Replica
JF-Expert Member
- Aug 28, 2017
- 1,681
- 8,887
Leo nimepita maduka kadhaa, kwenye shelf za maduka husika yamejaa mafuta ya kula yameandikwa Singida yakiwa yametengenezwa kwa zao la alizeti linalolimwa sana Singida. Hii imetokana na bei ya mafuta mengine kupaa hivyo watumiaji na wafanyabiashara kuamua kuhamia Singida, bei ya mafuta kutoka nje ingebaki kama awali pengine haya yasingeweza kufika hapa yalipo. Mahojiano yangu mafupi na muuza duka ni kwamba sasa yanatoka tofauti na zamani. Pamoja na maumivu ya bei kwenye sekta ya mafuta ya kula hasa kwa wananchi, upo upande chanya..
AJIRA
Mnyororo wa thamani katika utengenezaji wa mafuta haya ni mpana ikianza kwa wazalishaji wa mbegu, mashambani mpaka viwanda vidogo vidogo na kote huko watu wameajiriwa au kujiajiri. Uzalishaji wa mafuta nchini kuanzia mwanzo mpaka mwisho unarudisha ajira nchini ambazo awali tulikuwa tunazalishiwa na watu kutoka nje ya nchi. Kipato wanachopata walioajiriwa katika sekta hii wanazitumia nchini hivyo mnyororo kuwa endelevu kwenye bidhaa na sekta nyingine, upo uwezekano hata ndugu msomaji hela hizi kukutembelea bila kujua.
MATUMIZI YA FEDHA ZA KIGENI & KODI
Nchi inapunguza matumizi ya fedha za kigeni kununua mafuta nje ya nchi kwasababu sehemu kubwa wauzaji wanahitaji fedha ya Tanzania hivyo Serikali inaweza kuzitumia kwa mambo mengine ya maendeleo. Pia Serikali inaongeza wigo wake wa kodi mafuta yakizalishwa nchini, yakitoka nje wazalishaji wanalipa kodi kwenye nchi zao.
WAJASIRIAMALI WAPYA
Wafanyabiashara huwa wanaangalia kwenye faida na kufanya uwekezaji, mafuta ya alizeti ni uzalishaji, yanaweza kuwavuta wachuuzi wakawekeza huko badala ya kufanya udalali wa bidhaa kutoka nje ya nchi ambayo faida yake kwa Taifa ni ndogo. Pia wakulima, wazalishaji na wafanyabiashara wa alizeti kutoka Singida wataweza kukuza mitaji yao na kupanua nchi inavyonufaika.
KIAFYA
Ipo hoja ambayo sijaithibitisha kwamba mafuta haya ni mazuri kiafya, wananchi walio na afya njema ni nguvukazi nzuri kwa ujenzi wa Taifa na maendeleo yao binafsi. Lakini pia inapunguza matumizi ambayo taifa hutumia kuuguza na badala yake zinaweza kufanya mambo mengine aidha kwenye Serikali au Familia.
YAJAYO
Ni muhimu wizara za kilimo pia ya viwanda kuangalia namna ya kuifanya bei ya mafuta ya alizeti iwe chini, vita itaisha, covid itaisha na wazalishaji wa nje watarudisha uzalishaji na bei itashuka, mtanzania ni mtu wa kuangalia bei kabla ya mambo mengine hivyo kuleta uwezekano wa soko la mafuta ya alizeti kufa. Tuitumie vizuri ngekewa ya bei ya mafuta ya kula duniani kuongeza uzalishaji na kushusha bei.
Hii pia inahusu bidhaa zote zinazozalishwa nchini ambazo uzalishaji wake ulitetereshwa na bidhaa kutoka nje kama ngano na nyinginezo. Pia zipo zile ambazo matumizi yake yameongezeka baada ya bidhaa mbadala kutoka nje kupanda bei kama mihogo/viazi/maharage/supu kuwa mbadala wa chapati/maandazi(mafuta na ngano) pia tuziangalie kwa jicho chanya.