatana na Jaha Ubwa, aliyekuwa katibu wake. Walipokuwa wanatarajiwa kurudi Zanzibar, Karume, Yusuf Himid, Salim Rashid na Ali Mahfoudh walikwenda uwanja wa ndege kumsubiri.
Siku hiyo anaikumbuka vizuri Luteni Hashil Seif aliyekuwa ofisa wa zamu kwenye kambi ya jeshi huko Migombani karibu na uwanja wa ndege. Alipigiwa simu akitakiwa aende kwa haraka uwanja wa ndege. Hakuambiwa anaitiwa nini.
Alipofika ndipo alipoambiwa kwamba kuna ndege ya Shirika la Ndege la Afrika ya Mashariki iliyokuwa inakuja kutoka Dar es Salaam ndani yake wakiwemo pia Okello na Jaha Ubwa. Akaelezwa kwamba awaruhusu abiria wote pamoja na Ubwa washuke, lakini amzuie Okello asishuke. Halafu amwambie rubani ampeleke Okello Kenya.
Hashil naye akampigia simu komredi mwenzake Luteni Amour Dugheshina kumwita aende uwanja wa ndege amsaidie. Maluteni wote wawili walikuwa na bunduki za aina ya machine gun.
Ndege ilipotua walipanda ndani ya ndege, wakampokonya silaha Okello na kutekeleza amri waliopewa. Rubani wa ndege alikasirika sana. Uso wake ulighadhibika, utafikiri mnyama aliyekosewa risasi, alieleza Hashil.
Lakini rubani hakuwa na la kufanya ila kuiwasha ndege na kuelekea Kenya.
Huku nyuma Salim Rashid akampigia simu Oginga Odinga, Makamu wa Rais wa Kenya, kumuarifu kwamba wamemfukuza Okello na wanamrejesha Kenya. Alifanya hivyo kwa makosa kwa sababu kutokana na jina lake akifikiri kuwa Okello ni Mjaluo kutoka Kenya.
Kumbe alikuwa mtu wa kabila la Acholi aliyezaliwa Uganda na alikwenda Unguja kabla ya kuhamia Pemba ambako alikuwa mwashi, mtiaji rangi nyumba na mpasuaji mawe.
Swali la kujiuliza hapa ni; je, iwapo kweli Okello alikuwa kiongozi mpendwa wa Mapinduzi ilikuwaje wafuasi wake na wanamapinduzi wenzake wasimtetee alipoadhiriwa uwanja wa ndege na kufukuzwa nchini? Ilikuwaje akafukuzwa kwa urahisi hivyo?
Kuna uzushi mwingi kuhusu kipindi hiki kifupi cha historia ya Zanzibar. Kwa mfano, kuna filamu ya kubuni ya Wataliana inayoonyesha maiti chungu nzima za watu waliopigwa risasi. Filamu hiyo ilikuwa na lengo moja tu; kuonyesha ukatili na unyama wa Waafrika.
Hakuna ithibati yoyote kwamba watu waliouawa katika siku za mwanzo za Mapinduzi walifika elfu kumi. Ukweli ni kwamba jumla ya watu waliouawa siku hizo haipindukii 200, katika sehemu za mjini hawazidi 25.
Uzushi mwingine ni kwamba walipelekwa Watanganyika, Zanzibar wakiwa na silaha kwenda kupindua. Na si kweli kwamba Mapinduzi yalikuwa na msisitizo wa kikabila. Katika kipindi cha mwanzo cha Mapinduzi msisitizo ulikuwa wa kitabaka. Nyimbo zilizokuwa zikiimbwa kwenye Redio Zanzibar zikiwazungumzia wakwezi na wakulima na wafanyakazi kwa jumla na si makabila.
Mapinduzi ya Zanzibar yalianzisha taasisi mpya za utawala zikiwa pamoja na Baraza la Mapinduzi, Baraza la Mawaziri na ofisi ya Rais. Taasisi hizo zilikuwa zifanye kazi kwa muda wa mwaka mmoja tu kwa vile ilikwishaamuliwa kwamba Januari 1965 pafanywe uchaguzi wa kulichagua Bunge la Katiba, lililokuwa litunge Katiba ya kudumu ya Zanzibar.
Baraza la Mapinduzi la Zanzibar pamoja na Serikali mpya zilianza kwa ubia baina ya chama cha ASP na Umma Party. Ingawa wanachama wa ASP ndio waliofanya Mapinduzi waliutambua mchango wa wafuasi wa Umma Party na hasa mchango wa makada wao waliopata mafunzo ya kijeshi nchini Cuba.
Vijana hao wa Umma walizitia wasiwasi serikali za Marekani na Uingereza na kuzifanya ziamini kuwa utawala mpya wa Zanzibar ulikuwa wa kikomunisti. Dhana hiyo ndiyo iliyosababisha kuchukuliwa hatua ya kuyachimba na kuyagandamiza Mapinduzi ya Zanzibar yaliyodumu kutoka Januari 12, hadi 26 Aprili, mwaka 1964.

