UCHOMAJI WA TAKATAKA ZA HOSPITALI YA "SEKOU TOURE" - MWANZA, NI HATARISHI

UCHOMAJI WA TAKATAKA ZA HOSPITALI YA "SEKOU TOURE" - MWANZA, NI HATARISHI

Bonson

Senior Member
Joined
Apr 20, 2013
Posts
183
Reaction score
147
Ndugu wana FJ,

Naandika uzi huu ili uweze kumfikia Mkurugenzi wa Hospitali ya Mkoa wa Mwanza au Mganga Mkuu wa Mkoa wa Mwanza.

Siku chache zilizopita nilikwenda katika hospitali ya Mkoa kuchukua mwili wa ndugu yangu aliyefariki baada ya kuugua stroke. Jambo lililonishangaza ni kuona sehemu ya kuchomea takataka za hospitali hiyo ikiwa karibu kabisa na wodi za wagonjwa na chumba cha maiti. Moshi ulikuwa unazagaa kila mahali na kusababisha kero kwa watu wote maeneo hayo.

Nauomba uongozi wa Hospitali yetu hii wafanye jitihada za makusudi na za haraka ili kuhamisha eneo hilo la kuchomea takataka kwa sababu taka zingine huwa zikichomwa zinaweza zalisha sumu hatarishi. La sivyo, basi eneo hilo liboreshwe ili moshi usizagae hovyo.

Baada ya kusema hayo, niwapongeze uongozi wa Hospitali kazi kubwa wanayoifanya ya kuhudumia jamii ya Mwanza.

Mungu Ibariki Tanzania
 

Attachments

  • VID-20180719-WA0002[1].mp4
    VID-20180719-WA0002[1].mp4
    9.1 MB · Views: 21
  • IMG-20180719-WA0003[1].jpg
    IMG-20180719-WA0003[1].jpg
    48.7 KB · Views: 61
  • IMG-20180719-WA0004[1].jpg
    IMG-20180719-WA0004[1].jpg
    58.2 KB · Views: 48
  • IMG-20180719-WA0005[1].jpg
    IMG-20180719-WA0005[1].jpg
    35 KB · Views: 51
Hii ni incinerator ipo kwa ajili ya kuteketeza sindano zilizotumika, na taka nyingine hatarishi.

Walikosea kuiweka karibu sana na watu maana moshi wake ni sumu kali kutokana na chemical zinazochomwa.

Niliiona pia nilipokwenda kufuata mwili wa mwanangu.
 
Back
Top Bottom