Mkuu Yeri', tuwekee Weka
#, sisi wengine hasira zetu zi karibu na tu wepesi wa kuwa provocked hivyo tunachagua post za kusoma na hatusomi zote! haswa kwa kuzingatia, hii ndio top of the toppest threads kuchangiwa kuliko thread nyingine yoyote tangu jf kuanzishwa, ile 2006!, na hapa soon it hit 20,000 posts with 1000 pages!. You have "the powers!" na pia naomba nikiri Maalim Mzee Mohammed Said, "has the powers!"
P.
Ndugu zangu wanajamvi wote mlioshiriki mjadala huu,
Kwa namna moja ama nyingine naomba niwashukuru sana wote bila kujali itikadi ama mitazamo yetu,
Nafanya hivyo nikitambua umuhimu wa kila mmoja wetu hapa katika uzi huu tangu ulipoanzishwa nami 12/01/2013 mpaka hii leo tumekuwa hapa bega kwa bega usiku na mchana,
Nasema wote ninawashukuru kwa ushirikiano wenu, tumeongea pamoja, timecheka pamoja, tumekwazana pamoja, naam na sasa tunaagana pamoja!
Sisi sote ni waswahili na ni binadamu, tofauti zetu zilizotawala mjadala wetu tuziache hapa hapa, vinyongo vyetu tuviache hapa hapa, na kila husda tuliokuwa nao na tuuache hapa hapa!
Tumepata fursa adhimu ya kuzungumza yamoyoni, pia tumepata fursa yakufahamiana na kwa hili hakika tumejenga mtandao imara wa kifikra!
Shukrani zangu za pekee zimuendee Mzee wetu Mohamed Said, amekuwa mvumilivu sana mpaka mwisho akashindwa na hakika amejitahidi, nampongeza kwa hilo tu,
Pia niwapongeza wanahistoria wenzangu waliosimama nami kwa weledi wao kutetea ukweli na kuukemie upotoshaji wa Mohamed Said, hawa si wengingine bali ni Nguruvi3, Mag3, Mwanakijiji, JokaKuu, Jasusi, Son of Alaska, Nicholas, Zumbemkuu, Gwalihenzi, na wengine wengi walioshiriki nasi!
Lakini nitakuwa sina fadhila kama sitawashukuru ndugu zetu kama Ritz, The Big Show, Barubaru, Zomba, Sadeeq, Spike Lee, na wengine wote wakufanana nao!
Niwashukuru sana uongozi wa JF hasa Mods kwa kuusimamia mjadala huu kwa weledi wa hali ya juu sana! Hii ni heshima kubwa sana kwa JF na Tanzania kwa ujumla!
Mwisho,
Wale mliotaka kunifahamu mimii ni nani hasa? Ninawajibu rasmi!
Naitwa: Yericko Yohanesy Nyerere
Mahali nilipozaliwa: Nyololo, Mufindi, Iringa.
Kabila: Ni Mhehe,
Baba yangu: Yohanes Msambila Nyerere, (marehemu)
Mama yangu: Venancia Geremias Mgimwa,
Elimu: Muhandisi wa Umeme na Compyuta kutoka Chuo cha Beijing Information Technology College China (BITC)
Kazi: Mfanyabiahara, Mwenyekiti Mtendaji wa Umoja wa Makampuni ya YECCO GROUP LTD yanayojishughulisha na Ujenzi wa Majengo, Ujenzi wa Mabarabara, Umeme, Teknohama, Uwakala wa Usafirishaji, Uwekezaji katika Majengo, na Usanifu na Ukadiriaji Majenzi
Kuishi: Kigamboni Mbutu,
Nina mke mmoja na watoto wa wili ambao ni Che-Lee na Su-Yang
NB:
Mimi sina UNDUGU na Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, lakini chimbuko la Babu yake na Babu yangu Mzee Msambila Kihulo Lihangawike Nyerere "inasemekana" alikuwa ni wa kaskazini mwa Tanzania!
Kwahiyo katika uzi huu nimesimama kama Mtanzania mwingine yeyote anaekwazwa kuona dhihaka wanayofanyiwa Wanaukombozi wetu!
Nawashukuru nyote, nawaomba tofauti zetu zote tuziache hapa hapa na tuongee lugha moja ya maelewano na kidugu!
Kwa heshima na taadhima ninaomba niufunge mjadala huu kwakuwa ukweli tumeuwkea huru!
Asanteni sana!