Uchumi kupanda katikati ya matatizo ya wadau ni ukatili dhidi ya wanaokutegemea

Uchumi kupanda katikati ya matatizo ya wadau ni ukatili dhidi ya wanaokutegemea

kavulata

JF-Expert Member
Joined
Aug 2, 2012
Posts
13,778
Reaction score
14,214
Familia inatumia fedha zaidi kutatua changamoto itakayompata mwana familia kama vile kwenye ugonjwa, msiba, ada, kesi, kubomoka kwa nyumba, nk. Kwenye matukio kama haya kipato cha familia kitapungua kidogo ili kuhudumia mwanafamilia apate nafuu.

Kama baba anaendela kuvua samaki baharini kukuza uchumi wakati mkewe amefariki dunia hiyo sio sawa, maana kila mtu atakushangaa sana.

Serikali inapotangaza kuimarika kwa uchumi katikati ya covid-19 na vita ya ukraine inamaanisha kuwa haikujali changamoto za watu wake. Mfano, inashangaza kuona serikali imegomba sana kuondolewa sh. 100 kwenye kodi ya mafuta ya magari ili kupeleka nafuu kwa wadau wake kati kipindi hiki cha hali ya dunia, kuna mtu hataki kuona fedha hazina zinapungua litoke jua inyeshe mvua, hii sio sawa.

Nchi zote za dunia uchumi wao umeyumba kwasababu ya covid 19 na vita ya ukraine kwasababu wanajali hali na maisha ya watu wao kwanza, lakini sisi kwetu raia wetu atajijua mwenyewe TRA mwendo mdundo tumalizie miradi ya mkakati.

Dunia itatushangaa sana kukosa huruma kwa watu wetu, hebu tutafute namna ya kusamehe baadhi ya kodi kwenye makusanyo ili kusaidia wananchi wapite salama kwenye kipindi hiki cha mpito.
 
Back
Top Bottom