Uchukie umasikini kwa nguvu zako zote

Uchukie umasikini kwa nguvu zako zote

BilioneaPATIGOO

JF-Expert Member
Joined
Jun 23, 2012
Posts
12,320
Reaction score
11,327
Unasema basi hebu leo uache usafiri wako binafsi upande public transport.

Unachokuta huko ni zaidi ya masikitiko, ama kweli umasikini ukikutafuna na ukaukubali basi hata mawazo yako, ubongo wako hauwazi chochote cha maendeleo.

Unawaza kufa kufa tu yani unawaza tabu tabu tu huzuni huzuni tu shida shida tu, na zaidi hata hizi mnaziita stesheni za redio ukikaa kwenye public transport (usafiri wa umma) nyingi utakua ni mazungumzo ya shida taabu, umbeya, majungu, kifo, huzuni, ushambenga, uchawi, uswahili uswahili, na ajabu 90% ya abiria ambao ndio wanawakilisha asilimia kubwa ya Watanzania basi unakuta wanashangilia na kucheka. Mimi naamini pia baadhi ya stesheni za redio na televisheni zinachangia kwa kiasi kikubwa watu kuendelea kuwa masikini.

Nimeshangaa sana, leo mojawapo ya stesheni ya radio moja nchini kuna mada inasema kati ya jeneza na sanda kipi utapenda kikao nyumbani kwako, unashangaa muutikio wa watu wanashangilia mada na kutoa maoni kana kwamba itainua uchumi wao, najiuliza watu wamekata tamaa kiasi hiki hadi sasa wanawaza kufa kufa tu? Nimesikitika sana na kujiskia aibu.

Poverty is a SIN.
 
Maisha ukiyachukulia serious muda wote utapata tabu sana
 
Back
Top Bottom