Dossa the Economist
Member
- Apr 14, 2018
- 5
- 6
Utangulizi,
Uchumi ni neno lenye maana pana sanaa, ila kwa kifupu uchumi ni jinsi tunavyoweza kutumia rasilimali tulizo nazo kutimiza mahitaji yetu ya kila siku kama mtu mmoja, familia , ukoo, jamii mpaka taifa na kimataifa.
Uchumi endelevu ni jinsi ya kutumia rasilimali tulizonazo kujitosheleza bila kuharibu uwezo wa rasilimali hizo kuja kutumika na vizazi vyetu vijavyo kwenye ngazi ya mtu mmoja adi taifa na dunia kwa ujumla.
JE, TANZANIA INA UCHUMI ENDELEVU?
Uchumi wa nchi yetu unakua kwa wastani wa (4.5-6) kwa mwaka ila watu wengi hawajui ukuaji huo unafanyaje kazi, maana hawaoni kama kuna mabadiliko,
Kuna utofati wa uchumi kukua na uchumi endelevu
1. Uchumi kukua ni ongezeko la bidhaa na huduma kwa mwaka
2. Uchumi endelevu ni mwemdelezo wa ongezeko la bidhaa na huduma kila mwaka bila kuathiri matumizi ya rasilimali hizo kwa vizazi vijavyo.
Tanzania uchumi wetu unakua ila siyo endelevu kutokana na sababu mbalimbali kama zifuatazo;
(A) Maamuzi ya kisiasa kubadilisha mtazamo na mwelekeo wa uchumi wetu kila anapoingia kiongozi mpya , na hiyo inatokana na yeye kutaka kuonekana kafanya jambo flani ili anufaike kisiasa kama kukubalika zaidi au kuapata sifa , mfano raisi wa awamu ya nne alihimiza sana kilimo , ( kilimo kwanza) , kabla hajaifikisha kileleni hiyo sera akaja Raisi Magufuli aka anza na Tanzania ya viwanda, hatujafanya upembuzi yakinifu tuone kama tumefikia malengo , kaingia Rais Samia , yeye anaenda na kila sekta! Je tutakuwa na mwendelezo kwa sekta zote?
(B) Sekta kutotegemeana , mfana viwanda na kilimo na miundombimu zinatakiwa zitegemeanae na zifanye kazi pamoja ila haipo hivyo! hivyo kupelekea uchumi kutokuwa endelevu.
Nini kifanyikee?
i.Sekta zitegemeane ili kuleta uharaka wa maamuzi mfano mkilima akiwekeza basi kiwanda kiwe tayari kupokea malighfi na miundobinu iwe tayari kumrahisishia mkulima na kiwanda kusafirisha bidhaa na mazoa kwa haraka ili kuongeza uzalishaji na kuounguza mfumuko wa bei kutokana na kuchelwa kupata usafiri wa haraka kwa mazao na bidhaa.
ii. Tuwe na dira moja ya maendeleo ata akija raisi mpya hawezi pindisha mipango yetu kama nchi na pia kuwe na watendaji wanaosimamia dira mpak mwisho ata akija raisi mpya afuate dira moja ambayo itatufanya tuwe na uchumi endelevu kwa sasa na kwa badaye.
iii. Tupunguze ubadhirifu wa pesa za uma, kila mwaka Mkaguzi wa hesabu za serikali anakutana na ubadhirifu mkubwa na hatuoni sukuhisho , hii inpunguza kutofikia malengo kama nchi hivyo kutofikia malengo na kusababisha uchumi kudumaa.
Hitimisho
Kama nchi tunatakiwa tuwe tunafanya tathmini ya malengo kila mwaka na wahusika wawajibike ili kuhakikisha tunafikia malengo tunayojipangia kila mwaka na kwa baada ya miaka 5, 10 ,25 nk.
imeandikwa hassani ( Young economist)

Upvote
4