Kwa uelewa wangu, JK anataka kuweka vivutio kwa wawekezaji wa ndani na nje. Hakuna mahali ambapo taarifa imeeleza kuwa wanaotakiwa ni wawekezaji wa nje tu.
Ukweli unabaki kuwa, hakuna nchi duniani ina/itakayopata maendeleo ya kweli bila uwekezaji na hasa katika viwanda.
Kinachotakiwa kwa serikali ni kuhakikisha kuwa nchi iko tayari ku-support uwekezaji huo kwa vitendo. Vile vile, serikali inatakiwa kuhakikisha kuwa wawekezaji pamoja na Taifa wananufaika na uwekezaji huo.
Uwekezaji wa ndani ndio uwekezaji wa maana kuliko ule unatoka nje, ambao mara nyingi unatushinda katika ku-negotiate terms.