SoC02 Uchumi: Haja ya Serikali kupeleka wataalamu wa uchumi ngazi za kata na vijiji

SoC02 Uchumi: Haja ya Serikali kupeleka wataalamu wa uchumi ngazi za kata na vijiji

Stories of Change - 2022 Competition

Elias kastom

New Member
Joined
Jul 29, 2022
Posts
1
Reaction score
0
Uchumi limekuwa jambo ambalo kila taifa duniani linapambania, huduma nyingi za kijamiii zinatolewa ili watu wawe na wasaha wa kusonga mbele kiuchumi.

Vijiji vimekuwa na mchango mkubwa sana kukuza biashara za mijini, mfano mikoani kila mfanyabiashara huifurahia kazi yake wakati wa mavuno, hii inaonesha kuwa wananchi wa vijijini hufanya manunuzi kwa wingi nyakati hizo, kwa sababu wao ndio wenye ardhi ya kilimo. Lakini wananchi hawa hawana elimu ya kutosha ya namna gani wanaweza kuzalisha zaidi na kuzipa thamani inayoendana na ulimwengu huu wa sasa bidhaa zao.

Mfano kuna kata ina vijiji vitano lakini mtaalamu wa kilimo yupo mmoja na wa mifugo mmoja, ingali shughuli za kiuchumi eneo hilo ni kilimo na ufugaji, kwa kawaida mwananchi wa dalaja la chini kufunga safari kumfuata mtaalamu si jambo analoweza kulifanya kwa urahisi, labda awe amekumbwa na changamoto ya magonjwa kwa mifugo, na si kufuata elimu.

Iko haja ya kutazama katika kila kijiji ni shughuli gani inafanyika ili apelekwe mtaalamu wa shughuli hiyo na mtaalamu wa uchumi ili kuweka hali ya msawazo. Mfano kama sehemu inashuguli za madini, awepo mtaalamu wa madini kuwapa elimu watu wa eneo husika ni namna gani wafanye kazi yao kwa ubora zaidi na pia mtaalamu wa uchumi kuwapa elimu ni jinsi gani watumie kile wanacho kipata ili kuendana na dunia ya sasa kiuchumi.

Pia katika shughuli za kilimo na ufugaji, ni lazima raia wawe na wataalamu ili waweze kutoa bidha bora zinazo endana na wakati na pia mtaalamu wa kuwaelimisha ni kwa namna gani wanaweza kutumia kile wanacho kipata kipiga hatua.

Faida inayotokana na kuwasaidia wananchi wa hali ya chini kujiinua kiuchumi ni kuwaongezea uwezo wa wao kuweza kumudu ghalama za manunuzi ya mahitaji yao.

Mafano mvuvi atamudu ghalama za zana za kisasa za uvuvi, mkulima atamudu ghalama za pembejeo na zana za kisasa za kilimo, mfugaji atamudu ghalama za madawa na vifaa vya kisasa kwenye kazi yake, mchimbaji atamudu ghalama za vifaa vya kisasa vinavyo tumika kwenye uchimbaji ambavyo ni salama zaidi.

Matumizi yao yataenda kuwa na athari chanya ya moja kwa moja kwa wafanya biashara mijini hivyo kutakuwa na msawazo wa kiuchumi katika jamii. Pia wananchi hawa wa uchumi wa chini wataweza kumudu ghalama za elimu bora katika familia zao.

Kutokuwasaidia watu hawa ambao ni wengi sana kwa idadi kutafanya kuwe na kasi ndogo sana katika biashara nyingi nchini.
 
Upvote 0
Back
Top Bottom