Cc.. Wickama, Mag3, gombesugu, Barubaru, Nguruvi3, Kadogoo, JokaKuu, WildCard, THE BIG SHOW, Jasusi, zomba, Spike Lee, Pasco, Mzee Mwanakijiji,
 
Last edited by a moderator:

Ndugu yangu,

Kumchumchukia na kutopenda kumzungumzia hakuondoi ukweli,

Ukweli husimama wima na huwa hauwi tenge hata nyuzi moja!

Kwa nusu muongo sasa wazanzibar wanayaadhimisha mapinduzi haya tena kwa furaha yapekee!

Labda ujue kuwa katika ukombozi wa taifa kwa mtutu wa bunduki, damu ni sehemu ya chagizo la ukombozi huo!

Ni jambo lakujivunia na kumshukuru Mungu kuwa uhuru wa Tanganyika hatukubeba mtutu kuupata na hilo ni sehemu ya linalochagiza sifa kuu za kiongozi wetu wa harakati za uhuru huo mzee Nyerere!

Pamoja na utawala wa mkono wa chuma wa mwanamapinduzi Field Marshal John Okello katika ardhi ya Zanzibar, bado ukweli unasimama kuwa yeye ndie baba wa taifa la Zanzibar!

Yeye ndie kawatoa toka minyororo ya utumwa wa sultani, bila yeye nani muweza?

Katika kipindi cha miezi sita ya utawala wake hakuna kiongozi barani afrika na ulaya aliyethubutu kukenua kinywa juu yake!

Paka walichinjwa kwaajili yakulishana yamini na jeshi lake tiifu!

Ni Nyerere tu ndie aliyefanikiwa kuzungumza nae nakupunguza mbinyo hadi kuchukua madaraka ASP


Sasa ukichukia kuzungumza ukweli huo huko ni kujipunja mwenyewe kama mzanzibar na mtanzania
 
Ritz

Hawa wote akina Mohamed Said, Dr Ghassany, Ahmed Rajabu na wengine wengi, ni aina ile ile, yani unaweza kuita ni mtu mmoja linapokuja suala la Nyerere, uislamu na ukristu!

Kama nimsomaji mzuri wa machapisho yao wala hutapata kuumiza kichwa,

Wao wanamakovu ya Okello na wengine wanamakovu ya Nyerere!

Hivyo kamwe hawezi kuwa 1 mbele ya haya!
 
Dilikeni,
Nimewaomba sana waeleze huo ukweli...
Bado nasubiri In Sha Allah.

Aaah wapi...ndugu yangu ktk IMAAN...huyu mleta hoja amechoka kifikra...hana hoja anaishia kutoa matusi...Nna wasiwasi na akili yake! Mzee Mwanakikijiji ndio kabisa amejichimbia kwenye kutengeneza ngano mpya za huba.....muda mwingi anatumia hisia zake zake zaid katika kuumba hoja kuliko tafakuri

MAY ALLAH REWARD YOU....MOHAMED SAID
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…