Uchochezi wa Mohamed Said na dhihaka kwa Wapigania Uhuru wa Tanganyika na Zanzibar

Sasa kama ni ukweli unataka wakanushe nini?
 
Mleta mada umekiri kwa kusema "bahati mbaya sijui uhalali wa shutuma hizi"
Halafu unataka Mohamed Said achukuliwe hatua!
Mimi ningependa wanahistoria,wapangue shutuma na maandiko ya Mohamed Said kwa hoja na vielelezo
Hujaambiwa tatizo ni historia yake anayoandika. Uwe unasoma andiko kwa utulivu hata mara 7 ili uelewe points za msingi.
Tatizo ni uandishi wake kuonyesha kuwa dini fulani ilibaguliwa/ilionewa na inaendelea kubaguliwa/kuonewa hata sasa.
 
Historia yetu inahitaji kumulikwa zaidi,kuna mengi hatuyajui, hayakuandikwa, yanajaribu kupotoshwa na huenda mengine mengi yamepotoshwa.
 
wewe yeriko unataka kujilinganisha na mzee Mohd ?? wewe umelishwa matango pori na shule za Julius ! acha uelezwe ukweli amabao wengi wetu tulifichwa !
 
Unalalamika sana mzee wangu

Ova
Mrangi,
Hapana tuko hapa tunajadili historia ya wazalendo waliopigania uhuru wa Tanganyika ambao wengi hawakuwa wanafahamika.

Unajua mimi nimepokea tuzo tano kwa kazi hii.
Jamii haiwaadhimishi walalamikaji.

Jamii inawaadhimisha wale wanaotoa mchango wa maana katika jamii waishizo.

Serikali ya Tanzania ilipotambua mchangowa Abdul Sykes na mdogo wake Ally waliwapa nishani ya Mwenge wa Uhuru mwaka wa 2011 katika kuadhimisha miaka 50 ya uhuru wa Tanganyika.

Angalia picha hapo chini:


Medali ya Mwenge wa Uhuru aliyotunukiwa Abdul Sykes 2011

Nikiwa nimeishika Medali ya Mwenge wa Uhuru ya Abdul Sykes nikiwa na watoto wake kushoto Kleist Sykes, Miski Sykes, Aisha ''Daisy'' Sykes na Ilyaas Sykes

Maxence Melo Executive Director JF​
 
Huyo daisy amekuwa pamoja na mama yangu mdogo ujuwe
Hiyo familia hata mimi naijuwa vzr tu mzee wangu
Si ajabu hata wewe unaweza ukawa unamjuwa babu yangu hao wakina sykes wote walikuwa
Kundi moja na wana hang pamoja...
Hivi unajuwa nyerere alimchukulia babu yangu shamba lake lilikuwa babati na akampa ukoo wa kifalme ya uingereza,lakini hakuna aliyelalamika yaani fresh tu
Inaelekea na mimi ningekuwa nahuwa kuandika ningeandika mambo mengi
Ila mwishowe tupunguze kulalamika mzee wangu

Ova
 
Huyu Yaricko ni takataka tu, ana pumba nyingi sana. Alikuja na story za Okello zisizo na kichwa wala miguu
 
Naheshimu na kukubali sana taaluma yako kwenye historia
Hiyo haina ubishi

Ova
 
Mrangi,
Mimi nishakujibu swali hilo.

Yawezekana namfahamu babu yako mimi babu yangu Salum Abdallah alikuwa anaishi nyumba mkabala na nyumba ya akina Sykes Mtaa wa Kipata (sasa Mtaa wa Kleist Sykes) katika miaka ya 1930s.

Watoto wao wamesoma shule moja Al Jamiatul Islamiyya fi Tanganyika na wameishi pamoja hadi sisi tunazaliwa.

Huu ndiyo uhusiano wetu na sababu ya mimi kujua mengi katika historia ya TANU.

Angalia picha hiyo hapo chini:


Na Ally Sykes Muthaiga Club Nairobi, 1989

 
Baada ya kufahamu udini umemlewesha huyo mzee nilianza kupuuza naandiko yake yenye sumu ya Udini kama sumu kuvu kwenye nafaka.
 
Do! zungukeni kote lakini mwisho hakikisheni unatueleza tunatokaje kwenye umaskini uliokithiri tunaokaa nao bila sababu huku tukiendelea kuwaheshimu na kuwajengea himaya viongozi wasio waaminifu katika mali na raslimali za taifa.
 
Baada ya kufahamu udini umemlewesha huyo mzee nilianza kupuuza naandiko yake yenye sumu ya Udini kama sumu kuvu kwenye nafaka.
Nchi hii kama Waislam wangekuwa majority vita ingeshatokea siku nyingi sana.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…